Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inauza Habari za ofisi ya Rais Kikwete

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Waingereza wanasema, the one who speaks the truth is loved by God!

Rais wa nchi au Taifa lililojengwa katika misingi ya kidemokrasia ndani ya presidential system huwa anaajiriwa na wananchi kwa ajili ya kuwatumikia wananchi ndani ya mkataba uliokubaliwa kikatiba katika nchi au taifa.

Ndani ya presidential system, ofisi ya Rais huwa niya juu kabisa katika nchi au Taifa lolote hapa duniani.

Habari za Rais kuhusu kile anachokifanya kila dakika kwa faida ya nchi au taifa ni lazima zipatikane bure na ziwafikie wananchi wake katika wakati unaolingana na hali halisi ya mawasiliano katika nchi au taifa.

Tanzania kwa sasa tumepiga hatua mbele katika Nyanja mbali mbali za mawasiliano kama internet, instant messaging, Internet forums, and social networking kama inavyobainishwa kwenye The Global Information Technology Report 2014 iliyotolewa kwenye World Economic Forum 2014. Tanzania kwa sasa tuko kwenye nafasi ya 125 kati ya nchi 148 ambazo zimefanyiwa research.

Kwa nchi za Afrika, Tanzania tuko kwenye nafasi ya 19 kama inavyobainishwa - HAPA

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa kutambua umuhimu wa wananchi wake kupata habari ili kuwasaidia kukielewa kile anachokifanya kila dakika katika msingi wa uwazi na ukweli, ndiyo maana amelazimika kuunda kitengo cha mawasiliano na pia tovuti ya rasmi ya Ikulu achilia mbali tovuti ya Serikali na taasisi zake ili zifanye kazi ya kuwahabarisha wananchi wake chini ya Wakala ya Serikali Mtandao.

Wafanyakazi wa Kitengo cha mawasiliano cha Rais wanalipwa kwa kutumia kodi ya wananchi na kwa maana hii, kuuza habari au kukasimisha habari za Rais kwa watu au kikundi katika mlengo wa kuziuza ni makosa katika utaratibu, kimaadili na kisheria.

Kumekuwepo na mchezo mchafu unaoendelea kwa muda mrefu katika kitengo cha Kurugenzi ya Mawasilino Ikulu. Huu mchezo mchafu unapaswa kulaaniwa na wananchi wazalendo kwa nguvu zote.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais wa Jamhuri wa Muungano imekuwa ikitumia habari za Rais kwa ajili ya kuwapatia maslahi zaidi baadhi ya watu/watumishi wa kitengo cha Mawasiliano ya Rais kwa kutumia mlango wa nyuma kinyume na taratibu au maadili ya kazi zao.

Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais Kikwete imekuwa ikitoa habari na kuzikasimisha(commission) kimaslahi kwenye blog ya mwananchi mmoja anayeitwa Muhidin Issa Michuzi mwenye blog inayoitwa Issamichuzi Blogspot badala ya kuzitoa moja kwa moja kwa wananchi kupitia tovuti ya Ikulu, Blog ya Ikulu au Idara ya Habari (MAELEZO) katika muda mwafaka.

Katika kunufaika zaidi na habari za ofisi ya Rais, Blog ya Muhidin Issa Michuzi imeweka kizuio, kwa kiingereza wanasema, block visitors from right clicking or disable "copy and paste" to protect blog source code ili kuhakikisha habari za Rais Kikwete haziwezi kuchukuliwa na media au blog nyingine baada ya kuziweka kwenye blog yake.

Kuiacha kwa maksudi/malengo Tovuti Rasmi ya Ikulu iwe outdated kwa mlengo wa kukasimisha habari wakati kuna watu wanalipwa kwa kazi hiyo ni ufisadi na wizi wa pesa za walipa kodi wa nchi.

