Kuruhusiwa Maandamano kupinga ziara ya Joji Kichaka: Je, ni kupanuka kwa demokrasia?

Mbalamwezi

JF-Expert Member
Sep 30, 2007
800
171
Wakuu JF,

Hivi kuruhusu maandamano ya kupinga ujio wa Joji Kichaka bongo, na polisi kuwasindikiza waandamanaji hao, ni tukio lisilo la kawaida. Je, ni kweli inaashiria kupanuka kwa demokrasia?
 
This is tautology tayari ipo threas ya jambo hili.... peruzi kidogo mkuu
 
Mimi nimeshawahi kushuhudia KKK wakiandama huku wakisindikizwa na ma-sherriff deputies...
 
This is tautology tayari ipo threas ya jambo hili.... peruzi kidogo mkuu

Mbona siioni mkuu Masatu, hiyo thread inayofanya comparison ya kuruhusu maandamano na ukuaji wa demokrasia, tafadhali niwekee hapa.
 
Mbalamwezi bwana .Ipo mkuu wangu soma ukiwa umetulia utaiona .Kama wameanza kuwasindikiza basi salama next time wapinzani pia wasindikizwe badala ya kupeleka FFU
 
Ok Mkuu Lunyungu, sasa natafuta namna ya kuiondoa, nafanyaje? Nielekeze tafadhali.
 
Mods, nimenyanyaswa sana, nimefedheheshwa sana, sikusikilizwa, naomba hii thread yangu ijiuzuru, maana ipo inayoshabihiana nayo. tatizo ni hii thread yangu...
 
Kwa hakika huku ndio kukua kwa demokrasia, wanaita freedom of expression, kumruhusu mwingine aseme anachoamini kuwa ni sawa hata kama hukubaliani nacho, ilimradi kwa kufanya hivyo hajavunja sheria au katiba ya nchi. Ni mojawapo ya haki za binadamu: uhuru wa maoni.
 
Naam Kithuku, ndio demokrasia hiyo. Sasa naomba unisaidie na hili ndugu yangu:

Ni haki ya mtu yeyote Tanzania kuandamana kupinga ujio wa Kichaka.
Na, ni haki kwa mTanzania yeyote akiamua kuandamana kumuunga mkono Bw. Osama, kama hana kosa lolote alilokwishaitendea Tanzania.

Yote hiyo ni demokrasia, au sio?
 
Wakuu JF,

Hivi kuruhusu maandamano ya kupinga ujio wa Joji Kichaka bongo, na polisi kuwasindikiza waandamanaji hao, ni tukio lisilo la kawaida. Je, ni kweli inaashiria kupanuka kwa demokrasia?

Hebu jaribu kufanya maandamano yako ukipinga jinsi viongozi wa serikali wanavyofuja mali za umma uone kama kweli demokrasi imepanuka hivyo.
 
Naam Kithuku, ndio demokrasia hiyo. Sasa naomba unisaidie na hili ndugu yangu:

Ni haki ya mtu yeyote Tanzania kuandamana kupinga ujio wa Kichaka.
Na, ni haki kwa mTanzania yeyote akiamua kuandamana kumuunga mkono Bw. Osama, kama hana kosa lolote alilokwishaitendea Tanzania.

Yote hiyo ni demokrasia, au sio?

Naona umenukuu maneno yangu bila kuyatilia maanani. Hebu soma tena niliyoandika halafu ukikuta pale nilipoandika "....ili mradi kwa kufanya hivyo hajavunja sheria au katiba ya nchi" urudie mara kumi sehemu hiyo labda itakusaidia!
 
Ninalichukulia jibu lako hilo kuwa ni 'Ndio' mradi mwananchi huyo havunji sheria.

Nadhani nimejitahidi, kwa maana nimesoma x10 kama ulivyosema mwalimu.
 
Chiefs,

I'm not sure these demonstration portrays our true democracy, prove that we have matured in that field or even we are honestly democratic. It just occurred to me that whenever wapinzani want to have a public rally they have to apply for a permit and sometimes they are denied of their rights (right to assemble in peace, freedom of speech, etc). Isn't this hypocricy of our government to have selective portrayal of democracy?

My fellow JF members, let's try to imagine if next week Tanzanians march to regional headquaters to demand resignation of all MPs who are classified as mafisadi together with the Speaker; demand people involved in BoT scandal be brought to Justice, Kiwira returned to the State, etc...who will dare to do so? Would they even get a permit to do so? I don't think so, honestly.

Therefore, these demonstrations had some blessings because they were religious-driven but it does not have anything to do with democracy...this is just my opinion!
 
Back
Top Bottom