Kusambaa kwa corona: Rais Magufuli nakuomba uchukue hatua hizi na nyinginezo utakazoshauriwa na wasaidizi wako vinginevyo unaweza kuja laumiwa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
42,919
2,000
Mimi kama mwananchi wa kawaida,nashauri uchukue hatua zaidi katika kudhibiti kusambaa kwa huu ugonjwa ambapo sasa tunaambiwa kuna jumla ya wagonjwa 46, vinginevyo wewe na serikali yako mnaweza kuja kubeba lawama kuwa hamkuchuka hatua za kutosha katika kupambana na huu ugonjwa ikitokea hali inakuwa mbaya(Mungu apishie mbali).

Mhe.Raisi,kama sikosei,ilikuwa ni March 13 mwaka huu tulipotangaziwa mgonjwa wa kwanza wa Corona hapa nchini, hivyo ndani ya siku 30, tayari tumepata wagonjwa 46.Idadi/kasi hii si ndogo na tukumbuke sasa tumeingia katika kile kinachoitwa community transimission.

Hivyo,pamoja na hatua serikali yako ilizochukua mpaka sasa,napendekeza hatua zaidi ambazo ni hizi zifuatazo:

Zuia ibada zote kuanzia sasa
Mhe.Raisi,mikusanyiko na mikusanyiko tu na madhara yake katika kusambaza gonjwa hili yatabaki kuwa ni yale yale hivyo ni bora kuzuia Ibada kwa muda ili kulinda afya na uhai wa watu.

Tunaweza kuzuia Ibada kwa muda na baadae zikaendelea ila uhai wa mtu ukipotea,hakuna namna ya kuurudisha na tutambue madhara ya vifo vya wananchi ni pamaja na kutapoteza nguvu kazi ya Taifa inayotakiwa kutekeleza kauli mbiu yako ya 'hapa kazi tu".

Kingine,Ibada za Pasaka katika baadhi ya makanisa zimedhihirisha kuwa social distancing haiwezekani katika nyumba zetu za Ibada na hizi picha ni ushahidi tosha wa hali hii.

Hii ni hali katika kanisa la KKKT Ushariki wa Mjini Dodoma katika Ibada ya Pasaka siku ya jana.

1586775784009.png

Zuia mikusanyiko katika mabaa na sehemu zingine
Mhe.Raisi,kwenye mabaa na sehemu nyinginezo mikusanyiko bado ipo japo inawezekana imepungua.Nachokushauri, piga marufuku mikusanyiko kwenye mabaa na wakati huo huo, unaweza kuruhusu bar hizi kuuza pombe kwa mashariti ya mtu kwenda kunyewea nyumbani kwake na si baa.

Shauriana na Spika wa Bunge,Bunge lisitishwe
Mhe.Raisi,nakushauri ukutane na viongozi wa Bunge na mkubaliane kusitisha shughuli/vikao vya Bunge kwa muda ili kukabiliana nan huu ugonjwa.

Mhe.Raisi,uwepo tu wa wabunge na shughuli za Bunge mkoani Dodoma, maana yake ni kuwataka watu wasio wabunge ila wanaopaswa kuja Bungeni(mfaano maafisa wa serikali na madereva wao,n.k) nao wafike Dodoma kwa shughuli zinazohusiana na Bunge hivyo kuongeza muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Swali lingine ni kuwa,wabunge wetu hawa siku za mwisho wa wiki husafiri kurudi Dar,majimboni mwao na kwingineko hivyo wanaweza kabisa kuchangia katika kusambaza maambukizi unless wabunge wote wazuiwe kusafiri mpaka Bunge liishe na kama kusafiri basi iwe kwasababu maalumu.

Wafanyakazi wa umma wasio na ulazima wabakie majumbani
Mheshimiwa,nashauri ikiwezekana kuanzia Jumatatu iyayo au hata kabla ya hapo watumishi wote wa umma wanaoweza kubaki majumbani wabaki na wanaoweza kufanya kazi zao kutokea majumbani mwao waruhusiwe kufanya hivyo.

Kwa mfano,walimu wa shule na wahadhiri wa vyuo wabakie majumbani badala ya kutakiwa kuendelea kuripoti makazini

Nauli za mabasi na ndege kwenda na kutoka Dar-es-Salaam ziongezwe kwa asilimia 100
Kwakuwa Dar-es-Salaam kwa sasa ndio kituvo cha ugonjwa huu,nashauri serikali iongeze nauli za kusafiri kwenda na kutoka Dar-es-Salaam kwa asilimia mia moja au hamsini ili ku-discourage movement zisizo za lazima.

