Siwezi kubishana kwa hilo ya wezekekana one is a subordinate to the other, lakini Issa anatambulishwa rasmi kama mpiga picha wa rais na picha zote za shughuli za rais ni product yake.
fredy maro huyo hana ubavu kama michuzi..misafara mingi michuzi yupo na jk....si unajua ushkaji tenaMuhidin Michuzi ni mpigapicha wa Rais tangu lini ? Ninachojua Michuzi alienda Ikulu kipindi kifupi kupiga picha kwa ajili ya blog yake. Mpiga picha wa Rais hivi sasa ni Freddy Maro.
Michuzi ndio anaonekana yuko fasta zaidi. Hata hivyo Maro ni mpiga picha rasmi wa ikulu. Huenda urasimu nao huchangia katika suala hili hasa ukizingatia kila mtu anafanya kazi asijiweke katika mazingira mabaya na wengine.
Mkuu,Sichangii Mada yako ila umeniudhi kuweka msemo wa kiingereza ambao wahenga wetu pia wanao. Kwani ungesema "Msemakweli ni mpenzi wa Mungu" ungepungukiwa nini?
Nijuavyo mimi Michuzi ni mpiga picha wa rais, hivyo ana access ya moja kwa moja na shughuli za kikazi za rais (Mf. ziara ya rais Marekani). Kuzuia upakuaji picha na taarifa ktk blog yake kwangu mimi, ni ulinzi ili zisije tumiwa vibaya na ikachukuliwa source ni yeye. "Tuelomishane"
Hii habari imenisikitisha sana ... yaani ofisi kubwa namna hiyo nayo imekuwa ya kiubabaishaji kiasi hichoo... Mungu wa mbinguni tusaidie na kuwarehemu wahusika maana ni ufisadi wa hali ya juuu ... ofisi kuendeshwa kiswahili swahili ni hatari sana........
Hawa wana siasa akina chadema hawalioni hili? kwanini wasilipue bungeni?Mambo ya Tz yanapunguza umri wangu wa kuishi duniani.watu wanahoja nzito sana halafu hakuna mtu wa kutoa majibu.tunaishije wakuu?
Hivi majuzi yalitolewa madai ya Kwamba kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inauza habari na imekasimisha habari za Rais kimaslahi kwa watu wengine na hasa kwa blog ya mwananchi mmoja anayeitwa Muhidin Issa Michuzi.
Mara ya kwanza sikuona sababu ya kuchangia hoja hiyo wala kuitolea ufafanuzi ama jibu, lakini kwa mara nyingine shutuma hiyo imejirudia katika mitandao mingine ya kijamii, hivyo nikajikuta nashawishika kuchangia hoja hiyo na kumweleza aliyeijenga na kuitoa:-
Kwanza, naamini kuwa Kurugenzi imesikia na inaifanyia kazi hoja hii. Isipokuwa niseme mawili tu ambayo nayaelewa kiundani:
· Kubwa ambalo nina uhakika nalo ni kwamba kamwe haijapata na haitatokea kwa Kurugenzi ya IKULU kuuza ama kukasimisha kimaslahi habari za Rais na Ikulu kwa mtu ama kwa kikundi cha watu. Madai haya ni sehemu tu ya politics za kawaida za media scene ya hapa kwetu Tanzania. Kila mtu anamtafuta mtu, kama vile hakuna mambo ya maana zaidi ya kuhangaika nayo.
· Jambo moja ni dhahiri sana. Ndani ya Kurugenzi ile wanaofanya kazi ni binadamu kama alivyo mjenga hoja mwenyewe. Hivyo, wanaweza wasiwe watu wenye uwezo wa kupindukia sana. Lakini Kurugenzi ile ina watu makini sana, wenye kuelewa wanafanya nini na wenye maadili ya msingi kabisa ya utumishi wa umma. Madai kwamba wanaweza kuuza habari za Rais ni completely laughable.
Tuendelee kujadili kwa hoja na weledi, uzushi na tuhuma zisizo na msingi kila wakati hazina maana.