Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,797
- 11,959
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu yazungumzia matokeo ya ziara ya Rais nchini Oman na matokeo ya filamu ya Royal Tour.
Uwekezaji watajwa kuongezeka ikiwemo wawekezaji wanaotaka kuwekeza Serengeti, Kilimanjaro na Dar es Salaam na muwekezaji huyo ameshawasiliana na kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC)
Na serikali inaongeza nguvu ya kujua wawekezaji wakija wanawahudumiaje. Wakati huo TANAPA wameshabainisha maeneo yanayohitaji uwekezaji.
Mauzo ya nje yamefikia Dola milioni 10 ikiwa ni matokeo ya Economic Diplomacy. Thamani ya uwekezaji imeongezeka. kutokana na Royal Tour.
Serikali imeendelea kuhakikisha inaboresha uwekezaji na kujiandaa kuwapokea wawekezaji wakubwa katika kuongeza utalii, kukuza biasahara na kuwekeza katika viwanda.
MASWALI
Wakijibu swali la Mariam Mziwanda wa kutoka Uhuru Media, kuhusu hali ya mauzo ya nje yalikuwaje hadi kusema kuwa mauzo yameongezeka. Kurugenzi imesema mauzo ya nje yalikuwa kwa wastani wa bilioni 7 hadi 8 na sasa imefika dola bilioni 10 hali ambayo serikali inajivunia, japo wamesema inawezekana sio royal tour pekee bali kuna vitu vingine vinaweza kuwa vimechangia.