Kusema hakuna mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya Dkt. Magufuli ni kukosa akili

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,107
18,323
Kuna watu wataleta nyuzi za kishamba sana eti haoni mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya miaka 5 au 10 ya Dr Magufuli. Sisemei Dr Magufuli hajafanya kazi , la hasha, Kajitahidi na kachapa kazi ila Tanzania ina watu mil 58 , naamini kuna watu Zaidi ya mil 1 wanaoweza kufanya vizuri kwenye kiti cha Urais Zaidi ya Dr Magufuli.

Wengi wanaomzunguzia Dr Magufuli kama mungu ni washamba Fulani ambao hawana exposure ya kutosha na elimu yao ni ya chini sana. Lakini tatizo lao kubwa ni IQ yao kuwa chini sana below the bottom line .

Tanzania kukosa viongozi wazuri ni matokeo ya Katiba mbovu na matumizi mabaya ya vyombo vya dola ambavyo vinatumika kuua Demokrasia ambayo ndio njia sahihi ya kuwaona viongozi wazuri. Wengi wanahofu hata wamekata tamaa ya siasa kwa sababu ya vitisho vya wenye mamlaka wasio jali haki za binadamu hata ndani ya chama cha CCM.

Hata Nyerere aliimbiwa nyimbo kama hizi na maadhi ya wapumbavu na wasio na akili lakini mwishoni mwenyewe Nyerere akaona hatoshi. Laiti angekubali vichwa kama kina Kambona leo Tanzania ingekua moja ya nchi zenye uchumi bora na Imara Africa Zaidi ya Nigeria na South Africa.

Ethiopia imetawaliwa na Mawaziri wakuu wawili wakatili wasio jail haki za binadamu ,wao waliamini katika maendeleo ya mkono wa chuma nao si wengine ni Hailemariam Desalegn na Meles Zenawi.

Katika vipindi vyao haki za buinadamu zilizorota sana, waandishi wa Habari wengi walifungwa na kuteswa , wananchi wengi walikimbia nchi yao , wapinzania wangi wakaishia gerezani . Pamoja na maendeleo waliyo yaleta kama barabara, Ethiopia airlines, etc mwisho chama chao kikakiri hawahitaji viongozi wakatili wanao angalia maenmdeleo bila haki za binadamu , wanahitaji demokrasia, uhuru wa kuchagua, uhuru wa kuongea na kusikilizwa etc.

Hawa wote waliimbiwa manyimbo ya kipumbavu kama wanayo imba kima kessy, msukuma, lijuakali,Sanga na wapumbavu wengine bungeni wasio jitambua kutokana na IQ zao kuwa chini sana.

Baada yah hapo chama kikamleta kijana msomi na mwelevu Abiy Ahmed ambaye ameleta neema kwa watu wa Ethiopia, maendeleo anasimamia, uchumi unaenda kwa kasi, hata kisasi na mtu, vyama vya siasa vinafanya siasa, wandishi wanaandika mambo yao kwa uhuru, walio kimbia nchi yao wamerudi,mahakama zinafanya kazi zao kwa uhuru, vyombo vya dola vinasimamia haki sawasawa bila kumwonea mtu etc.

Ni lazima watanzania tuendelee kuzipuuza sauti za hawa wachumia tumbo, wasio na akili. Tanzania inauwezo wa kutoa viongozi ambao wanaweza kubadilisha nchi hii ndani ya miaka michache, ikawa nchi nzuri, yenye uhuru, yenye uchumi imara, yenye kujali haki za binadamu, yenye demokrasia etc.

Kumbuka: Wale waliokua nondo Olevel wakiamini wao ndio wenye akili Tanzania, Siku wameenda shule kama Ilboru , Mzumbe Kibaha, wakashangaa wanashika mkia.

Pongezi sana kwa Dr Magufuli na Marais wote waliopita,
Dr Magufuli fanya kazi yako ,sepaaaaa.
Wapo wengi wenye maono na Taifa hili.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania wote Mil 58.
 
Ingalikuwa tu endapo kungekuwa na uhuru wa vyombo vya habari kufanya mijadala huru na ya wazi kuhusu kukubalika kwa Mkulu, taasisi binafsi zingepata nafasi ya kufanya "fair opinion polls" juu yake, wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani na wanaharakati wangekuwa na uhuru wa kufanya shughuli zao bila ya mbinyo wowote wa vyombo vya dola pale wanapotoa madhaifu ya utendaji wa serikali yake.

Basi hapo angalau tungepata vigezo vya kumpa kongole zake anazozistahili zingalikuwa ni bayana. Vinginevyo hizi zote ni harakati za kujipendekeza tu kwake, hasa kwa wale wanufaika wa utawala wake.
 
Mleta mada usipate taabu kwani kikao cha kwamba bwana yule aendelee miaka 100 ijayo kimefanyikia Chuo Kikuu cha Milembe Lumumba Campus.
Watoa mada walikuwa wawili
1. Yule kichaa aliyechorewa mlango ubaoni akaambiwa aufungue akakubali hadi leo anatafuta ufunguo
2. Wa pili ni yule kichaa aliyekuwa hapigi kelele alipoulizwa mbona upo kimya akasema ame atamia mayai
Huyu aliyeileta humu kama thread ni huyo namba mbili
 
Back
Top Bottom