Kurugenzi ya Sheria ofisi ya Rais msaidie Jaffar kuweka "citations" za sheria aliyotumia pale anapotekeleza majukumu yake, kuondoa utata wa press zake

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Press release za serikali ya Tanzania zimekuwa na story tu, zinakosa Jambo kuu ambalo ni msingi wa sheria pale hoja inapohusuJambo la kisheria. Rais anapofanya uteuzi Kuna sheria iliyompa hiyo mamlaka, lakini press zote hazina sheria inayoonyeshwa. Rais anapofuta umiliki wa ardhi au anapotengua mtu au anapokabidhi Mali au nyaraka lazima anafanya kwa mujibu wa sheria.

Press za Ikulu zikizingatia sheria lazima wizara na idara nazo zitalazimika kufanya hivyo. Hi itawasaidia Sana wataalam wetu wa sheria kuumiza kichwa lakini itawajengea uwezo wakusoma kila Rais anapozungumza au anapotoa maelekezo, in longrun wananchi watazielewa sheria zinazosimamia mambo mbalimbali lakini pia zitawajenga watu kufanya mijadala kwa misingi ya sheria.

Natambua si lazima Kurugenzi ya mawasiliano na Msemaji wa serikali achukue ushauri huu ila naamini Kama tunataka kuzifahamu sheria zetu lazima tuzisome na kuzitumia lakini pia lazima kwakuzitumia watu wengine watazisoma na watajadili mapungufu na uzuri na hivyo itasaidia maboresho. Tumewasomesha watu wapeni kazi wafanye, waelekezeni wanasheria washiriki kuandaa press zenu ni muhimu Sana.

Hakuna maagizo au maamuzi ya serikali yanayotoka nje ya sheria. Tujisahihishe.
 
Huwa naiona sheria ya press kutua au kuondoka uwanja wa ndege.Hiyo wamekariri sana.

Yapo mengi hawajipangi

Mfano Rais anafika kwenye hafla then anakaa tena utasikia Mhe usimame ili uimbwe wimbo wa Taifa.Heshima ya Rais na wimbo wa Taifa inashuka.
 
Back
Top Bottom