Kusafisha na kung'arisha uso vizuri, tumia face wash au facial cleanser

Magnificient

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
1,162
705
UTUMIAJI WA FACE WASH AU FACIAL CLEANSERS HUPENDEZESHA ZAIDI USO WAKO
U hali gani rafiki yetu na mpenzi wa mambo ya vipodozi na muonekano wa mwili? Karibu katika somo la leo linalohusiana na vipodozi viitwavyo Face Wash au Facial Cleanser vitumikavyo kwa ajili ya kuoshea uso.

FACE WASH/FACIAL CLEANSER NI NINI?
Face wash au Facial cleanser ni vipodozi vinavyofanya kazi ya kusafisha uso kwa kiasi kikubwa kabisa kwa kuyayusha na kuondoa kiasi kikubwa cha uchafu wa usoni kama vile mafuta, jasho, vumbi, seli zilizokufa na takataka zingine.
Matokeo yake ni kwamba mtu ambaye ametumia kipodozi hiki anabaki na ngozi safi kabisa na inayong’aa kwa sababu kiasi kikubwa sana cha uchafu na vitu vingine vilivyokuwa vinafunika ngozi yake vimeondolewa. Ufanisi wake katika kusafisha uso ni mkubwa kuliko sabuni.

KWA NINI NI BORA UKATUMIA FACE WASH AU FACIAL CLEANSER?
Kwanza Face wash au Facial cleanser zinasaidia kuondoa sehemu kubwa sana ya uchafu na vitu vingine vinavyoziba ngozi yako. Hii ni bora zaidi kwa sababu itakuacha na ngozi laini, inayong’aa na kuvutia vizuri.
Pili Face wash sio kali sana kama sabuni, na ni nzuri zaidi kuoshea uso wako. Sabuni huweza kuwa kali na pia kama ni ya mche au kipande huweza kuwa inaharibu ngozi yako na kupasua chunusi, kuleta michubuko nk kama utajisugulia kwa nguvu.
Hayo hufanya Face wash au Facial Cleansers kuwa bora zaidi katika kusaidia kuondoa chunusi na pimples, kung’arisha uso, kumaliza uchafu usoni, kuzuia magonjwa ya ngozi usoni, kupunguza kasi ya uso kuzeeka na kuzipa seli za uso kuweza kupumua, kukua na kuendelea vizuri.

MAMBO YA KUZINGATIA
Chagua Face Wash/Facial Cleanser nzuri na yenye ubora unaofaa kwa ngozi yako. Kama ngozi yako ni kavu chagua Face wash kwa ajili ya ngozi kavu, na kama uso wako ni wa mafuta basi chagua face wash/facial cleanser kwa ajili ya uso wa mafuta. Kadhalika na kwa ngozi ya kawaida na ngozi mchanganyiko.
Tafuta ya gharama unayoimudu vizuri ili uweze kuitumia vizuri na kwa uhuru zaidi.
Kuna Face wash/Facial Cleanser zinazoweza kuwa feki na kali kwa ngozi yako. Pata ushauri kutoka kwa watu wanaojua vizuri masuala ya vipodozi na uzuri wa mwili.

S&E BEAUTY SOLUTIONS
inakutakia kila la kheri katika kujipendezesha na uzuri wako.
Kama una tatizo lolote , swali au unahitaji bidhaa yoyote au ushauri wa afya, urembo na vipodozi karibu sana kwetu.


S&E BEAUTY SOLUTIONS
TEMEKE BUZA NA ILALA BUNGONI
DAR ES SALAAM
Simu : 0 659 528 724 , 0 784 082 847
E-mail :
tecetra@gmail.com
Au tembelea ukurasa wetu wa facebook uitwao S&E BEAUTY SOLUTIONS
Au blog yetu
www.afyazaidi.blogspot.com
 
Kuna thread inasema Wanaume wa Dar wanatumia mkorogo, kutinda nyusi, manicure na pedicure..... Naomba thread hii I justify kama mambo hayo ni kwa ajili ya watu wa jinsi gani na mkoa gani
 
Back
Top Bottom