Kushindwa kujizuia kujikojolea /kupitisha haja kubwa kwa wanawake. (vvf) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kushindwa kujizuia kujikojolea /kupitisha haja kubwa kwa wanawake. (vvf)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Mar 27, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kwa kitaalamu fistula hujulikana kama njia isiyo ya kawaida inayounganisha mfuko wa mkojo na uke, ambayo huruhusu mkojo na/au haja kubwa kutoka bila kujizuia kwenye kuta za uke.
  [​IMG]
  Nini hutokea?
  Tatizo la kushindwa kujizuia kujikojolea na/au kupitisha haja kubwa kwenye tupu ya mwanamke linalojulikana kama fistula hutokea baada ya mwanamke kupata madhara kipindi cha kujifungua kutokana na kuwa kwenye uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu (Prolonged and obstructed labor), kutokana na kichwa cha mtoto kushindwa kupita kwa urahisi kwenye tupu ya mwanamke.

  Hali hii husababisha tishu za kwenye tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na puru (rectum), kugandamizwa kati ya kichwa cha mtoto na nyonga za mwanamke. Hii husababisha mfumo wa damu kwenye tishu hizi kuharibika na tishu kukosa damu na kuwa katika hali inayojulikana kitaalamu kama ischemic necrosis. Baadaye tundu hutokea kati ya tupu ya mwanamke na kibofu cha mkojo au kati ya tupu ya mwanamke na puru.

  Matokeo yake ni mwanamke kutoa mkojo na/au haja kubwa bila kujizuia kupitia tupu yake (vagina).

  Ukubwa wa tatizo

  Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linakadiria kuwa wasichana na wanawake wapatao millioni 4 duniani wanaishi na tatizo hili wakati kila mwaka wasichana na wanawake wengine 50,000 - 100,000 hupatwa na tatizo hili.
  [​IMG]
  Fistula huonekana sana kwenye bara la Afrika na Asia ya kusini. Kwa Tanzania, wanawake na wasichana 1,200 kila mwaka hupatwa na tatizo hili. Katika tafiti mbili zilizofanyika Tanzania, iliripotiwa kuwa wanawake walio katika umri kati ya miaka 22-24 ndiyo hupatwa na tatizo hili zaidi.

  VVF husababishwa na nini?


  • Uchungu wa muda mrefu (Prolonged labour) ambao husababishwa na
   • Kutokuwa na usawa wa uwiano wa nyonga ya mama na ukubwa wa mtoto (CPD)
   • Mtoto kulala vibaya (malpresentation)
  • Upasuaji wa kuondoa kizazi (hysterectomy)
  • Upasuaji wa njia ya mkojo (repair of urethral diverticulum, electrocautery of bladder papilloma)
  • Upasuaji wa kansa za nyonga (pelvic carcinomas).
  Dalili

  • Mkojo kutoka bila kujizuia kwenye kuba ya uke ndio dalili muhimu
  • Kuna uwezekano wa kupata maambukizi hivyo dalili zifuatazo huweza kuambatana na dalili ya mwanzo homa na maumivu ya tumbo hasa ubavu na chini ya kitovu.
  Vipimo


  • Majimaji yanatoka kwenye kuta za uke huchunguzwa vitu vifuatavyo:
   • Urea, creatinine, na potassium ili kuwa na uhakika kuwa ni VVF na sio Vaginitis (maambukizi ya uke)
   • Mkojo huoteshwa kuangalia kama kuna vimelea na kujua dawa gani yaweza kuvimaliza vimelea hivyo
  • Rangi ya indigo carmine hutolewa kwa njia ya mshipa na pindi inapoonekana ukeni huthibitisha VVF
  • Cystourethroscopy
  • Intravenous urogram
  Matibabu

  [​IMG]
  Kama tatizo limegundulika siku chache baada ya upasuaji mpira wa kukojolea (urinary catheter either transurethral or suprapubic) huwekwa kwa siku 30. Fistula ndogo (chini ya sentimita 1) huweza kupona yenyewe au kupungua.

  Upasuaji ili kurekebisha VVF, aina za upasuaji:

  • Vaginal approach
  • Abdominal approach
  • Electrocautery
  • Fibrin glue
  • Endoscopic closure using fibrin glue with or without adding bovine collagen
  • Laparascopic approach
  • Using interposition flaps or grafts
  Baada ya upasuaji

  • Mgonjwa huwekewa Suprapubic catheter (mpira wa mkojo) kwa siku 6 hadi 60 ili kupunguza mvutano wa nyuzi
  • Vitamin C 500mg mara tatu kwa siku ili mkojo uwe wa asidi ili kuzuia maambukizi na kutengenezwa kwa mawe.
  • Tiba ya kichochezi cha ostrogeni kwa wakina mama walikwisha acha kupata siku zao (postmenopausal)
  • Dawa za kuzuia mshtuko wa mfuko wa mkojo-methylene blue na Atropine sulfate
  • Antibaotiki
  • Pumzisha nyonga kwa kuzuia tendo la ndoa kwa kipindi cha wiki 4 hadi 6. Ingawa wengine hushauri hadi miezi mitatu.
  • ​Kushindwa Kujizuia Kujikojolea /Kupitisha Haja Kubwa kwa Wanawake. (VVF)
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutoa elimu hii mkuu.
  Kuna kampeni kubwa sana hufanyika mara kwa mara, lakini hospitali ya CCBRT iliyopo msasani dsm inatoa matibabu bure kwa waathirika wa fistula. Endapo unakutana na mtanzania yeyote mwenye hilo tatizo, tafadhali msaidie kupata mawasiliano na CCBRT (unaweza ku-google kupata simu ama email). Mgonjwa anatumiwa nauli ya kwenda hospitali na gharama zote hadi za kumrudisha nyumbani kwake zinakuwa covered.
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ushachezewa kindumbwendumbwe wewe?
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  I was a smart kid b4 I was born NN, ila ww inaelekea ilikuwa ndo zako. Unacheza mpira ukilala hoi, hutaki usumbufu!
   
 5. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  asanate sana mkuuu kwa topic yako. najua watu engi wana tatizo hili, kitendo cha mtu Kushindwa kujizuia kujikojolea /kupitisha haja kubwa huitwa INCONTINENCE na fistula ni mojawapo ya sababu za mtu Kushindwa kujizuia kujikojolea /kupitisha haja kubwa, na hii si kwa wanawake tu, bali hata wanaume. kunasababu nyingi ambazo husababisha ugonjwa huu, mfano, kwa wanawake baada ya kuzaa watoto wakubwa, wenigne huzaliwa na fistula, magonjwa ya kuambukizwa katika njia ya mkojo, kuvimba au kuongezeka ukubwa kwa tezi za kiume (enlargement of prostatic gland), ugonjwa wa kiharusi, umri mkubwa, kisukari, unene (obesity), sphincter kushindwa kukaza (sphincter relaxation), umri mkubwa, multiple screlosis nk.
  Kuna kitu pia huitwa Coital incontinence. Ni kitendo cha mkojo kutoka wakati unapenyeza au unamwaga (orgasm) na hutokea wakati unafanya mapenzi au kupiga punyeto.
  Kuhusu FISTULA, zipo za aina nyigi za weza tokea katica mfumo wowote wa mwili mafano macho (lacrimal fistula, mzunguko wa damu, arteriovenus fistula n.k)
  matibabu ni kama ulivyo elezea kwa akina mama, lakini pia wanaweza tumia ajizi usafi (absorbent pads), diapers, undergaments,catheter (milija) nk
   
Loading...