Kusamehe na kusahau

Daty

Senior Member
Jul 1, 2011
126
13
Ni kweli unaweza ukasamehe na ukasahau kutoka moyoni? Nimejaribu imenishinda. Wanajf nisaidieni njia ya kusamehe na kusahau kutoka moyoni
 
Ni kweli unaweza ukasamehe na ukasahau kutoka moyoni? Nimejaribu imenishinda. Wanajf nisaidieni njia ya kusamehe na kusahau kutoka moyoni

Huo ni msemo tu...hauna uhalisia wowote kwakweli...kuna mmoja wasema forgive your enemies but dont forget their names.
 
Ni kweli unaweza ukasamehe na ukasahau kutoka moyoni? Nimejaribu imenishinda. Wanajf nisaidieni njia ya kusamehe na kusahau kutoka moyoni
Inategemea uzito wa kosa lenyewe. Toa mfano wa kosa lenyewe.

Kuna makosa unaweza kusamehe na kusahau (vikosa uchwara)
Kuna makosa unaweza kusamehe lakini husahau (makosa yanayotibua hisia)

mwengine aendeleze......................
 
i never forget my friends.....i never forgive my enemies.........
 
kusamehe ni muhimu sana,tena sio kwako adui yako bali ni muhimu zaidi kwako.
1. Ukisamehe hata moyo wako unakuwa huru na unajiepusha na matatizo mbalimbali kama vile ugonjwa wa moyo kwa sababu unakuwa unaondoa hasira moyoni mwako. Pia inakuepusha na kumsababishia madhara aliyekukosea kwa mfano kuua,kujeruhi au kumdhuru kwa namna yoyote ile.
2. Unapalilia uhusiano wako na Mungu wako. Kwa sababu inatupasa kusamehe kwanza ili nasi tusamehewe dhambi zetu.
Kwa hiyo ndugu wewe muombe mungu wako akuwezeshe kusamehe. ''HAKUNA LISILOWEZEKANA CHINI YA JUA''
 
i never forget my friends.....i never forgive my enemies.........

You had better changed the last statement unless you don't want to be forgiven by God.
It's written,...

For if you forgive people their trespasses
[their reckless and willful sins, leaving them, letting them go, and giving up resentment],
your heavenly Father will also forgive you. Matthew 6: 14

Anyway,tumeamrishwa kusamehe mara moja pale tunapokosewa (ni amri)
Lakini haijaandikwa popote pale kwenye bible kwamba ukisha msamehe mtu
basi ni lazima umuamini,au umruhusu akuumize tena.

Samehe right away,usisubiri kuombwa msamaha.
Ni kazi ya aliye kukosea kukufanya umuamini tena.

Kwa mfano,nimetapeliwa na mshirika wangu kwenye biashara,nitamsamehe.
Akiomba msamaha,nitamwambia nimesha kusamehe toka zamani.
Lakini,sijaamrishwa popote kwamba niendelee kushiriki nae kwenye biashara,
kuendelea kushiriki nae ita maanisha namuamini bado,au kama simuamini basi
namruhusu aniumize tena.

Katika hali ya kibinadamu ni vigumu kusahau,lakini jitahidi kuomba ili usahau.God is faithful.

Lakini pia,ili usahau jitahidi kumpenda uliye kosana nae.
Upendo huondoa maumivu yote,huondoa uoga.
After all,utapata thawabu kwa Mungu ukimpenda uliyekosana nae.
(soma wafilipi2:1-2)

Ingawa hapo juu nimesema unaweza kuchagua kukaa nae mbali
ili asikuumize tena,hiyo ni option ya mwisho kabisa.

Kumbuka kwamba maisha ni "kujifunza jinsi ya kupenda",....life is all about learning to love.
(Unajifunza ili ukaoneshe wapi upendo wako,hilo ni somo lingine kubwa tu.)
Muumba wako anataka uthamini mahusiano yako na ndugu na marafiki wako wa kiroho
kwanza na kimwili pia.
Utapata thawabu kama utafanya juhudi kuwaleta karibu na wewe wale wote ulio kosana nao
kuliko kusamehe na kumtupilia mbali uliye kosana nae.
Chukua mfano wa Mungu,.....ukiomba msamaha,ingawa utaendelea kumkosea hakuachi upotee.

Kwa manufaa zaidi,jitahidi usome kwa makini na uelewa haya:-
Then Peter came up to Him and said, Lord,
how many times may my brother sin against me and I forgive him and let it go?
[As many as] up to seven times? Jesus answered him, I tell you, not up to seven times, but seventy times seven!
Matthew 18: 21-22
 
mfano: ulisafiri mkeo akakusaliti tena kwa kutembea na rafiki yako. Bahati nzuria au mbaya ukapata ushahidi na uthibitisho naye kweli akakiri kosa. Utamsamehe au hutamsamehe? Pili, huyo jamaa yako naye utamsamehe au hutamsamehe? Ni mkasa wa kweli uliotokea wee ungefanyaje?
 
Ni kweli unaweza ukasamehe na ukasahau kutoka moyoni? Nimejaribu imenishinda. Wanajf nisaidieni njia ya kusamehe na kusahau kutoka moyoni
<br />
<br />
siyo kila kosa linasameheka kirahisi na kusahaulika. utasamehe lakini hutaweza kusahau.
 
kweli kusamehe inategemea na kosa hata ukisamehe moyoni haliwezi kutoka litabaki maana mengine ni maudhi ya hali ya juu sana
 
Ni kweli unaweza ukasamehe na ukasahau kutoka moyoni? Nimejaribu imenishinda. Wanajf nisaidieni njia ya kusamehe na kusahau kutoka moyoni

mwenzetu umeshindwa nini? kusamaheh au kusahau au yote mawili?
Sijui nianzie wapi kabla sijapata ufafanuzi tajwa.................
 
Mimi nasamehe ila siwezi kusahau.
Ni rahisi kusamehe kuliko kusahau ila cha kufanya, usijipe hata muda kidogo wa kuwazia ulichotendwa. Ukiona mawazo hayo yanakuja tafuta jambo la kufanya ambapo akili yako itahamia huko.
Kama umeamua kumsamehe mtu, usiyafikirie mabaya yake. Jitahidi kufikiria mazuri yake maana unapofikiria mabaya hasira na chuki ni rahisi kujirudia hata kama ulisamehe.
Kama ni mpenzi wako alikukosea jambo kubwa ukamsamehe, jitahidi jambo lolote kama limekukwaza hata kama ni dogo umwambie mlitatue. Unapolimbikiza mauzi/kero ni rahisi kukumbuka na mauzi ya zamani na kujutia kwa nini ulimsamehe!
 
sometimes maisha ni kama vita...
kuna watu ukiwasamehe lazima watarudia tena kwa nguvu zaidi....

i dont forgive....i only let it go......
 
Forgiving is the best thing... Living with the one you have forgiven is another.... (thou depends on the mistake)
 
sometimes maisha ni kama vita...kuna watu ukiwasamehe lazima watarudia tena kwa nguvu zaidi....i dont forgive....i only let it go......
Unaweza kufafanua tofauti ni nini? Nafikiri ni bora mtu awasamehe waliomkosea aweze kuondoa kisasi na hasira moyoni mwake na kuwa na utulivu maishani mwake, lakini asisahau kamwe asije akakosewa tena.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom