Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inauza Habari za ofisi ya Rais Kikwete

"Katika kunufaika zaidi na habari za ofisi ya Rais, Blog ya Muhidin Issa Michuzi imeweka kizuio, kwa kiingereza wanasema, block visitors from right clicking or disable "copy and paste" to protect blog source code ili kuhakikisha habari za Rais Kikwete haziwezi kuchukuliwa na media au blog nyingine baada ya kuziweka kwenye blog yake."

Kuiacha kwa maksudi/malengo Tovuti Rasmi ya Ikulu iwe outdated kwa mlengo wa kukasimisha habari wakati kuna watu wanalipwa kwa kazi hiyo ni ufisadi na wizi wa pesa za walipa kodi wa nchi.

Hii nayo ni "ESCROW" nying
ine kwa mtindo mwingine
.

Technology inasonga mbele na hakuna uwezo wa kufunga. Nieleze picha yoyote unayohisi imezuiliwa niilete kwenye hii forum.
 
Technology inasonga mbele na hakuna uwezo wa kufunga. Nieleze picha yoyote unayohisi imezuiliwa niilete kwenye hii forum.

Pamoja sana mkuu.Kwa mujibu wa bandiko ambalo ndilo kiini cha mjadala huu, Blog ya Muhidin Michuzi inahusika sana.
 
Moja ya alama ya taasisi inayoanguka ni kutoweza ku update tovuti. Hili nilijifunza 1999 wakati najifunza mambo ya Website design. Wenyewe wanaita "cobwebsite"

Ikulu haina website, ina cobwebsite.
Ni aibu sana kuwa na Tovuti ya ofisi kuu ya serikali nchini ambayo inaachwa kuwa outdated(cobweb site) kwa sababu ya migongano ya maslahi.

Tovuti ya Rais wa Zanzibar inakuwa update kwa kila tukio linaloihusu ofisi ya Rais wa Zanzibar.

Hata Press release za kutoka Kurugenzi ya Mawasialiano ya Ikulu, mara nyingi huwa zina makosa mengi sana ya kiuandishi. Hiki ni kiashiria cha uwepo wa matatizo katika kitengo cha mawasiliano katika ofisi kuu ya nchi. Kwa lugha nyingine, kama ofisi ya Rais haiko makini katika utendaji wake, haiwezekani ofisi na taasisi zilizo chini yake zikawa makini.
 
Pamoja na kuwa kazi yake ni hiyo ya kuambatana na rais na kuchukua picha, Je taratibu za kazi ndivyo zinavyoelekeza? Anatakiwa achukue hayo matukio na kuweka ktk blog yake? Hizo taarifa anazochukua zinatakiwa kuwasilishwa wapi? HATA HIVYO UNAPOSEMA KURUGENZI YA HABARI YA IKULU "UNAIMANISHA YEYE HAHUSIKI NA KITENGO HICHO"
Tuache kutetea makosa yanayofanyika.

Kwa maelezo yangu yalijikita katika HOJA ya muanzisha uzi huu, kuwa, kwanini Kurugenzi ya Habari Ikulu inamilikisha habari zake kwenye blog ya Issa Michuzi na ambaye ana block watu wengine washindwe kuzipakua *download" na wao kuzitumia.
 
Wivu wa kike tu umewajaa na unawasumbua. Mbona hio tovuti ya Ikulu ipo uptodate sana tu? Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Ikulu
Halafu mnadhani Michuzi anategemea habari za Ikulu peke yake? Anaweza akaachana nazo na kuandika kibao zingine anazoacha na isiwe tatizo. Kuhusu kuuza habari hiyo nayo ni uwongo. Michuzi blog yake ni kuangalia bure. Wewe unayetaka kuiba picha ndiyo umezuiwa. Isitoshe habari za Ikulu huwa zinatika katika blogs zote mbona hamlalamiki?
Upungufu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ni kushindwa kupromote website yake na ama kufungua akaunti za twitter na facebook kama wafanyavyo wenzao. Hilo nalo inabidi liangaliwe, mambo ya kungoja habari hadi saa mbili usiku kwenye taarifa za habari ama magazetini kesho yake yamepitwa na wakati. Salva na wenzie angalieni hili
 
