Kusafisha maji ya kisima kuwa safi na salama kwa matumizi ya binadamu

Djuba

Member
Mar 7, 2016
19
9
Ndugu wana Jamvi,
Heri ya Mwaka mpya 2017.
Nimechimba kisima chenye urefu wa mita 80 na kufanikiwa kupata maji mengi tu. Tatizo nililo nalo ni kwamba maji haya yana chumvi nyingi sana kiasi kwamba huwezi kutumia kwa kuyanywa bali hufulia nguo na kuosha vyombo ama kusafishia nyumba.

Nachohitaji ni utaalamu wa kuyasafisha maji haya yawe safi na salama kwa kunywa, kupikia na hata shughuli nyingine yeyote kwa binadamu. Ninahitaji kuwa na uwezo wa kusafisha lita 25,000 kwa siku....kwa yeyote mwenye ufahamu wa vifaa vya kusafisha maji, tafadhari nielekewe ntavipata vipi.
 
Hiyo technology ni gharama sana kuyatoa maji ya chumvi kuwa matamu bora uchimbe kisima chengine kwa knowledge yangu
 
Gharama kwa 25k litres ni expensive sana,jaribu machine ya litre 1000 unaweza kupata Merry water.
 
Mkuu hayo maji yamepimwa? Kama yamepimwa weka report inayoonesha contents za maji ili iwe rahisi kukushauri mashine gani inakufaa zaidi kulingana na mineral contents za kwenye maji
 
Back
Top Bottom