Kusambaa kwa "mkataba" wa Buzwagi; kwa nini Serikali iko kimya?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Leo asubuhi kwenye kipindi cha "power breakfast" cha Clouds FM, watangazaji wawili wa kipindi hicho Masudi na Fina walimshangaa mwenzao Gerald HAndo pale alipojidai kuwa anao mkataba wa Buzwagi! Sababu ya kumshangaa mwenzao kujidai kuwa anao huo mkataba ni kuwa wao wanao siku nyingi na ya kuwa uko mitaani ukigawiwa kama njugu na kwa mjanja kama yeye ni aibu kutangaza kuwa ndiyo kwanza ameupata.

Hapa JF tunajidai tu kwa kusoma na kuujadili huo "mkataba" ambao serikali inadai kuwa mikataba ya madini ni "siri" kubwa.

Mwanzoni nilidhani serikali ingeng'aka na kukanusha kuwa huo si mkataba wa Buzwagi ambao umezua Buzwagigate bali ni mkataba feki wenye nia ya kuipaka matope serikali; lakini cha kushangaza ni kuwa Serikali inaingia JF na kuuona huo "mkataba" ambao wana JF tunajipatia bure na WaTZ tunatumiana tu kwenye mitandao popote duniani hadi kule kwenye Congress USA!

Hivi ni kwa nini serkali hadi sasa haijatoa tamko kuhusu huo "mkataba"? Maana mikataba ya madini ni siri kali na kwa kuvunjisha nyaraka za serikali ni kosa la jinai.

Why the government is silent? Maana kila wanapokwenda kujaribu kutetea Buzwagigate wanazomewa na huku wanadai kuwa mkataba wa Buzwagi ni kwa maslhi ya Taifa!

Ningependa Serikali ituambie Watanzania, hivi huo "mkataba" unaotandaa mtandaoni na mitaani ndiyo maktaba wenye maslahi kwa Taifa? Kama huo "mkataba" wa Mtandaoni nifeki mbona Serikali iko kimya hadi sasa?
 
Dr. Kafumu alisema hana uhakika km ndio weneyewe, mwingine alinukuliwa akisema wanamtafuta aliyeuvujisha. Hawajui kuwa aliyeuvujisha ni mTZ mwenye uchungu na wizi wa mafisadi kama Kara? Nafikiri wako kimya wakiangalia namna ya kuzima soo.... lakini imeshindikana na wameamua kubaki kimya!!!!!!
 
wanatafuta nitoke vipi hapo. Ni bora wakae kimya wajipange kwanza kabla ya kukurupuka maana watazidi kugawa point bure. ninawasiwasi kunawatu watapoteza hata kazi kwa sababu ya kuuvujisha. Kweli Tanzania ni kiboko. Kwani Castodian wamikataba ni nani? Watu hapo watatolewa kafara lakini bora kutolewa kafara kwa sababu ya uchungu na nchi yako.
 
Dr. Kafumu alisema hana uhakika km ndio weneyewe, mwingine alinukuliwa akisema wanamtafuta aliyeuvujisha. Hawajui kuwa aliyeuvujisha ni mTZ mwenye uchungu na wizi wa mafisadi kama Kara? Nafikiri wako kimya wakiangalia namna ya kuzima soo.... lakini imeshindikana na wameamua kubaki kimya!!!!!!

Alah! Wanatafuta aliyeuvujisha? Wameingia mkenge hawataweza kuukana tena.

I think their time is very imminent; hawataweza kuponyoka tena. Naamini mikataba itaendela kuvuja na tutaona mengi and in 2010 wataanza kupata majibu.
 
Wameziasi fikra za mwalimu wamekosa pa kushikilia,wao kama wao hawana uwezo wa kukataa hizo tuhuma sababu zinawahusu moja kwa moja,wanamsubiri Muungwana arudi toka ufaransa ambako anapata matibabu ya maradhi yanayomsumbua kwa muda sasa,
atakuja kuuza sura na kutoa mwelekeo wa serikali yake,

sababu ya pili wanajua katiba inatoa uhuru wa maoni na inakataza sheria yoyote kukiuka katiba(sheria ya usalama wa taifa 1970).

angalia ibara ya 30 kifungu cha 5
"endapo katika shauri lolote linalodaiwa kwamba sgeria yoyote iliyotungwa au hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali au mamlka nyingine inafuta au inakatika HAKI,UHURU NA WAJIBU muhimu zitokanazo na ibara ya 12 hadi ibara ya 29 za ktiba hii,mahakama kuu inaridhika kwamba sheria au hatua inayohusika,kwa kiwangi kinachopingika na katiba ni BATILI au kinyume cha katiba basi mahakama kuu ikiona yafaa au hali au maslahi ya jamii yanahitajika hivyo,badala ya kutamka kuwa sheria au hatua hiyo ni batili,itakuwa na uwezo wa kuamua fursa kwa ajili ya serikali au mamlaka nyingine yoyote inayohusika kurekebisha hitilafu iliyopo katika sheria inayotumiwa au hatua inayohusika katika muda na kwa jinsi itakavyotajwa na mahakama kuu,na sheria hiyo au hatua inayohusika itendelea kuhesabiwa kuwa ni halali hadi ama marekebisho yatakapofanywa au muda uliowekwa na mahakam kuu utakapokwisha,mradi muda mfupi zaidi ndio uzingatiwe"

ibara ya 12 hadi ya 29 zinazungumzia haki ya usawa,usawa mbele ya sheria,haki ya kuwa hai,haki ya uhuru wa mtu binafsi,haki ya faragha na usalama wa mtu,uhuru wa mtu wa kwenda atakako,UHURU WA MAONI,UHURU WA KUSHIRIKIANA NA WENGINE,uhuru wa kushiriki shughuli za umma ,haki ya kufanya kazi,haki ya kumiliki na kulinda mali ya umma,ulinzi wa taifa

ndio maana kina karagamagi wanatishia kwenda mahakamni ila wanajua watashindwa,

mapambano ya kifikra yanaendelea,mpaka sheria ya usalama wa taifa ibatilishwe!watanzania wa sasa sio wa mmiaka ya 70
 
Baada ya dhiki faraja,

Kwa Tanzania ya sasa msemo huo unabadilika, BAADA YA DHIKI NI DHIKI KUU
 
Kwani Mkataba Si Umevuja Kwa Wananchi Ambao Ndo Stake Holders Ktk Ilo Kuna Tatizo Gani.ukimya Wa Serikali Ni Kwamba Wanaona Soo Namna Ya Kuutetea Huo Mkataba Bse Jinsi Ulivyo Ni Kimeo.ungekuwa Uko Sawa Zamani Watu Wangewajibishwa.
 
Mimi naona mkataba haujavuja bali umerudi kwa wenyewe (sisi wananchi) ili tukae na kunadili tuone ni kwa jinsi gani hao watu tuliowatuma (Karamagi,Muungwana et al)kwenda kusign mikataba badala yetu wanalinda maslahi yetu.Kwa hiyo hapa hakuna cha kuvuja kwa mkataba wala nini,swala ni kuwa mikataba imerudi kwetu na bado mingine tunaitaka...ole wao mafisadi siku zao zimekaribia...
 
walipokuwa wakisema mikataba ni siri, walikuwa wanataka kututia mchanga wamacho wananchi.

mikataba ni mali ya umma, lazima nipatiwe, kama si raia wa kawaida basi angalau wabunge wetu.

mbunge hawezi kukataliwa kupewa mkataba.
 
mikataba ni mali ya umma, lazima nipatiwe,

It does not matter, tunao mkataba wa Buzwagi anyway so what? Liwalo na liwe tunao Karamagi akale chupa if he may, kwani serikali ni wajinga kuwa hawajui kuwa hili sooo linaanzia huko huko ndani CCM?

Unapoanza kuwakamata wabunge kuwa ni wala rushwa ulitegmea nini? Unapomfukuza Mahalu peke yake kuwa ni mwizi wakati wezi wakubwa wanajulikana ulifikiri itakuwaje? Unafikiri walipomuita Muungwana kule kamati kuu na kumuomba aimalize ile kesi ya wabunge ama sivyo hakutakalika unafikiri walikuwa wanatania?

Kifo cha panzi hiki mwanangu, believe me huu ni mwanzo tu, mengi yanakuja, yaani wananchi wamechoka mpaka kwenye TV zetu vijana wa kibongo wanasema wazi tu kuwa na mimi mninao mkataba wa Buzwagi, now wasup with that? Kwani usalama hawakuwaona hao watangazaji,


Enough na ufisadi hata mimi ninao mkataba wa Buzwagi, let the chips fall where they may!
 
Ni jukumu la rais ambaye amepewa rungu kulitumia hivi sasa na kufuta mikataba yote uchwara NOW and then tuanze kutafakari what next. Bila kusahau kuwaondoa vibaka kwenye serikali.
 
JAMANI gazeti la THISDAY la leo Kurasa nne za ndani zimewekwa mkataba wote wa BUZWAGI, mbele wameweka, "EXCLUSIVE... Full text of Buzwagi Contract inside!" uko page 15, 16, 17 na 18" na katika gazeti la KULIKONI ukurasa wa kwanza kuna habari kuu, "Mkataba wa Buzwagi sasa Kwenye Mtandao"..... wakinukuu sehemu kubwa ya JF... ile iliyowekwa na CMB, BRAVO JF...... Awali ilikua JF inanukuu magazeti, leo magazeti yananukuu JF, kesho na keshokutwa serikali, bunge, mahakama watanukuu JF, itazidi kuwa chombo muhimu kwa maslahi ya TAIFA
 
Mkataba wa Buzwagi haujavuja, sema umefika kwa wamiliki wake wakuu, ambao ndio sisi.
 
Mstari unachorwa ardhini, na watawala wetu wajue kuwa hawatauvuka tena! Sheria ya Usalama wa Taifa ya 1970 ni sheria ambayo kwa dhamiri safi siwezi kuitii!!
 
Ndio gharama za utandawazi hizo, ukishaukubali utandawazi uwe tayari kupokea na madhara yake. vyote vilivyofichika huko nyuma itajulikana. let's wait and see
 
Halisi

Awali ilikua JF inanukuu magazeti, leo magazeti yananukuu JF, kesho na keshokutwa serikali, bunge, mahakama watanukuu JF, itazidi kuwa chombo muhimu kwa maslahi ya TAIFA

Mkuu Halisi,

Hapa chini ni utabiri nilioutoa mwezi August 11, 2007:-

Mwisho naomba nimalizie na my dream, I have a dream kwamba hii forum itakuwa chombo kikali na kikubwa sana kwa taifa, kisiasa katika kupima uwezo wa viongozi wa taifa letu huko siku za mbele, katika kupima na kupata ukweli wa ishu muhimu za taifa letu. Wanachama wote watakuwa wakiingia kwa majina yao kamili, na taifa zima litaipigia magoti hii forum siku za karibuni kwa sababu kitakuwa ndicho chombo pekee ambacho wananchi watakuja kupata ukweli wa mambo muhimu ya taifa letu. Na pia kitakuwa ndio thermometer muhimu ya taifa letu katika kupima na kupitisha maamuzi muhimu ya taifa letu, na ni kiongozi atakayekubalika na hii forum, ndiye atakayechaguliwa au kupita katika uchaguzi wowote wa kisiasa ndani ya taifa letu, I am sold na this dream that I am betting it with my life!

Mungu Aibariki Hii Forum, na Wanachama Wake Wote!, kwa sababu we are doing God's work kwa kuwaongelea wanyonge wasioweza kujiongelea wenyewe! God is kool with that!


In the wake ya yanayoendelea sasa, nafikiri hatuko mbalia sana na huu ukweli!
 
Mkuu Halisi,

Hapa chini ni utabiri nilioutoa mwezi August 11, 2007:-

Mwisho naomba nimalizie na my dream, I have a dream kwamba hii forum itakuwa chombo kikali na kikubwa sana kwa taifa, kisiasa katika kupima uwezo wa viongozi wa taifa letu huko siku za mbele, katika kupima na kupata ukweli wa ishu muhimu za taifa letu. Wanachama wote watakuwa wakiingia kwa majina yao kamili, na taifa zima litaipigia magoti hii forum siku za karibuni kwa sababu kitakuwa ndicho chombo pekee ambacho wananchi watakuja kupata ukweli wa mambo muhimu ya taifa letu. Na pia kitakuwa ndio thermometer muhimu ya taifa letu katika kupima na kupitisha maamuzi muhimu ya taifa letu, na ni kiongozi atakayekubalika na hii forum, ndiye atakayechaguliwa au kupita katika uchaguzi wowote wa kisiasa ndani ya taifa letu, I am sold na this dream that I am betting it with my life!

Mungu Aibariki Hii Forum, na Wanachama Wake Wote!, kwa sababu we are doing God's work kwa kuwaongelea wanyonge wasioweza kujiongelea wenyewe! God is kool with that!


In the wake ya yanayoendelea sasa, nafikiri hatuko mbalia sana na huu ukweli!

Ubarikiwe sana na mungu akusaidie kwa maneno yako mazuri, nimekukubali mkuu AMEN
 
juhudi za jambo forum kuipeleka nchi yetu katika nchi ya ahadi uko mbioni kufanikiwa.
najua Muungwana atakuwa anajiuliza afanye nini kurudisha credibility yake aliyopetozwa na karamagi,EL,Msolla,Balali,Chenge,Masha,Msabaha,rutabanzibwa,Mkono,mgonja,ZM,buriani.
Mhe. kikwete unasubiri nini kuwaondoa hawa watu?au unasubiri tuanze kukung'oa wewe mwenyewe 2010?
 
Back
Top Bottom