Tumtenganishe Salva na Ikulu yetu

Msomaji Raia

Toleo la 294
15 May 2013

PAMOJA na kuwa mwandishi kanjanja, lakini namfahamu Salva Rweyemamu. Yule Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ikulu yetu ya Dar es Salaam. Ni mwandishi wa habari mzoefu aliyefanya kazi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwenye sekta binanfsi na sasa serikalini.
Tangu alipoagana na sekta binafsi kwenda serikalini kuongoza kitengo cha Mawasiliano Ikulu, yamejitokeza mengi ambayo yanastahili kujadiliwa. Machache yake ni pamoja na hali ya kuporomoka kwa kiwango cha taarifa za Ikulu kwa umma; kukosekana kwa weledi katika uamuzi na utendaji wa Kurugenzi ya Mawasiliano; na dalili za kuigeuza Ikulu kuwa kijiwe cha kisiasa na vijembe; na udhalilishaji wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, utendaji wa Salva Rweyemamu umeendelea kuzua gumzo kwa baadhi ya watu, kila wakati anapofunua mdomo wake au kutumia kalamu yake. Hulka hii ya Salva inaelekea kuingilia eneo nyeti linaloweza kuharibu utakatifu wa Ikulu. Eneo nyeti hilo ni pale maneno ya Salva Rweyemamu yanapoweza kutafsiriwa kuwa ni maneno ya Ikulu.
Moja ya nukuu muhimu za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kuhusu Ikulu, ni pale aliposema "Ikulu ni mahali patakatifu". Yeye alikaa Ikulu miaka zaidi ya 23 na mpaka anaondoka alikuwa na jeuri na ujasiri wa kusema hadharani kuwa Ikulu ni mahali patakatifu. Watanzania walimwelewa na kumwamini hata kama wanaweza kutofautiana juu ya ni nini hasa kiini cha utakatifu wa Ikulu.
Utakatifu wa Ikulu kwa Baba wa Taifa ulianza mapema kabla hata hajazoea kukaa katika jengo hilo. Kwake yeye, aliona Ikulu ni eneo muhimu kwa utambulisho na utakatifu wa maamuzi ya kila siku kwa taifa. Kutokana na chuki ya Baba wa Taifa kwa ukoloni na wakoloni, alifikia hata kukejeli jumba hilo kwa kuwa lilikaliwa na wakoloni.
Kwa ufahamu na heshima yake kwa kitu kinachoitwa Ikulu, alipata shida sana kuona mtu anawezaje kuishi ikulu kisha akakandamiza, akahujumu uchumi, akaiba, akadanganya, akatukana, akafanya usanii, akafanya uhuni, akadhulumu, akapotosha, akaringia wananchi, akafanya biashara, akapigana na mkewe, au hata kupageuza Ikulu kuwa eneo la kufugia, kutunza ukoo wake na mambo mengine binafsi. Kwake Baba wa Taifa, Ikulu yalikuwa ni madhabahu ya taifa letu, mahali pa kuheshimiwa na kuogopwa.
Haikushangaza wengi, miaka michache baada ya uhuru, Baba wa Taifa alianza jitihada za kuhama Ikulu na kuishi katika nyumba yake binafsi iliyo Msasani. Alifanya hivyo si kwa sababu aliidharau Ikulu ya Magogoni, bali alikuwa anajilinda ili asiingie katika majaribu ya kuigeuza Ikulu kuwa ni nyumba ya ukoo wa Burito.
Aliona Ikulu ni ofisi na alikwenda kazini kama Watanzania wengine, kisha alirudi kulala Msasani katika nyumba aliyojenga mwenyewe kwa mkopo ambao alishindwa hata kuulipa na kukaribia kunyang'anywa.
Kutokana na hofu iliyoambatana na heshima kwa Ikulu yetu, Baba wa Taifa aliona Ikulu pawe ni mahali pa kukaribisha wageni wa kitaifa, kufanya shughuli za ofisi na kufanyia maamuzi muhimu ya kitaifa. Alijua yeye kama mwanadamu anaweza kuwa na hulka zisizohitajika na kuingilia maslahi ya taifa letu.
Hakuwa na maana kuwa marais watakaofuata wasiishi Ikulu kama yeye, bali alilenga kuonyesha eneo lile liwe zaidi ya pango la kuishi wanadamu wenye kutanguliza maslahi yao, familia zao na marafiki zao. Haishangazi kuona leo watu wanahasimiana kutaka kwenda kuishi katika jengo hilo la kikoloni.
Ukiiangalia Ikulu ya Baba wa Taifa na Ikulu yetu ya leo ni kama tuna Tanzania mbili. Ukiacha mengi yanayoweza kujadiliwa kwa nafasi yake, hili la matamko yanayotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano yanaacha maswali mengi na sononeko la mioyo kwa Watanzania wengi wanaoiheshimu Ikulu yetu.
Salva Rweyemamu alikuwa mwandishi mchambuzi na jicho la jamii kuhakikisha utukufu na utakatifu wa Ikulu unatunzwa. Kwa kalamu yake aliichambua Ikulu ya Benjamin Mkapa na kukaribia kuisambaratisha.
Alitusaidia sana ili tusianguke katika mtengo wa kumtukuza mpangaji wa Ikulu huku tukisahau kuwa utukufu wa mpangaji wa Ikulu hauna budi utokane na utukufu wa eneo na majukumu yake. Pamoja na mafanikio aliyoyapata akiwa Ikulu, Benjamin Mkapa alichambuliwa vilivyo na kalamu ya Salva. Laiti aliyoyakosoa akiwa nje ya Ikulu kama angeyaendeleza akiwa ndani!
Tangu aingie Ikulu, Salva amejijengea sifa moja kubwa kuhusiana na mwenendo wa matamko ya Kurugenzi yake. Sifa hiyo ni ile kusema asipostahili kusema na kunyamaza pale anapotakiwa kusema. Yamekuwapo mashambulizi mengi kuhusu mwendendo wa serikali hii na hasa huko jikoni (Ikulu). Masuala ya msingi yameibuliwa yaliyohitaji ufafanuzi wa Ikulu yetu lakini Salva alikaa kimya. Lakini kila yalipoibuliwa masuala ambayo si muhimu sana, Salva alikuwa mwepesi wa kuja juu na matamko yaliyoandikwa ovyo ovyo.
Mathalani, zilipotolewa tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti na wawekezaji, Salva aliandika taarifa ndefu iliyojaa utetezi wa Rais kama mtu binafsi badala ya kuitetea hiyo inayoitwa Taasisi ya Urais. Watanzania wanajua kuwa Taasisi ya Urais haivai suti na kwa hiyo isingeweza kuhongwa suti.
Wanajua kuwa ndani ya taasisi hiyo yumo mtu mmoja aitwaye Jakaya Kikwete, anavaa suti, zinampendeza na anazipenda. Wawekezaji kwa kuliona hilo, huenda walimpa takrima ya suti, iliyotafsriwa na Wikiliki kuwa ni hongo ya suti. Kurugenzi yetu ililipa suala hili uzito wa juu tena kwa kutumia lugha za kejeli na vijembe.
Wiki hii, Kurugenzi hiyo imetoa tamko la kumkejeli Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa kwa madai yake kuwa Rais Kikwete na timu yake walifanya kampeini za udini katika nyumba za ibada. Salva akatumia kodi za Watanzania si kukanusha tu bali kupiga vijembe.
Wote tunajua kuwa Rais Kikwete anaweza kuwa si mdini lakini ana dini. Dini yake haipaswi kuwa ya Watanzania na kimsingi si lazima iwe dini ya Salva. Dini ya Kikwete si dini ya Ikulu wala ya CCM. Watanzania wanasumbuliwa na udini unaotishia amani ya nchi. Waganga na waganguzi wanahitajika kutujulisha udini umetokea wapi na tuufanyeje.
Dk. Slaa ananukuliwa katika gazeti moja kuwa Rais Kikwete na timu yake ndicho chanzo. Iwe kweli au uongo haisaidii kwa sasa. Taifa letu limo katika tatizo kubwa la udini. Salva angekubali ukweli huu bila ulazima wa kupiga vijembe kwa kutumia nembo ya Ikulu kupiga kejeli na vijembe. Dk. Slaa kama waganga na waganguzi ametoa hoja, ijibiwe au ipuuzwe kama yalivyopuuzwa mengine mengine na Ikulu yetu.
Tatizo hapa ni kwa nini Salva aone matamshi ya Dk. Slaa ni muhimu kujibiwa kuliko masuala mengine mengi makubwa yanayosubiri ufafanuzi usiotolewa mpaka leo. Matumizi mabaya ya nembo ya Ikulu yanazidi kuzamisha utukufu na utakatifu wa Ikulu. Tusipojihadhari, mambo mabaya yatafanywa na watu walioko Ikulu halafu tutadai yamefanywa na Ikulu.
Nimshauri Salva akae kimya na kufurahia fadhila alizopewa na Jakaya kwa mkono wa Rostam Aziz.

- See more at: Raia Mwema - Tumtenganishe Salva na Ikulu yetu
 
Wivu wa kike tu umewajaa na unawasumbua. Mbona hio tovuti ya Ikulu ipo uptodate sana tu? Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Ikulu
Halafu mnadhani Michuzi anategemea habari za Ikulu peke yake? Anaweza akaachana nazo na kuandika kibao zingine anazoacha na isiwe tatizo. Kuhusu kuuza habari hiyo nayo ni uwongo. Michuzi blog yake ni kuangalia bure. Wewe unayetaka kuiba picha ndiyo umezuiwa. Isitoshe habari za Ikulu huwa zinatika katika blogs zote mbona hamlalamiki?
Upungufu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ni kushindwa kupromote website yake na ama kufungua akaunti za twitter na facebook kama wafanyavyo wenzao. Hilo nalo inabidi liangaliwe, mambo ya kungoja habari hadi saa mbili usiku kwenye taarifa za habari ama magazetini kesho yake yamepitwa na wakati. Salva na wenzie angalieni hili

rudi juu kasome thread tena...
 
Technology inasonga mbele na hakuna uwezo wa kufunga. Nieleze picha yoyote unayohisi imezuiliwa niilete kwenye hii forum.

ukiweza wewe kuitoa kwenye blog ya michuzi hainamaana wote wataweza ila hoja ni kwamba ziko blocked na haina maana kuwa akiziblock haiwezekani kabisa kuzipakua...
 
ukiweza wewe kuitoa kwenye blog ya michuzi hainamaana wote wataweza ila hoja ni kwamba ziko blocked na haina maana kuwa akiziblock haiwezekani kabisa kuzipakua...

What a contradiction! !!
 
Huo ni ufisadi mwingine....michuzi amechukua nafasi/ opportunity na anaitumia.lazima zile picha anazipeleka kwa handlers wake...sasa kuanzia hapo ndo udhaifu unaanza kujitookeza.labda hakuna mtu ambaye yuko dedicated na ku update issues za ikulu...ila pia huo ni udhaifu idala na wizara nyingi za serikali!!.vijana wengi wamemaliza vyuo it!.wawape ajira na itawafaa na lawama zitapungua!.kama agizo la rais wakati fulan mawazir wawe wanaongea na wananchi...??!.rais alikuwa na kawaida ya kuhutubia nchi kila mwisho wa mwezi... toka alivyoondoka bwana Marwa iliishia wap ile?..mara utasikia anaongea na wazee wa dodoma au dar ndo imetoka!!.hakuna utaratibu rasmi!.rais anatakiwa anafanya press conference kila mwez na waandishi nguli wa habari wenye weledi na sio makanjanja watakao uliza maswali...na kupitia hapo yy mwenyewe atajua udhaifu wa serikali yake sio outdated info!.
 
