Kushangalia kuna madhara makubwa, tujitathmini tuwe Wazalendo

FIKRA HAI

JF-Expert Member
May 22, 2013
231
79
Uchaguzi mkuu umepita, tumepata viongozi ambao tumewachagua na tunaamini kwamba misingi iliyowekwa na watangulizi na waasisi wa nchi itafuatwa!

Nachelea kusema kwamba hii tabia ya kuchekelea uchonganishi dhidi ya mataifa ya nje eti kwamba Uchaguzi wetu haukuwa haki ni Jambo Baya mnoo! Tumeshindwa kujifunza kutoka Kwa wenzetu wa Libya, Ivory coast na kwingineko!

Mataifa ya ulaya yanalinda masilahi yao dhidi ya watu wao, hawana uchungu na sisi hata kidogo, wanatamani tuanzea kupigana Vita wenyewe kwa wenyewe ili watuuzie silaha.

Prof. PLO Lumumba wa Kenya katika Moja ya mihadhara yake aliwahi kusema Vita vya makabila kule Ulaya wanaita Vita vya Kwanza vya dunia au Vita vya pili vya Dunia lakini huku Africa watasema Vita vya kikabila.

Tukiruhusu Vita au kuvamiwa na walowezi Kwa kisingizio chochote kile hatubaki salama daima, ni mwanzo wa kuvurugana na kuchinjina.

Nawaasa hasa vijana ambao tumejikuta tunashabikia na kuunga mkono machafuko, tujitathmini tuwe wazalendo Kama Raisi wetu, Serikali yoyote duniani haigawi hela. Ila hutengeneza mazingira Bora watu wake wafanye biashara yenye tija na kujipatia kipato halali kitu ambacho wazungu na vibaraka wao hawapendi.
 
UChaguzi mkuu umepita, tumepata viongozi ambao tumewachagua na tunaamini kwamba misingi iliyowekwa na watangulizi na waasisi wa nchi itafuatwa!...
Unatakiwa uwe Mzalendo Kwa nchi yako sio Kwa Mtu (Rais) au Serikali.

Nadhani hapo ndipo watu wengi tunapotofautiana. Mzalendo wa Kweli ni Yule anayetetea na kulinda maslahi mapana ya nchi yake na sio mtu au kikundi fulani.

Kuwa Mzalendo Kwa mtu ni Unafki hali inayopelekea kujikomba/kujipendekeza. Hivyo Rai yako ya kututaka tuwe wazalendo Kwa Mhe. Rais (Mtu) ni Batili mana ni kututaka tuwe wanafki.

Tunapaswa tuwe wazalendo Kwa Taifa letu na tulinde maslah ya nchi yetu dhidi ya wavunja Katiba na Sheria tulizojitungia.
 
Back
Top Bottom