Kutoa habari na Presidential Press release na kumpa kwanza Muhidin Issa Michuzi ili aziweke kwenye blog yake ili wananchi watembelee kwanza blog yake kwa manufaa ya kumpatia Issamichuzi Blogspot kipato kupitia wadhamini wa matangazo ndani ya blog yake ni uvunjifu wa taratibu na maadili ya utumishi achilia mbali sheria mama ya nchi kama ilivyoainishwa katika Sura ya Kwanza, kifungu cha 18(2) kinachohusu Haki ya Uhuru wa Mawazo kama kinavyosema, 18 (2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

Kwa sasa ukitembelea Tovuti Rasmi ya Ikulu, kwenye section inayoitwa kituo cha Habari. Habari inayoonekana ni mpya ni habari ya Jumanne, Oktoba 14, 2014, inayohusu Rais kutoa Hati za Uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 162 ambao walikuwa wakimbizi kutoka Burundi. Hii ni habari ambayo kwa sasa ni zaidi ya mwezi mmoja tokea tukio litokee lakini ukienda kwenye Blog ya Muhidin Issa Michuzi unakutana na latest news kuhusu Rais Kikwete.

Ukitembelea kwenye sehemu ya Matukio katika Tovuti ya Ikulu unakutana na matukio ya Tuesday 4th March 2014 ambayo yanahusu Rais Kikwete alipotembelea vikosi vya JWTZ vya Komando Morogoro. Kwa sasa ni zaidi ya miezi minane tokea matukio, lakini kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Ikulu, hii ndiyo LATEST NEWS, lakini ukitembelea Blog ya Muhidin Issa Michuzi utakutana na matukio mapya kuhusu Rais Kikwete anavyoendelea kiafya kwenye matibabu, Marekani.

Hata hotuba za Rais Kikwete kwenye Tovuti Rasmi ya Ikulu ni outdated lakini kwenye Issamichuzi blogspot utapata the latest speech.

Ziara ya Rais Kikwete nchini China iliyoanza tarehe 21 Oct 2014 ilikuwa inapewa coverage kila siku katika Blog ya Muhidin Issa Michuzi lakini katika blog Rasmi ya Ikulu, habari zilikuwa zinawekwa baada ya siku tatu au nne.

Video ya ziara ya Rais Kikwete nchini China imewekwa kwenye Blog Rasmi ya Ikulu tarehe 6 November 2014 wakati Ziara ilimalizika tarehe 26 Oct 2014.

Ninaungana na Gazeti la RaiaMwema katika kukemea utendaji wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu katika makala yake ya tarehe 13 May 2013 inayosema, Tumtenganishe Salva na Ikulu yetu Salva na Ikulu yetu kama ilivyoandikwa na Msomaji Raia.

Makala ya RaiaMwema inapatikana - HAPA

Kama kulipa kodi ni lazima ili serikali itoe huduma za jamii, vile vile ni lazima kwa serikali kutoa huduma za jamii kama inavyodai kodi.

Ukweli lazima usemwe na katika ukweli, ndiyo tunapata nafasi ya kujitathmini kiutendaji.

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, tutendeeni haki ya msingi kama ilivyoainishwa kwenye Katiba yetu.
 
"Katika kunufaika zaidi na habari za ofisi ya Rais, Blog ya Muhidin Issa Michuzi imeweka kizuio, kwa kiingereza wanasema, block visitors from right clicking or disable "copy and paste" to protect blog source code ili kuhakikisha habari za Rais Kikwete haziwezi kuchukuliwa na media au blog nyingine baada ya kuziweka kwenye blog yake."

Kuiacha kwa maksudi/malengo Tovuti Rasmi ya Ikulu iwe outdated kwa mlengo wa kukasimisha habari wakati kuna watu wanalipwa kwa kazi hiyo ni ufisadi na wizi wa pesa za walipa kodi wa nchi.


Hii nayo ni "ESCROW" nying
ine kwa mtindo mwingine
.

 
Nijuavyo mimi Michuzi ni mpiga picha wa rais, hivyo ana access ya moja kwa moja na shughuli za kikazi za rais (Mf. ziara ya rais Marekani). Kuzuia upakuaji picha na taarifa ktk blog yake kwangu mimi, ni ulinzi ili zisije tumiwa vibaya na ikachukuliwa source ni yeye. "Tuelomishane"
 
Nijuavyo mimi Michuzi ni mpiga picha wa rais, hivyo ana access ya moja kwa moja na shughuli za kikazi za rais (Mf. ziara ya rais Marekani). Kuzuia upakuaji picha na taarifa ktk blog yake kwangu mimi, ni ulinzi ili zisije tumiwa vibaya na ikachukuliwa source ni yeye. "Tuelomishane"
Huyu Misupu awekwe kwenye source za info if at all amepiga picha kwa niaba ya ikulu. Hata hivyo je unamtambua Fred Maro?
 
Tatizo la maandiko yako unayatupa BBC yakiwa na contents ambazo ingawa zinakusaidia kulipwa mshahara yanaianika nchi hata kama watendaji wetu wanakasoro
 
Mkuu mbona Safari zote Za JK Issa michuzi yupo, hata hi wanao rudi kesho yumo Kwenye msafara, wanampa Kwa Raha zao wala hanunui, watauziwa hao wengine, zamani Issa michuzi alikua akimnanga JK Mpaka basi, sasaivi yuko nae uso na macho anakula matunda ya uhuru hasemii...
 
Huyu Misupu awekwe kwenye source za info if at all amepiga picha kwa niaba ya ikulu. Hata hivyo je unamtambua Fred Maro?

Mkubwa nadhani Fred Maro si ndiye hasa mpigapicha mkuu wa raisi anayetambulika kiutumishi? Maana navyoelewa Michuzi alilazimishwa tu kuwa mpiga picha wake kwa sababu ya uSaigoni wake tu. The sad thing vijana wa Michuzi media wanatumia baadhi ya vifaa vya upigaji picha ambavyo ni mali ya umma kwenye ishu zao binafsi hasa za matukio.
 
Nijuavyo mimi Michuzi ni mpiga picha wa rais, hivyo ana access ya moja kwa moja na shughuli za kikazi za rais (Mf. ziara ya rais Marekani). Kuzuia upakuaji picha na taarifa ktk blog yake kwangu mimi, ni ulinzi ili zisije tumiwa vibaya na ikachukuliwa source ni yeye. "Tuelomishane"

Ninavyofahamu, mpiga picha wa Rais au Ikulu ni Bw Maro; na siyo Issa Muhidin Michuzi
 

Ninavyofahamu, mpiga picha wa Rais au Ikulu ni Bw Maro; na siyo Issa Muhidin Michuzi

Siwezi kubishana kwa hilo ya wezekekana one is a subordinate to the other, lakini Issa anatambulishwa rasmi kama mpiga picha wa rais na picha zote za shughuli za rais ni product yake.
 
Heee picha zote zinazohusu Rais Kikwete na ikulu ni mali ya Michuzi smh...yeye ndio aliyempigia kura peke yake?
 
Nijuavyo mimi Michuzi ni mpiga picha wa rais, hivyo ana access ya moja kwa moja na shughuli za kikazi za rais (Mf. ziara ya rais Marekani). Kuzuia upakuaji picha na taarifa ktk blog yake kwangu mimi, ni ulinzi ili zisije tumiwa vibaya na ikachukuliwa source ni yeye. "Tuelomishane"
Pamoja na kuwa kazi yake ni hiyo ya kuambatana na rais na kuchukua picha, Je taratibu za kazi ndivyo zinavyoelekeza? Anatakiwa achukue hayo matukio na kuweka ktk blog yake? Hizo taarifa anazochukua zinatakiwa kuwasilishwa wapi? HATA HIVYO UNAPOSEMA KURUGENZI YA HABARI YA IKULU "UNAIMANISHA YEYE HAHUSIKI NA KITENGO HICHO"
Tuache kutetea makosa yanayofanyika.
 
Back
Top Bottom