Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Mimi kama mwananchi wa kawaida,nashauri uchukue hatua zaidi katika kudhibiti kusambaa kwa huu ugonjwa ambapo sasa tunaambiwa kuna jumla ya wagonjwa 46, vinginevyo wewe na serikali yako mnaweza kuja kubeba lawama kuwa hamkuchuka hatua za kutosha katika kupambana na huu ugonjwa ikitokea hali inakuwa mbaya(Mungu apishie mbali).
Mhe.Raisi,kama sikosei,ilikuwa ni March 13 mwaka huu tulipotangaziwa mgonjwa wa kwanza wa Corona hapa nchini, hivyo ndani ya siku 30, tayari tumepata wagonjwa 46.Idadi/kasi hii si ndogo na tukumbuke sasa tumeingia katika kile kinachoitwa community transimission.
Hivyo,pamoja na hatua serikali yako ilizochukua mpaka sasa,napendekeza hatua zaidi ambazo ni hizi zifuatazo:
Zuia ibada zote kuanzia sasa
Mhe.Raisi,mikusanyiko na mikusanyiko tu na madhara yake katika kusambaza gonjwa hili yatabaki kuwa ni yale yale hivyo ni bora kuzuia Ibada kwa muda ili kulinda afya na uhai wa watu.
Tunaweza kuzuia Ibada kwa muda na baadae zikaendelea ila uhai wa mtu ukipotea,hakuna namna ya kuurudisha na tutambue madhara ya vifo vya wananchi ni pamaja na kutapoteza nguvu kazi ya Taifa inayotakiwa kutekeleza kauli mbiu yako ya 'hapa kazi tu".
Kingine,Ibada za Pasaka katika baadhi ya makanisa zimedhihirisha kuwa social distancing haiwezekani katika nyumba zetu za Ibada na hizi picha ni ushahidi tosha wa hali hii.
Hii ni hali katika kanisa la KKKT Ushariki wa Mjini Dodoma katika Ibada ya Pasaka siku ya jana.
Zuia mikusanyiko katika mabaa na sehemu zingine
Mhe.Raisi,kwenye mabaa na sehemu nyinginezo mikusanyiko bado ipo japo inawezekana imepungua.Nachokushauri, piga marufuku mikusanyiko kwenye mabaa na wakati huo huo, unaweza kuruhusu bar hizi kuuza pombe kwa mashariti ya mtu kwenda kunyewea nyumbani kwake na si baa.
Shauriana na Spika wa Bunge,Bunge lisitishwe
Mhe.Raisi,nakushauri ukutane na viongozi wa Bunge na mkubaliane kusitisha shughuli/vikao vya Bunge kwa muda ili kukabiliana nan huu ugonjwa.
Mhe.Raisi,uwepo tu wa wabunge na shughuli za Bunge mkoani Dodoma, maana yake ni kuwataka watu wasio wabunge ila wanaopaswa kuja Bungeni(mfaano maafisa wa serikali na madereva wao,n.k) nao wafike Dodoma kwa shughuli zinazohusiana na Bunge hivyo kuongeza muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Swali lingine ni kuwa,wabunge wetu hawa siku za mwisho wa wiki husafiri kurudi Dar,majimboni mwao na kwingineko hivyo wanaweza kabisa kuchangia katika kusambaza maambukizi unless wabunge wote wazuiwe kusafiri mpaka Bunge liishe na kama kusafiri basi iwe kwasababu maalumu.
Wafanyakazi wa umma wasio na ulazima wabakie majumbani
Mheshimiwa,nashauri ikiwezekana kuanzia Jumatatu iyayo au hata kabla ya hapo watumishi wote wa umma wanaoweza kubaki majumbani wabaki na wanaoweza kufanya kazi zao kutokea majumbani mwao waruhusiwe kufanya hivyo.
Kwa mfano,walimu wa shule na wahadhiri wa vyuo wabakie majumbani badala ya kutakiwa kuendelea kuripoti makazini
Nauli za mabasi na ndege kwenda na kutoka Dar-es-Salaam ziongezwe kwa asilimia 100
Kwakuwa Dar-es-Salaam kwa sasa ndio kituvo cha ugonjwa huu,nashauri serikali iongeze nauli za kusafiri kwenda na kutoka Dar-es-Salaam kwa asilimia mia moja au hamsini ili ku-discourage movement zisizo za lazima.
Naelewa kuna watu wanaweza kulalamika ila watanzania tutambue wenzetu katika nchi nyingine wako katika lockdown hivyo hii yetu bado inaweza kuwa ni nafuu ukilinganisha na kinachoendelea katika mataifa mengine.
Vile vile fedha inayozidi baada ya nyongeza hiyo ya nauli ipelekwe serikalini katika mfuko wa kupambana na corona(naamini mfuko huo upo na kama haupo,basi ni wakati muafaka uanzishwe).
Hata hivyo,ningependa kutoa ushauri wa ziada kuwa kwa wale wenye safari za lazima kwenda au kurudi Dar waruhusiwe bila kutozwa gharama ziada ila iwe ni baada ya wahusika kutoa vithibitisho maalumu mfano kuonyesha barua ya rufaa kwenda Muhimbili kwa walio wagnjwa,n.k.
Nauli za kutoka na kwenda mikoa miingine iongezwe kwa asilimia 50
Hapa lengo likiwa ni lilelile la ku-discourage movements zisizo za lazima humu ndani ya nchi kama njia mojawapo ya kudhibiti kusambaa kwa COVID-19.
Nasema haya kwasababu bado baadhi yetu hatuko serious sio katika kunawa tu,bali bado wako watu wanaosafiri kwenda kusalimia ndugu,jamaa na marafiki.
Hela zote zitazopatikana kutokana na ongezeko hili la nauli zielekezwa serikalini katika kupambana na huu ugonjwa.
Hata hivyo,bado nasisitiza safari za lazima ziruhusiwe ila cha msingi tuwe na udhibiti vinginevyo gonjwa hili linaweza kuja kutuelemea huko mbeleni.
Serikali itoe ruzuku kwa viwanda vinavyotengeneza sanitizer/hand wash humu nchini
Katika kuhamsisha matumizi ya vitakasa mikono na kuwapunguzia watu gharama za kununua hizi sanitizer,napendekeza serikali itoe ruzuku kwa viwanda vyote vinavyozalisha bidhaa hii ili kupunguza bei ya bidhaa hii ndani ya nchi yetu.
Serikali ipunguze kodi ya kuzalisha na kuagiza vitakasa mikono
Vile vile serikali inaweza kuvipunguzia kodi viwanda vinavyozalisha hii bidhaa pamoja na kupunguza kodi ya kuingiza vitakasa mikono humu nchini lengo likiwa ni kushusha bei ya bidhaa hii muhimu katika kupambana na COVID-19.
Miradi yote mikubwa na midogo isitishwe kwa muda
Mhe.Raisi,ni vizuri na ni bora ukaagiza kusitishwa kwa miradi yote mikubwa na midogo nchi nzima mpaka pale hali ya maambukizi itakopkuwa imekwisha kwani shughuli za hii miradi zinachangia sana movement na muingiliano wa watu kuanzia wafanyakazi wa hii miradi pamoja na wale wote wanaopata riziki kupitia miradi hii bila kusahau ndugu na jamaa zao wanaowaacha huku majumbani mwano pamoja na wale wanaokutananao huko mitaa wanakoishi baada ya kutoka makazini/vibaruani..
Mhe. Raisi,hizo hapo juu ni baadhi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa na serikali yako ila bado wataalamu wanaweza kuziboresha na hata kushauri njia nyingine bora zaidi ambazo mimi hapa sijazitaja.
Naelewa kabisa ugonjwa huu hapa nchini unaweza usilete madhara makubwa kulingana na hofu iliyopo lakini tutambue hii bado ni probability hivyo ni bora tuchukue tahadhari mapema kama ambavyo ni bora kuamini Mungu yupo, kuliko kutoamini yupo alafu ukaja kutananae huko Mbinguni.
Mwisho,tutambue kote wanakotangaza kufanikiwa kupunguza maambukizi,mfano China na sasa Italy, hawa wote walilazimika kuchukua maamuzi magumu zaidi ya haya nayopendekeza hivyo na sisi ni lazima tuwe tayari kuji-sacrifice kabla ya kutegemea ushindi dhidi ya hili gonjwa.
Tutambue pia sisi ni masikini sawa na yatima asietakiwa kudeka.