Wivu wa kike tu umewajaa na unawasumbua. Mbona hio tovuti ya Ikulu ipo uptodate sana tu? Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Ikulu
Halafu mnadhani Michuzi anategemea habari za Ikulu peke yake? Anaweza akaachana nazo na kuandika kibao zingine anazoacha na isiwe tatizo. Kuhusu kuuza habari hiyo nayo ni uwongo. Michuzi blog yake ni kuangalia bure. Wewe unayetaka kuiba picha ndiyo umezuiwa. Isitoshe habari za Ikulu huwa zinatika katika blogs zote mbona hamlalamiki?
Upungufu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ni kushindwa kupromote website yake na ama kufungua akaunti za twitter na facebook kama wafanyavyo wenzao. Hilo nalo inabidi liangaliwe, mambo ya kungoja habari hadi saa mbili usiku kwenye taarifa za habari ama magazetini kesho yake yamepitwa na wakati. Salva na wenzie angalieni hili
Watanzania tumepofushwa na nini/nani? Mtoa mada yuko 'very precise' jinsi Michuzi anavyonufaika na 'updated news' za Ikulu. Kila news-room ina haki za kupata picha za matukio ya Rais bila kikwazo, whether through copy-paste au dispatch from Mawasiliano Ikulu. Nini kisichoeleweka kuwa 'formal source' haziwi updated kumnufaisha Michuzi?

What if Michuzi ndio yuko responsible kuupdate pictures kwenye 'formal source' na hafanyi hivyo ili blog yake ipate visitors wengi na kujiongezea mapato through ads? Umepofushwa na nini hata kushindwa kuunganisha dots zilizowazi kabisa?

Tanzania ilipofikia inahitaji sana mtu kama mtoa mada maana kila mtendaji amekuwa "Mpigaji"! Hakuna mtendaji anayejari maadili ya utumishi wa umma; kila mtu anaangalia apige vipi fedha. Kila mmoja anaangalia kisogo cha mkuu wa kaya, inaudhi kweli!!
 
mbona povu linakutoka soma uzi vizuri wewe! ndomana ikulu imeja makanjanja watupu
 
well said mkuu.....mimi mwenyewe leo nmesoma uzi huu na nmeuelewa vilivyo nini mleta mada ana maanisha
 
Huo ni ufisadi mwingine....michuzi amechukua nafasi/ opportunity na anaitumia.lazima zile picha anazipeleka kwa handlers wake...sasa kuanzia hapo ndo udhaifu unaanza kujitookeza.labda hakuna mtu ambaye yuko dedicated na ku update issues za ikulu...ila pia huo ni udhaifu idala na wizara nyingi za serikali!!.vijana wengi wamemaliza vyuo it!.wawape ajira na itawafaa na lawama zitapungua!.kama agizo la rais wakati fulan mawazir wawe wanaongea na wananchi...??!.rais alikuwa na kawaida ya kuhutubia nchi kila mwisho wa mwezi... toka alivyoondoka bwana Marwa iliishia wap ile?..mara utasikia anaongea na wazee wa dodoma au dar ndo imetoka!!.hakuna utaratibu rasmi!.rais anatakiwa anafanya press conference kila mwez na waandishi nguli wa habari wenye weledi na sio makanjanja watakao uliza maswali...na kupitia hapo yy mwenyewe atajua udhaifu wa serikali yake sio outdated info!.

ni kweli rais hafanyagi mahojiano na waandishi nguli, na huyo michuzi ikulu kaingizwa kiushkaji tu kwa sababu ya ukaribu na mkulu.....
 
Nijuavyo mimi Michuzi ni mpiga picha wa rais, hivyo ana access ya moja kwa moja na shughuli za kikazi za rais (Mf. ziara ya rais Marekani). Kuzuia upakuaji picha na taarifa ktk blog yake kwangu mimi, ni ulinzi ili zisije tumiwa vibaya na ikachukuliwa source ni yeye. "Tuelomishane"

Point ya mleta mada ni kwanini habari zisiwepo kwenye blog/tovuti ya habari ya Ikulu? kama nimemuelewa. Blog ya Michuzi ni personal lakini ina habari kuliko blog/tovuti ya Ikulu na za Ikulu haziwi updated.

Hapa kuna tatizo na tusikatae.
 
Back
Top Bottom