Elections 2010 Kusema Mahanga Kashinda ni Matusi na Uzandiki

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Nchi hii imeoza kwa Rushwa.

Watawala wa nchi hii wanadharau sana wananchi.

Nina uhakika 100% Mahanga amepoteza kiti cha ubunge jimbo la Segerea. Lakini cha ajabu kabisa ametangazwa mshindi. Haya mambo hayatapita yakaachwa.

Hii ni dhulma.

Wanasegerea lazima tuchukue hatua mpaka matokeo yabatilishwe.
 
Na hii avatar yako ni inaonesha ni jinsi gani umechukia, ametangazwa kweli?
 
Na hii avatar yako ni inaonesha ni jinsi gani umechukia, ametangazwa kweli?

Ni kweli. Lakini kama mwananchi wa Segerea nimekereka sana.

Kuna mambo mengine yanafanyika ninafika mahali ninajiuliza: Hivi kweli Mungu yupo?
 
Na hii avatar yako ni inaonesha ni jinsi gani umechukia, ametangazwa kweli?

Ametangazwa kweli. Kura zake ziko mbali sana na Mpendazoe. Pia alikamatwa na masanduku ya kura! Watz tunadhalauriwa sana.
 
Mahanga ni mshenzi na mwizi, wanasegerea tuchuke hatua! Amekamatwa live na kura feki, anaoutoglu nako zimekamatwa, hiyo si kesi jamani?
 
Ni kweli. Lakini kama mwananchi wa Segerea nimekereka sana.

Kuna mambo mengine yanafanyika ninafika mahali ninajiuliza: Hivi kweli Mungu yupo?[/QUOTE]

Yupo na kwake hakuna zambi ndogo, akishuka kwa makongoro atatupitia na sisi pia. Ila malipo ya mwizi kama makongongoro yapo haha hapa dunia. Hasira ni za bwana
 
Ni kweli. Lakini kama mwananchi wa Segerea nimekereka sana.

Kuna mambo mengine yanafanyika ninafika mahali ninajiuliza: Hivi kweli Mungu yupo?

Usiwe na mashaka yupo na ulipa hapa duniani...subiri uone hao mashetani ya CCM kitakachowapata na shehe yahya wao
 
Mimi nafikiri Chadema waangalie utaratibu wa kufile appeal kesi mahakamni, and we will back them. Tuechoka kuburuzwa ka wendawazimu
 
Kama kweli amekamatwa na kura feki haki itapatikana mahakamani.Tume ya uchaguzi ni tawi la CCM na ufisadi na rushwa ni culture yao.Hii inauma sana halafu wanasema vyama vya upinzani vinavuruga amani na utulivu.Tume ya uchaguzi inapaswa kuvunjiliwa mbali na kuundwa tume huru.
 
mahanga oyeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!
mpenda kuzoa chaliiii!!!!!!!!!!
kip it up
 
Kura yangu mimi, familia yangu, majirani zangu na watu wote ninaofahamu hapa jimbo la segerea tulimpigia Mpendazoe, halafu asishinde?? hata wana CCm walikuwa wanasema hawawezi kumpigia maana alitukana eti wakazi wa Tabata ni kama Mabarmedi. Huyu Mahanga, wakala wa Mafisadi na mwizi wa mali za umma hawezi kuwa Mwakilishi wetu!! Hatumtaki wala hatukumchagua! Lazima ang'olewe kwa njia yoyote ile hata kama ni kumwaendea kwa sangoma!!! Ninaomba hata wale waliokuwa wamejipambanua ktk ccm kuwa ni wapambanaji dhidi ya ufisadi watuunge mkono kumng'oa fisadi pumbafu huyu!!!!
Come on S.Six
 
Anguko la roma lilianza kama utani. Watawala walipoambiwa habari za wananchi kutoridhika na mambo ya utawala wao hawakujali kwa kuwa walishinda kila vita ndani na nje wakitumia majambia na mapanga! Same thing happening to tanzania kwamba watawala wanapoambiwa hawatakiwi wanasema wanalinda amani maana hakuna mtu mwingine anayeweza kuilinda na ndipo wanapolazimisha kumtangaza mtu asiyehitajika kwa wananchi kwa madai ya kulinda amani.
je, hawafahamu kuwa amani inalindwa na mtu mmoja mmoja?
 
ndio maana bado siamini kama kwa mtindo huu tutapata haki katika kupiga kura....Mahanga ni jambazi alishafanya mpango kabambe wa kuiba kura zamani ,hata kwa vyovyote vile......ukitathmini ,asilimia kubwa ya wapiga kura wa segerea hawamtaki lakini still ameshinda....na bado atatuangamiza katika miaka mitano ijayo.....
sasa nini kifanyike?????
 
Ni kweli. Lakini kama mwananchi wa Segerea nimekereka sana.

Kuna mambo mengine yanafanyika ninafika mahali ninajiuliza: Hivi kweli Mungu yupo?

Mungu yuko kaka ila uwe na subira maangamizi makubwa kwao wafanyao dhuluma inakuja tena muda mfupi tu ujao na hili litakuwa ushuhuda kwako ili imani yako iongezeke.
 
Ee Mungu wa dunia yote wakiwemo Watanzania,
mambo haya yanatukatisha tamaa, pigana nao Mungu
wale wanaopigana na haki ya Watanzania, kwanini kila siku wao tuu
 
Nchi hii imeoza kwa Rushwa.

Watawala wa nchi hii wanadharau sana wananchi.

Nina uhakika 100% Mahanga amepoteza kiti cha ubunge jimbo la Segerea. Lakini cha ajabu kabisa ametangazwa mshindi. Haya mambo hayatapita yakaachwa.

Hii ni dhulma.

Wanasegerea lazima tuchukue hatua mpaka matokeo yabatilishwe.

Tumedharauliwa saaana, na hata baadhi yetu wanashirikiana na watawala kutubeza.

dawa ni kukata rufaa

Rufaa ya nyani utapeleka kwa ngedere???? Haisaidii.

Mahanga ni mshenzi na mwizi, wanasegerea tuchuke hatua! Amekamatwa live na kura feki, anaoutoglu nako zimekamatwa, hiyo si kesi jamani?

Watanzania tuchukue hatua.

Mungu yuko kaka ila uwe na subira maangamizi makubwa kwao wafanyao dhuluma inakuja tena muda mfupi tu ujao na hili litakuwa ushuhuda kwako ili imani yako iongezeke.

Dhuluma haitashinda , Watanzania TUTASHINDA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom