Kusafisha fedha haramu ndiyo nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kusafisha fedha haramu ndiyo nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Radhia Sweety, Mar 25, 2012.

 1. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,453
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Naamini kuna watu wenye uelewa wa hii makitu wazee. Hivi mtu anaposema sijui kutakatisha fedha haramu huwa anakuwa na maana gani. Mara nasikia ooh fulani amehukumiwa kwa kosa la kusafisha fedha zilizotokana na madawa ya kulevya. Hizi fedha zinasafishwa na nini? Na huo uchafu unaosafishwa ni upi? Naomba majibu na siyo masaibu.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,460
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Mbona ni rahisi? Tuseme wewe mathalan unauza unga, au madawa mengineyo ya kulevya ambayo ni haramu. Pesa unayopata kwenye hiyo biashara ni pesa chafu. Na kwa nchi kama vile Marekani, huwezi kuiweka benki kwa sababu watataka kujua umeipataje na kama umelipa kodi. Nasikia kwa wenzetu Waitalia ilikuwa rahisi kwenda Mombasa na Zanzibar kujenga hoteli za utalii. Pesa waliyotumia ilikuwa pesa haramu lakini biashara ya hoteli ni biashara halali inayotambulika. Sasa kwa mtu kama huyu hapo Bongo, labda atajenga nyumba, hoteli, au hata flats za kupangisha. Kwa kufanya hivyo, anasafisha pesa haramu. Umenielewa bibie?
   
 3. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,453
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Kwahiyo fedha itokanayo na dawa za kulevya pekee ndiyo haramu? Vipi kuhusu fedha itokanayo na rushwa? Na ina madhara gani kwenye uchumi? Kwani kuna tatizo gani kama nauza unga kisha natumia faida kujengea hospitali, shule za kisasa, hoteli etc na kutoa ajira?
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hii kitu wenyewe wanaiita Money Laundering.
  Unachukua fedha haramu ambayo ni Mamilioni ya $$$$ na kuirudisha katika mfumo wa Mabenki kwa kukata 10%- 20% ya fedha haramu kwa maajenti wa abenki Makubwa ya kimataifa.

  Network ya Money Laundering wenyewe wanaiita Cartail


  Kama ulivyosema ni figurative language kuonyesha kwamba unatakasisha fedha Haramu.

  Ukiuza madawa ya kulevya na kupata $10,000 ni rahisi sana kuingia nazo mtaani na kutumia bila matatizo yeyote. ukiwa na $100,000 vile vile unaweza usipate taabu sana kutumia bila kufanya watu wajue na kukutuhumu.
  Sasa fikiria ukipata $1000,000,000.00 unaweza kuingia nazo mtaani ukaanza kutumia bila kufanya jamii au serikali kushituka?
  Wale wauzao madawa ya kulevya na kutengeneza fedha za nguvu kaa $10Million ni lazima watafute njia ya kuziingiza katika system kama Mabenki ya ndani na ya nje bila kuishitua serikali au jamii.

  Hapo ndipo kazi ya kusafisha Fedha huanza.
  Money Laundering ni shughuli yenye kuingiza faida zaidi ya USD Billion 100 kila mwaka.

  Wezi wa EPA wote walifanya Money Laundering.
  Malipo ya pembeni ya mikataba Fake yote Tanzania yamelipwa through System kama hiyo.

  Ukiwa na Fedha kibao hapo naongelea $2000,000.00 huwezi kwenda nazo cash benki na kusema nataka kufungua Account.
  Benki zote za kawaida duniani watakuuliza umetoa wapi.

  Siku z anyuma Benki za Somalia, Rwanda Burundi na Zaire hazikuwahi ona taabu kufungua account ukija na mabilioni ya dola kufungua account kwa sababu serikali za nchi hizo hazikuwa na sheria ya Money Laundering. Hata sasa hivi ni rahisi kwa benki nyingi za nchi masikini kufungua account cash za fedha nyingi ili mradi uwe tayari kukata mpunga wa nguvu.

  Katika nchi masikini kama Tanzania kuna Financial companies nyingi sana ambazo ni maajenti wa biashara ya Money Laundering kwa niaba ya mabeni mazito ya Uswis Marekani na Wingereza.

  Ni biashara haramu ambayo viongozi wa serikali nyingi duniani huitumia kusafirisha fedha wanazo ibia serikai zao na kuziweka katika Mabenki ya Uswis na sasa Dubai.   
 5. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,635
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 160
  hata hiyo ya ujenzi wa hospital, shule, hotel na kupeleka kwenye betting ni moja ya njia ya kusafisha hiizo hela kwa unakuwa umeficha chanzo cha hizo hela zako ndio maana inakubidi ufanye hivyo kingine hata kama walivyo fanya CDM kwenye ile M4C pale arusha kama mtu anajua kabisa ana hela za magumashi lazima azipeleke huko..
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,460
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Hata fedha ya rushwa ni haramu. Katika nchi zinazofuata utawala wa kisheria kama umechukua hongo lazima ulipie kodi lakini wengi hawalipi kodi kwa sababu hawataki ijulikane kama wamepokea hongo. Na ikithibitika kuwa umepokea hongo, kama Marekani, IRS (Internal Revenue Service) wanakufungulia mashtaka ya tax evasion. Ubaya wa kutumia madawa ya kulevya kujengea hospitali ni kwamba biashara yenyewe ni haramu. Ni kama vile uwe madame wa danguro na fedha hizo utumie kujenga hoteli. Siku utakapogundulika unapelekwa mahakamani.
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Look a the transaction of selling drugs as a two way traffic.

  Unauza dawa unapata fedha, mnunuzi anapata madawa anayatumia.
  Madawa ya kulevya ni very addictive, watu wakiwa addicted wanageuka kuwa mzigo wa jamii.
  Mwanzo unauza madawa kufanya watu wengine kuwa Mateja baada ya miaka 10 majirani marafiki na hat ndugu zako nao wanakuwa mateja mwishowe watoto au wajukuu zako wanakuwa mateja hapo ndipo utamu wa fedha za madawa hufikia kilele.

  Kama wewe ni muuzaji pekee kwa miaka yote inaweza kuwa tatizo dogo.Lakini pale kundi kubwa la watu wakianza kuuza na kuitaka faida uipatayo ugomvi wa Market unazuka. Rule ya kuuza madawa duniani kote ni PROFIT BY ALL MEANS.
  killing for profit huanza.
  Serikali ya nchi ya Colombia ilisambaratika kwisha na Mamilioni ya wananchi wake kuuawa sababu kubwa ikiwa ni Biashara ya madawa ya kulevya.
  Leo hii Mexico wanauana kama Kuku ili Ku control Masoko na route za kupelekamadawa nchni Marekani.
  Biashara ya kuingiza madawa nchini Marekani ni ya $6,000,000,000,000.00 hiyo ni Billioni Sita sawa na
  Tshs 9600,000,000,000,000 yaani 9.6 Trillioni.
  Huko Columbia Watu wanang'a kahawa migomba na kupanda Mikoka mashamba ya mahindi nyanya na viazi mviringo nayo hubadirishwa na kuwa ya Mikoka. Uwezekano wa njaa ya kitaifa kuingia ni mkubwa.

  Hebu Fikiria sisi kule kwetu Njombe na Mufindi tukiacha kulima Mahindi na kupand zao la GANJA itakuwaje??

  The same way Mtu akituibia fedha za serikali say za Kukarabati Daraja la Malagalasi na kujengea hoteli ya nguvu Arusha. Siku Daraja likivunjika kwa Maintanance Mbovu hasara yake ni Uchumi kwa kanda nzima. hoteli ile iliyoko Arusha haiwezi saidi kuvusha watu kuja Dar mara daraja likibomoka.

  KWa hiyo ukiuza madawa bila kuweka dhana ya madhara ya madawa kichwani mwako ni kweli hakuna matata.
  Fedha siyo ukombozi wa matatizo fedha ni means tunayo tumia kuexchange value.
  Value ya madawa ya kulevya kwa muuzaji ni Fedha aipatayo.'Value ya Madawa ya kulevya kwa mnunuzi ni kubwia na kuwa teja.
  Uko Tayari watoto wako kuishi na kuchanganyikana na mateja??
  Uko Tayari kuwa na jirani Teja??
  Mateja wakichacha wanageuka wezi sugu wenye kutuia silaha kali waibapo.

   
 8. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,453
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Nashukuru sana kwa maelezo hapo juu. Kumbe tunaweza kuliondoa tatizo kwa kuanza kutoza kodi kila hela inayoingia kwenye mfumo wa benki. Vinginevyo naweza kusema kuwa hela nyingi iliyopo kwenye mzunguko hapa nchini ni haramu, kuanzia hela ya vibaka hadi walaji rushwa kubwa kubwa.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24,909
  Likes Received: 1,934
  Trophy Points: 280
  Unachukua fedha unaziloweka kwenye beseni + jik then unazisuza na maji safi kisha unazianika=Unakua ushazitakatisha fedha chafu :D
   
 10. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 16,778
  Likes Received: 2,971
  Trophy Points: 280
  Katika wote, wewe ndio nimekuelewa!!!
   
 11. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,248
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  hata mm nimempata sawia. Wengine wametumia kiswahili kigumu sana na kuzunguka zunguka.
   
 12. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 453
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu Madela wa Madilu:Umegusia hapo juu kuwa hapa Tanzania kuna financial companies zinatomika katika money laubdering. Unamaanisha banks bureau de change au nini maana hizi nazo no companies. Na kama unazifahamu huoni kuwa na wana Jf wengine wanastahili kuzifahamu? Tuelimishe vizuri maana inaelekea wewe ni resource person kwenye hili swala la money laundering
   
 13. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 988
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Maelezo yenu bomba ila nimsikia pia kuwa zoezi linaloendelea la kuhakiki account benki ni kuzuia kutakatisha fedha chafu. swali ni je mwalimu anayepokea kamshahara kake kasikofikia hata 300,000 anatakatisha nini? Mbona tunanyanyaswa tu na watakatishaji wanajulikana?
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 29,478
  Likes Received: 9,892
  Trophy Points: 280
  Money laundering refers to the process of concealing the source of illegally obtained money. The methods by which money may be laundered are varied and can range in sophistication. Many regulatory and governmental authorities quote estimates each year for the amount of money laundered, either worldwide or within their national economy. In 1996 the International Monetary Fund estimated that two to five percent of the worldwide global economy involved laundered money. However, the FATF, an intergovernmental body set up to combat money laundering, admitted that "overall it is absolutely impossible to produce a reliable estimate of the amount of money laundered and therefore the FATF does not publish any figures in this regard."[SUP][1][/SUP] Academic commentators have likewise been unable to estimate the volume of money with any degree of assurance.[SUP][2][/SUP]
  Regardless of the difficulty in measurement, the amount of money laundered each year is in the billions (US dollars) and poses a significant policy concern for governments.[SUP][2][/SUP] As a result, governments and international bodies have undertaken efforts to deter, prevent and apprehend money launderers. Financial institutions have likewise undertaken efforts to prevent and detect transactions involving dirty money, both as a result of government requirements and to avoid the reputational risk involved.
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Fedha yoyote inayopatikana kwa njia za haramu ni fedha haramu, hata fedha yoyote isiyolipiwa kodi ni fedha haramu. Kuiingiza kutoka kwenye uharamu ulikoipata na kuiweka kwenye uhalali wa kazi za halali ndio kuisafisha hiyo fedha.

  Hata fedha unayoipta kwa njia ya kuuza mwili, kama sheria ya unapoishi haikuruhusu kufanya hivyo, basi hiyo ni fedha haramu.
   
 16. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,453
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  Kuuza mwili inakuwaje fedha haramu wakati mtu anauza mwili wake mwenyewe? Basi kama vipi hata fedha inayopatikana kwa kucheza mpira nayo ni haramu.
   
 17. s

  silanga Member

  #17
  Mar 25, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuuza mwili ni kosa la jinai kwa hiyo mapato yake si halali, tatizo kubwa ni kuweza kuthibitisha mtu huyu anajiuza ndio mana hata kesi zao hua wanaambiwa ni za uzururaji. Kwa nchi nyingine kuuza mwili imehararishwa kisheria! Hela itokanayo na mpira ni halali kabisa na huwezi linganisha na kujiuza
   
 18. B

  BASIASI JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 2,471
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  ajajibu swali unasafishaje pesa haramu??frm uchafu
   
 19. B

  BASIASI JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 2,471
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  hapo ndipo unaponimaliziga mkuu wangu ngoja niende msalani narudi
   
 20. U

  Uwilingiyimana Member

  #20
  Mar 25, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FOOLISH. Why the hell dont u simply shut up? Watu wamejitahidi kumwelewesha muuliza swali vizuri kabisa, kitaalamu, wewe unaleta hoja-taka zako hapa. Ama kweli JF nayo imevamiwa, waungwana bora tuanze kufikiria kuhamia mtaa wa pili!
   
Loading...