Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 530
Leo asubuhi kwenye kipindi cha "power breakfast" cha Clouds FM, watangazaji wawili wa kipindi hicho Masudi na Fina walimshangaa mwenzao Gerald HAndo pale alipojidai kuwa anao mkataba wa Buzwagi! Sababu ya kumshangaa mwenzao kujidai kuwa anao huo mkataba ni kuwa wao wanao siku nyingi na ya kuwa uko mitaani ukigawiwa kama njugu na kwa mjanja kama yeye ni aibu kutangaza kuwa ndiyo kwanza ameupata.
Hapa JF tunajidai tu kwa kusoma na kuujadili huo "mkataba" ambao serikali inadai kuwa mikataba ya madini ni "siri" kubwa.
Mwanzoni nilidhani serikali ingeng'aka na kukanusha kuwa huo si mkataba wa Buzwagi ambao umezua Buzwagigate bali ni mkataba feki wenye nia ya kuipaka matope serikali; lakini cha kushangaza ni kuwa Serikali inaingia JF na kuuona huo "mkataba" ambao wana JF tunajipatia bure na WaTZ tunatumiana tu kwenye mitandao popote duniani hadi kule kwenye Congress USA!
Hivi ni kwa nini serkali hadi sasa haijatoa tamko kuhusu huo "mkataba"? Maana mikataba ya madini ni siri kali na kwa kuvunjisha nyaraka za serikali ni kosa la jinai.
Why the government is silent? Maana kila wanapokwenda kujaribu kutetea Buzwagigate wanazomewa na huku wanadai kuwa mkataba wa Buzwagi ni kwa maslhi ya Taifa!
Ningependa Serikali ituambie Watanzania, hivi huo "mkataba" unaotandaa mtandaoni na mitaani ndiyo maktaba wenye maslahi kwa Taifa? Kama huo "mkataba" wa Mtandaoni nifeki mbona Serikali iko kimya hadi sasa?