Naelewa kuna watu wanaweza kulalamika ila watanzania tutambue wenzetu katika nchi nyingine wako katika lockdown hivyo hii yetu bado inaweza kuwa ni nafuu ukilinganisha na kinachoendelea katika mataifa mengine.

Vile vile fedha inayozidi baada ya nyongeza hiyo ya nauli ipelekwe serikalini katika mfuko wa kupambana na corona(naamini mfuko huo upo na kama haupo,basi ni wakati muafaka uanzishwe).

Hata hivyo,ningependa kutoa ushauri wa ziada kuwa kwa wale wenye safari za lazima kwenda au kurudi Dar waruhusiwe bila kutozwa gharama ziada ila iwe ni baada ya wahusika kutoa vithibitisho maalumu mfano kuonyesha barua ya rufaa kwenda Muhimbili kwa walio wagnjwa,n.k.

Nauli za kutoka na kwenda mikoa miingine iongezwe kwa asilimia 50
Hapa lengo likiwa ni lilelile la ku-discourage movements zisizo za lazima humu ndani ya nchi kama njia mojawapo ya kudhibiti kusambaa kwa COVID-19.

Nasema haya kwasababu bado baadhi yetu hatuko serious sio katika kunawa tu,bali bado wako watu wanaosafiri kwenda kusalimia ndugu,jamaa na marafiki.

Hela zote zitazopatikana kutokana na ongezeko hili la nauli zielekezwa serikalini katika kupambana na huu ugonjwa.

Hata hivyo,bado nasisitiza safari za lazima ziruhusiwe ila cha msingi tuwe na udhibiti vinginevyo gonjwa hili linaweza kuja kutuelemea huko mbeleni.

Serikali itoe ruzuku kwa viwanda vinavyotengeneza sanitizer/hand wash humu nchini
Katika kuhamsisha matumizi ya vitakasa mikono na kuwapunguzia watu gharama za kununua hizi sanitizer,napendekeza serikali itoe ruzuku kwa viwanda vyote vinavyozalisha bidhaa hii ili kupunguza bei ya bidhaa hii ndani ya nchi yetu.

Serikali ipunguze kodi ya kuzalisha na kuagiza vitakasa mikono
Vile vile serikali inaweza kuvipunguzia kodi viwanda vinavyozalisha hii bidhaa pamoja na kupunguza kodi ya kuingiza vitakasa mikono humu nchini lengo likiwa ni kushusha bei ya bidhaa hii muhimu katika kupambana na COVID-19.

Miradi yote mikubwa na midogo isitishwe kwa muda
Mhe.Raisi,ni vizuri na ni bora ukaagiza kusitishwa kwa miradi yote mikubwa na midogo nchi nzima mpaka pale hali ya maambukizi itakopkuwa imekwisha kwani shughuli za hii miradi zinachangia sana movement na muingiliano wa watu kuanzia wafanyakazi wa hii miradi pamoja na wale wote wanaopata riziki kupitia miradi hii bila kusahau ndugu na jamaa zao wanaowaacha huku majumbani mwano pamoja na wale wanaokutananao huko mitaa wanakoishi baada ya kutoka makazini/vibaruani..

Mhe. Raisi,hizo hapo juu ni baadhi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa na serikali yako ila bado wataalamu wanaweza kuziboresha na hata kushauri njia nyingine bora zaidi ambazo mimi hapa sijazitaja.

Naelewa kabisa ugonjwa huu hapa nchini unaweza usilete madhara makubwa kulingana na hofu iliyopo lakini tutambue hii bado ni probability hivyo ni bora tuchukue tahadhari mapema kama ambavyo ni bora kuamini Mungu yupo, kuliko kutoamini yupo alafu ukaja kutananae huko Mbinguni.

Mwisho,tutambue kote wanakotangaza kufanikiwa kupunguza maambukizi,mfano China na sasa Italy, hawa wote walilazimika kuchukua maamuzi magumu zaidi ya haya nayopendekeza hivyo na sisi ni lazima tuwe tayari kuji-sacrifice kabla ya kutegemea ushindi dhidi ya hili gonjwa.

Tutambue pia sisi ni masikini sawa na yatima asietakiwa kudeka.
 
Administer

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
703
1,000
Mimi kama mwananchi wa kawaida,nashauri uchukue hatua zaidi katika kudhibiti kusambaa kwa huu ugonjwa ambapo sasa tunaambiwa kuna jumla ya wagonjwa 46.

Mhe.Raisi,kama sikosei,ilikuwa ni March 13 mwaka huu tulipotangaziwa mgonjwa wa kwanza wa Corona hapa nchini, hivyo ndani ya siku 30, tayari tumepata wagonjwa 46.Idadi/kasi hii si ndogo na tukumbuke sasa tumeingia katika kile kinachoitwa community transimission.

Hivyo,pamoja na hatua serikali yako ilizochukua mpaka sasa,napendekeza hatua zaidi ambazo ni hizi zifuatazo:

Zuia ibada zote kuanzia sasa
Mhe.Raisi,mikusanyiko na mikusanyiko tu na madhara yake katika kusambaza gonjwa hili yatabaki kuwa ni yale yale hivyo ni bora kuzuia Ibada kwa muda ili kulinda afya na uhai wa watu.

Tunaweza kuzuia Ibada kwa muda na baadae zikaendelea ila uhai wa mtu ukipotea,hakuna namna ya kuurudisha na tutambue madhara ya vifo vya wananchi ni pamaja na kutapoteza nguvu kazi ya Taifa inayotakiwa kutekeleza kauli mbiu yako ya 'hapa kazi tu".

Kingine,Ibada za Pasaka katika baadhi ya makanisa zimedhihirisha kuwa social distancing haiwezekani katika nyumba zetu za Ibada na hizi picha ni ushahidi tosha wa hali hii.

Hii ni hali katika kanisa la KKKT Ushariki wa Mjini Dodoma katika Ibada ya Pasaka siku ya jana.

View attachment 1418089

Zuia mikusanyiko katika mabaa na sehemu zingine
Mhe.Raisi,kwenye mabaa na sehemu nyinginezo mikusanyiko bado ipo japo inawezekana imepungua.Nachokushauri upige marufuku kwenye mabaa ila unaweza kuruhusu bar hizi kuuza pombe kwa mashariti ya mtu kwenda kunyewea nyumbani kwake na si baa.

Shaurina na Spika wa Bunge,Bunge lisitishwe
Mhe.Raisi,nakushauri ukutane na viongozi wa Bunge na mkubaliane kusitisha shughuli/vikao vya Bunge kwa muda ili kukabiliana nan huu ugonjwa.

Mhe.Raisi,uwepo tu wa wabunge na shughuli za Bunge mkoani Dodoma, maana yake ni kuwataka watu wasio wabunge ila wanaopaswa kuja Bungeni(mfaano maafisa wa serikali na madereva wao,n.k) nao wafike Dodoma kwa shughuli zinazohusiana na Bunge hivyo kuongeza muingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Swali lingine ni kuwa,wabunge wetu hawa siku za mwisho wa wiki husafiri kurudi Dar,majimboni mwao na kwingineko hivyo wanaweza kabisa kuchangia katika kusambaza maambukizi unless wabunge wote wazuiwe kusafiri mpaka Bunge liishe na kama kusafiri basi iwe kwasababu maalumu.

Wafanyakazi wa umma wasio na ulazima wabakie majumbani
Mheshimiwa,nashauri ikiwezekana kuanzia Jumatatu iyayo au hata kabla ya hapo watumishi wote wa umma wanaoweza kubaki majumbani wabaki na wanaoweza kufanya kazi zao kutokea majumbani mwao waruhusiwe kufanya hivyo.

Kwa mfano,walimu wa shule na wahadhiri wa vyuo wabakie majumbani badala ya kutakiwa kuendelea kuripoti makazini

Nauli za mabasi na ndege kwenda na kutoka Dar-es-Salaam ziongezwe kwa asilimia 100
Kwakuwa Dar-es-Salaam kwa sasa ndio kituvo cha ugonjwa huu,nashauri serikali iongeze nauli za kusafiri kwenda na kutoka Dar-es-Salaam kwa asilimia mia moja au hamsini ili ku-discourage movement zisizo za lazima.

Naelewa kuna watu wanaweza kulalamika ila watanzania tutambue wenzetu katika nchi nyingine wako katika lockdown hivyo hii yetu bado inaweza kuwa ni nafuu ukilinganisha na kinachoendelea katika mataifa mengine.

Vile vile fedha inayozidi baada ya nyongeza hiyo ya nauli ipelekwe serikalini katika mfuko wa kupambana na corona(naamini mfuko huo upo na kama haupo,basi ni wakati muafaka uanzishwe).

Hata hivyo,ningependa kutoa ushauri wa ziada kuwa kwa wale wenye safari za lazima kwenda au kurudi Dar waruhusiwe bila kutozwa gharama ziada ila iwe ni baada ya wahusika kutoa vithibitisho maalumu mfano kuonyesha barua ya rufaa kwenda Muhimbili kwa walio wagnjwa,n.k.

Nauli za kutoka na kwenda mikoa miingine iongezwe kwa asilimia 50
Hapa lengo likiwa ni lilelile la ku-discourage movements zisizo za lazima humu ndani ya nchi kama njia mojawapo ya kudhibiti kusambaa kwa COVID-19.

Nasema haya kwasababu bado baadhi yetu hatuko serious sio katika kunawa tu,bali bado wako watu wanaosafiri kwenda kusalimia ndugu,jamaa na marafiki.

Hela zote zitazopatikana kutokana na ongezeko hili la nauli zielekezwa serikalini katika kupambana na huu ugonjwa.

Hata hivyo,bado nasisitiza safari za lazima ziruhusiwe ila cha msingi tuwe na udhibiti vinginevyo gonjwa hili linaweza kuja kutuelemea huko mbeleni.

Serikali itoe ruzuku kwa viwanda vinavyotengeneza sanitizer/hand wash humu nchini
Katika kuhamsisha matumizi ya vitakasa mikono na kuwapunguzia watu gharama za kununua hizi sanitizer,napendekeza serikali itoe ruzuku kwa viwanda vyote vinavyozalisha bidhaa hii ili kupunguza bei ya bidhaa hii ndani ya nchi yetu.

Serikali ipunguze kodi ya kuzalisha na kuagiza vitakasa mikono
Vile vile serikali inaweza kuvipunguzia kodi viwanda vinavyozalisha hii bidhaa pamoja na kupunguza kodi ya kuingiza vitakasa mikono humu nchini.

Miradi yote mikubwa na midogo isitishwe kwa muda
Mhe.Raisi,ni vizuri na ni bora ukaagiza kusitishwa kwa miradi yote mikubwa na midogo nchi nzima mpaka pale hali ya maambukizi itakopkuwa imekwisha kwani shughuli za hii miradi zinachangia sana movement na muingiliano wa watu kuanzia wafanyakazi wa hii miradi pamoja na wale wote wanaopata riziki kupitia miradi hii bila kusahau ndugu na jamaa zao wanaowaacha huku majumbani mwano pamoja na wale wanaokutananao huko mitaa wanakoishi baada ya kutoka makazini/vibaruani..

Mhe. Raisi,hizo hapo juu ni baadhi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa na serikali yako ila bado wataalamu wanaweza kuziboresha na hata kushauri njia nyingine bora zaidi ambazo mimi hapa sijazitaja.

Naelewa kabisa ugonjwa huu hapa nchini unaweza usilete madhara makubwa kulingana na hofu iliyopo lakini tutambue hii bado ni probability hivyo ni bora tuchukue tahadhari mapema kama ambavyo ni bora kuamini Mungu yupo, kuliko kutoamini yupo, alafu ukaja kutananae huko Mbinguni.

Mwisho,tuambue kote wanakotangaza kufanikiwa kupunguza maambukizi,mfano China na sasa Italy, hawa wote walilazimika kuchukua maamuzi magumu zaidi ya haya nayopendekeza hivyo na sisi ni lazima tuwe tayari kuji-sacrifice kabla ya kutegemea ushindi dhidi ya hili gonjwa.

Tutambue pia sisi ni masikini sawa na yatima asietakiwa kudeka.
Uko sahihi
 
Daudjuma

Senior Member
May 31, 2011
100
225
Mtoa Mara uko sawa kabisa,ila hofu yangu ni utekelezaji,Binafsi nashindwa kuelewa kama viongozi wetu wanakiona kinachoendelea kwa wenzetu wa Dunia ya kwanza.Nakuunga mkono kwa maana ya kwamba vita hii ni kuwa kuliko ile ya kwanza na ya pili.Kibaya zaidi vita hii adui haonekani kwa macho.Duh,tumwombe Mungu wetu kwa nguvu zote.
 
ERoni

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
29,604
2,000
Kila ulichoandika ni sawa kabisa, we're heading the rough road. Najaribu kufikiria jinsi uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa utakavyokuwa baada ya hili janga.
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,375
2,000
13 Apr 2020

MTANGAZAJI TBC AFARIKI KWA CORONA, WAZIRI AZUNGUMZA - "WANAZIKWA KABURI MOJA"Mbunge wa Jimbo la Vwawa ambaye ni Waziri wa Kilimo, Mh. Japhet Hasunga amewakumbusha viongozi wa dini na waumini wote nchini kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona wakati wakiwa katika ibada na kwenye shughuli zao za kila siku.

Waziri Hasunga amewataka watanzania wote kwa pamoja kutambua kuwa ugonjwa huo ni janga la Dunia nzima lisilobagua matajiri wala masiki hivyo muhimu kila mmoja kuchukua tahadhari iwezekanavyo.

Wakristo kote Ulimwenguni jana Aprili 12, 2020 wameungana kusherehekea siku ya kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo maarufu kama Pasaka.

Source : Global TV online
 
Bignation

Member
Jun 3, 2015
66
125
Acha ujuaji pimbi wewe
Katika Mambo yote omba mungu akuepushe kutokuwa miongoni mwa wajinga. Taifa linapita katika kipindi kigumu wagonjwa wanaongezeka, shughuli nyingi zinasuasua, serikali Kwa upande wake inapambana na kufanya kila jitihada zilizokuwa ndani ya uwezo wake kudhibiti maambukizi, kutoa elimu Kwa wananchi na tahadhari mbali mbali dhidi ya coronavirus covid-19. sasa mtu anatoa mawazo au ushauri wewe unakebehi badala na wewe kujibu Kwa hoja au kutoa njia mbadala jinsi gani Kwa pamoja tutaudhibiti na kuutokomeza ugonjwa huu hatari.
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,983
2,000
Mkuu mleta mada nilikua naandika hoja kama hii sasa ngoja nikaifute ila niongeze nyama kidogo.
Nitaanza na DSM.
Jiji la DSM liwekwe lock down kwa wiki moja na yafuatayo yafanyike.
1.Wananchi wajurishwe kua wabaki majumbani mwao kwa wiki moja.
2.Usafiri wa kutoka DSM kwenda mikoani usitishwe ndani ya wiki moja pamoja na wakutoka mikoani kuja DSM
3. Serikali iwaondoe watu wote wasio na makazi na kuwapeleka kwenye mashule
4.Kila mtaa ifanyike kazi ya kupima kila mtu yaani nyumba kwa nyumba asa joto nk ili lifanyike kwa kushirikisha polisi,jeshi,viongozi wa mitaa na wizara ya afya.
5.Serikali igawe sanitizer na barakoa kwa kila familia au nyumba
6.Kuna familia ambazo zitakua na shida ya chakula nk..apa Serikali igawe unga kilo 20 ,maharage kilo tano na mchele kilo 10 kwa kila mwenye kuhitaji.
7.Serikali ipige marufuku huduma za mwendokasi,baa na ibada zote.
8.Kwa wale wagonjwa wanao hitaji huduma za hospitali kila siku basi vituo vya Afya vyote view na gari/ magari ya wagonjwa( Ambulance
9.Wafanyakazi wa Serikali na binafsi ni bora wakati huu wakafanyia kazi majumbani labda kama kuna ulazma.
10.Masoko yote yapewe siku mbili tu kujiandaa kufunga na baada ya apo yafungwe wiki nzima.
11.Magari ya kupeleka mizigo au kuleta mizigo nchini na jijini DSM yaruhusiwe baada ya kuwapima wahusika na kuyanyizia dawa.
12. Watakao kutwa na ugonjwa au dalili za corona wapelekwe kwenye kambi mfano kwenye mashule nk.
13.Hii itapendeza zaidi ikifanyika kwenye majiji yenye muingiliano mkubwa wa watu.
Sipingi hoja hii..ila nashauri kua aya yakifanyika yanaweza kutusaidia sana...Naomba tusiangalie ili kwa kuangalia mitazamo yangu kwenye Siasa zetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU TUSAIDIE KATIKA KUFANYA MAAMUZI.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom