Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,204
- 12,700
Kumekuwa na haka kamsemo ka kizembe kuwa lengo kuu la chama cha siasa ni kushika madaraka. Huu ni upotoshaji. kwanza chama cha siasa ni kitu gani? chama cha siasa ni umoja wa watu wenye mawazo(Sera) zinazofanana juu ya kuendesha nchi. Mwanachama wa chama cha siasa lengo lake kuu ni kuona sera hizo zinafanyiwa kazi.
Mfano, mwanachama wa chama cha CDM anatamani kuona sera ya majimbo ikitekelezwa. Haijalishi CDM wapo madarakani au la. CDM ikishika madaraka na isitekeleze zile sera zilizokubaliwa na wanachama, malengo ya chama cha siasa yanakuwa bado hayajafikiwa.
Kuna njia nyingi za kufanya sera za chama zitekelezwe. Chama kinaweza kisiwe ndani ya madaraka lakini sera zake zikatekelezwa. Mfano ni jinsi sera ya ufisadi ya CDM ilivyofanyiwa kazi(Kwa sehemu kubwa) na serikali ya CCM. Hili la kusema lengo ni kushika madaraka ndiyo maana serikali inakataza siasa baada ya uchaguzi.
Lengo kuu la chama cha siasa ni kuona sera zake zinatekelezwa na si kushika madaraka.