Kushangilia kwa kupiga makofi msibani,ni utamaduni wetu?

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,065
Ndugu zangu nimestuka sana baada ya kuona jana kwenye TV wakati mwakilishi wa New Habari alipokuwa anatoa salamu za rambirambi toka kwa Rostam Aziz.
Alipotamka kuwa mke wa marehemu Danny atalipwa mshahara kwa miaka mitano sikuamini masikio yangu niliposikia makofi yakipigwa na pia ulipoelezwa utaratibu wa kusomesha watoto na dependants.
Nafsi yangu inashindwa kuona nafasi ya kushangilia kwa kupiga makofi msibani.Naamini mke wa marehemu na watoto wake hawakupiga makofi kwani kwao hakuna kitakachokuwa mbadala wa Danny.
Piili haya mambo ya kutoa msaada na kuutaja wazi kiasi kile nayo mmhhhhhh
 
Sio jambo la ajabu. Ila kinachonitatiza ni jinsi Rostam atakavyo-sustain utaratibu huo kwa wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo watakaofariki.
 
Are you a christian or a moslem? misiba ya kikristo huwa wanaimba na kupiga makofi coz kuna arusi 3 za mwanadamu, kuzaliwa, kuoa/kuolewa na kufa. Ina maana wewe hujawahi kuhudhria msiba wa kikristo hata mara moja? Na kama umehudhuria, hujawahi kuona nyimbo zikiimbwa na makofi kupigwa huu wa Danny ndio wa kwanza kwako? Danny ni mkristo, so makofi na uimbaji ni sehemu ya msiba si kitu cha kushangaza, sioni kosa hapo kwa kweli coz ni kawaida sana
 
Ndugu zangu nimestuka sana baada ya kuona jana kwenye TV wakati mwakilishi wa New Habari alipokuwa anatoa salamu za rambirambi toka kwa Rostam Aziz.Alipotamka kuwa mke wa marehemu Danny atalipwa mshahara kwa miaka mitano sikuamini masikio yangu niliposikia makofi yakipigwa na pia ulipoelezwa utaratibu wa kusomesha watoto na dependants.Nafsi yangu inashindwa kuona nafasi ya kushangilia kwa kupiga makofi msibani.Naamini mke wa marehemu na watoto wake hawakupiga makofi kwani kwao hakuna kitakachokuwa mbadala wa Danny.Piili haya mambo ya kutoa msaada na kuutaja wazi kiasi kile nayo mmhhhhhh
sasa asipotimiza ahadi mashaid watatoka wapi?
 
Sidhani kama ni utamaduni mzuri na pengine unaposema "wakristo" uelewe tupo several denominations. Kwangu sikubaliani nalo na sio jambo la kawaida. ni uzuzu wa aina fulani. Ni harusi ya tatu lakini ni ya huzuni tofauti na harusi ya 1 na ya 2. we have to make a difference.
 
Ndugu zangu nimestuka sana baada ya kuona jana kwenye TV wakati mwakilishi wa New Habari alipokuwa anatoa salamu za rambirambi toka kwa Rostam Aziz.
Alipotamka kuwa mke wa marehemu Danny atalipwa mshahara kwa miaka mitano sikuamini masikio yangu niliposikia makofi yakipigwa na pia ulipoelezwa utaratibu wa kusomesha watoto na dependants.
Nafsi yangu inashindwa kuona nafasi ya kushangilia kwa kupiga makofi msibani.Naamini mke wa marehemu na watoto wake hawakupiga makofi kwani kwao hakuna kitakachokuwa mbadala wa Danny.
Piili haya mambo ya kutoa msaada na kuutaja wazi kiasi kile nayo mmhhhhhh
Mkuu lazima uelewe ni nini kilichoshangiliwa. Kilichoshangiliwa siyo kifo cha Danny, hili ni jambo la huzuni. Na kwa sababu marehemu alikuwa anategemewa na familia yake financially kwa kusomesha watoto wake na wale wanaomtegemea na kwa huduma mabli mbali, kufariki kwake kulileta financial gap ambayo pengine wana familia waliobaki wasingeweza kuiziba ili watoto waendelee kusoma na familia kwa ujumla waendele kupata huduma kama mwanzo.Hii inafanya inafanya kuwe na majonzi mara 2; kuondokewa na mpendwa wao na kuwana ni jinsi gani wataweza kumudu maisha yao. Inapotokea mtu akajitokeza kusaidia mahitaji haya muda ambapo familia haijui itafanya nini kukidhi huduma hizi huwa ni jambo la furaha na halina budi kushangiliwa hata kama ni katikati ya majonzi.
 
I am a Moslem.
Naamini yangetumika maneno kama "Bwana Yesu asifiwe" yangekuwa na uzito kuliko kushangilia kwa makofi hasa yanapozungumzwa mambo ya fedha katika msiba.
Samahani ndugu zangu niliguswa na nsina nia ya kusahihisha dini za watu wengie.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom