X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
JF ni moja ya forum inayosomwa na watu wengi sana wenye kupenda mambo ya mtandao, kiasi ya kwamba nimesikia kuwa kuna baadhi ya waandishi wa habari wameifanya ndio chanzo chao cha habari nyingi zinazo jiri kila kukicha.
Nikatarajia kuwa Moderators ama viranja wanao simamia forum hii kuwa ni watu wapenda haki, waadilifu, wanaojali na kuheshimu uhuru wa kutoa maoni, kufuata na kutangaza misimamo ya kisiasa, kiitikadi na kiimani.
Nilidhani JF inachukizwa na vitendo vya Watanzania kuendelea kuwa kwenye mateso ya kiuchumi waliokuwanayo na wanapenda mabadiliko.
Vile vile nilitegemea kuwa JF wanavumilia katika kuto kukubaliana kimawazo, bila ya kutumia matusi, kejeli na vitisho kwa wale wanao sigana kihoja.
Nilitegemea kuwa wanachama watalindwa na kuvumiliwa mawazo yao.
Lakini ile thamani ya kuwa jukwaa huru la watu kuongea kwa uwazi haionekani humu! Jinsi ilivyo wenye kumiliki JF wanaimba kijamaa lakini wanacheza kibebari, je kwa mwenendo huu, tutafika tunako elekea?
Kujiunga kwangu kwenye hii forum ya Jamii, nilitegemea kujifunza mambo mengi na kupata mafundisho mengi yaliyo bora na yanayostahiki kuigwa na kila mwana jamii apendae maendeleo ya nchi yake au yake binafsi.
Hebu tutafakari na kujiuliza, hivi utapungukiwa kitu gani, ukijali na kutetea utaifa wako bila kujali itikadi za kisiasa na kiimani? Sasa tena mbona tunazibana midomo na kushikana mashati ili tusisogee kule tunapotarajia kwenda? Hivi hapa JF kuna wenye haki na wasio na haki kwenye kuzungumzia mustakabali wa nchi yetu? Refa anakamata jezi ya mchezaji, ili asiende kufunga, na baadhi ya watazamaji badala ya kushangaa wanashangilia...!
Ningependa tukumbushane kuwa; nchi hii ni yetu sote! Amani na utulivu havipatikani kwa kuwadhulumu, kuwakandamiza na kuwanyamazisha wengine halafu kutoa sababu zisizo za msingi! Na wala havitapatikana kuwa kuwapachika watu wanaodai haki zao kuwa wachochezi, wanatumiwa na majina mengine ya ajabu ajabu.
Haya hayatasaidia kitu! Ifahamike wazi kuwa amani na utulivu havipatikani katika nchi ambayo Katiba inakiukwa kila kukicha. Lakini mbona tunazibwa midomo pale tunapoamua kuzumngumza kwa uwazi? Kwannii lakini JF inajidharirisha kwa mambo ambayo yapo wazi kabisa?
Moderators wa JF wenyewe wanaonekana kujidhalilisha wenyewe katika hili. Nahisi na inawezekana hisia zangu zikawa za kweli, sitaki kuamini kuwa JF inafadhiriwa na serikali, na haya marumbano yote yasiyo na tija ndiyo yenye kuruhusiwa humu ndani.
JF ipo hapa kwa ajili ya hao mafisadi au wamefadhiliwa na sasa wanachukua nafasi hizo kulipa fadhila badala ya kuleta maendeleo yanayokusudiwa kwa nchi nzima bila kujali itikadi zao.
Sitaki kupandikiza hisia kuwa ile article yangu isemayo Vipi refa anapoamua kukwatua? inatishia usalama wa JF au kitaifa au inaingiliana na serikali, chama au dini. Kiasi ya kwamba imekuwa ni jinai ama kosa kubwa na nyeti sana kuwepo na watu wakapata wasaa wa kuchambua yaliomo, wakaamua kuinyofoa kabisa na kuweka kifungoni bila kuifikisha mahamani na bila maelezo yoyote yale. Hata pale nilipohamua kuwasiliana na Moderators kwa private message ili kujuwa kulikoni, sijajibiwa mpaka hivi sasa.
Hii ina maanisha kuwa hawana la kusema wala kujitetea maana haya na soni zimewakamata kisawa sawa kiasi ya kukosa majibu mwafaka.
Kuna msemo mmoja unasema hivi...
"LAKINI mtu anapokichukia kitu, haina maana kuwa lazima kitu hicho kiwe kibaya au hakifai. Huenda ikawa kasoro ni ya yule anayekichukia na siyo kile kinachochukiwa. Mwenye homa huweza akayachukia maji ya kunywa, yaliyo matamu na baridi, siyo kwa sababu maji hayo ni mabaya; bali ni kwa kuwa kinywa cha mgonjwa huwa ni chapwa, hakihisi ladha ya chakula hata kikiwa kitamu vipi!"
Nasikitika kusema kuwa JF imefikia hapa kiasi ya kukosa ladha! Yaani ni mchuzi uliokosa chumvi.
Ni matumaini yangu kuwa wanachama wachache sana miongoni mwetu wataendelea kusema kweli na kuchambua kwa ufasaha kila linalo jiri ili tupate kusonga mbele katika harakati za kuutetea utaifa wetu, bila kujali itikadi za kisiasa na kidini.
Japokuwa wataendelea kushikwa mashati na kukatwa ngwara (kukatwa mtama) (!?) na marefarii uchwala, lakini wasikate tamaa... ipo siku refarii atajisahau na kujifunga bao menyewe.
Niliambiwa zamani kuwa... kusema kweli ni sehemu ya uadirifu.
Ila uongozi wa JF uadilifu ni msamiati uliopitwa na wakati na hauna maana yoyote kwao...!
Nimepigwa ngwara...! Na nimenyanyuka tena na nitaendelea kusimama kidete, kila nitapo dondoka tena na tena...!