Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeshindwa kazi; yatumika kumhujumu Rais Kikwete

kwani hizo hotuba zake sina saidia nini wanachi wakati kila siku hali inazidi kuw mbaya kwa wananchi .
yeye anapanda ndege kila siku kwenda kucheki balance .......sisi hata gari za wagonjwa au zima moto hakuna
 
Kulikuwa hakuna cha maana atakachoongea kwani tokea aingie madarakani hakuna hotuba yoyote yenye mwonekano /mwelekeo wa kutoa matumaini ya maisha bora kama alivyoahidi.Labda ahutubie aseme familia yake imesonga mbele sana kwa muda mfupi kwani wanamiliki mali za kutosha.
 
sijawah kufatilia hotuba za huyu prezidaa ila jana nilikaa na kusubiri kwa hamu sana kusikia ataongelea nini kuhusu dr Ulimboka na mgomo wa madaktari, NADHANI ALIOGOPA KULIKOROGA ZAIDI AKAINGIA MITINI

jamni hebu muacheni Rais wangu kipenzi kwani yupo anajiandaa na mwezi mtukufu wa ramadhani kwani si mnajua mabo ya tende za iran!
 
wananchi mna moyo hivi kweli mnakaa chini mnaacha shuhuli yenu mnasubiri kudanganyika
 
Kwa niaba ya Chama changu makini CCM naomba kuwataka radhi Wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano mliokesha usku kucha kusubiri hotuba ya Mpendwa Rais wetu Mh Jakaya bila mafanikio hivyo naomba mtusamehe kwa uzembe uliofanywa na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kwa kutokutoa Tangazo la Mh Kuhairisha kuhutubia Taifa siku ya tararehe 30/06/2012.

Kwa sisi wananchi na wapenzi makini wa Chama cha mapinduzi tunaona kuna uzembe wa hali ya juu uliofanywa na wasaidizi wa Rais na kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kutokana na sakata hili ambalo hadi kufikia sasa bado wahajatoa kauli kwa vyombo vya habari ya kuhairishwa kwa hotuba ya Rais.

Kutokana na Rais kushindwa kuhutubia Taifa hapo jana baada ya Taarifa kuwa zimetolewa na Vyombo vya habari Wananchi wapo katika taharuki kubwa kwani hawajui kitu kinachoendelea na kitu kilichompata Rais Wetu hadi kufikia kushindwa kuhutubia Taifa.

Kwasasa Tunaitaka Kurugenzi ya Mawasilino Ikulu kuwajibika kwa kuupotosha Umma juu ya jambo hili nyeti kwa Taifa na aidha tunawataka kutoa tamko kwa vyombo vya habari na kuwaomba radhi wananchi wote waliokesha ucku kucha kusubiri hotuba ya Mpendwa wao Rais na kupelekea wengine kushindwa kwenda kwenye Ibada siku leo.

Hakuna cha kushangaza kuhusiana na hii Serikali DHAIFU...Eti Rais atahutubia Taifa leo kumbe ni usanii mtupu!!!!
 
Rais alitoa hotuba ambayo imesifiwa na watu wengi jana asubuhi (15 Desemba 2013) kwenye mazishi ya Madiba. Leo saa 5:27 asubuhi (11:27am) ya tarehe 16 Desemba 2013, yaani zaidi ya masaa 24 tangu tukio hilo, eti Ikulu ndio wanatoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu tukio hilo na kuiwekea tarehe ya jana.

Zifuatazo ni sababu 10 kwa nini Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ni mzigo mkubwa kwa Rais Kikwete, serikali na wananchi kwa ujumla. (Sijui nao waitwe na Kamati Kuu ya CCM kuhojiwa?)

1. Kushindwa kutoa habari zinazomhusu Rais kwa muda unaotakiwa

2. Kushindwa kutoa habari zinazomhusu Rais kwa Kiswahili, Kiingereza na kwa mfumo wa electronic media
(yaani redio na TV). Wao daima hutoa taarifa kwa Kiswahili tu, hata kama Rais alikuwa anaongea Kiingereza. Magazeti ya Kiingereza yanapotafsiri taarifa za Ikulu kutoka Kiswahili, maneno hayaendani na maneno halisi aliyoongea Rais (real meaning lost in translation)

3. Kushindwa kutoa hotuba za Rais kwa wakati
(Rais akihutubia leo, hotuba yake hutolewa kesho au kesho kutwa)

4. Kushindwa kuwa na tovuti rasmi ya Ikulu, mpaka leo wanatumia blogspot

5. Kushindwa kuwa na professional email address
(wanatumia ikulucommpress@googlemail.com)

6. Kushindwa kumuweka Rais awe karibu na media
. Hii ni pamoja na kushindwa kumshawishi Rais afanye mikutano ya mara kwa mara na media

7. Kufanya PR blunders mara kwa mara
(kama walivyotoa picha ya Rais akiwa anabembea Jamaica wakati nchi ikikumbwa na matatizo makubwa kama mgao wa umeme)

8. Kushindwa kumsaidia Rais kujenga vizuri taswira yake
(image) kwenye jamii kupitia kwa media

9. Kushindwa kumsaidia Rais kwenye reputation management kwenye social media
(yaani kwenye mitandao kama humu JF, Twitter, Instagram na Facebook)

10. Kutoa taarifa za mambo trivial (madogo madogo) au ya shughuli za kibinafsi za Rais ambazo siyo habari na hazisaidii kumjenga Rais
(eg kutembelea wagonjwa fulani hospitalini au Rais kukutana na Ray C). Siyo kila kitu anachofanya Rais lazima kipelekwe kwa media, hakuna uchujaji wowote unaofanywa kujua matukio gani ni shughuli binafsi za Rais na siyo habari au yanaweza kuleta taswira mbaya.
 
Punda akijibebesha mzigo mwenyewe hastahili kuchapwa viboko ili mzigo ufike. Hiyo kurugenzi ya Habari ni mzigo ambao Kikwete amejibebesha mwenyewe kwa kuwaweka jamaa zake waliomsaidia kuwatukana akina Salim Ahmed Salim in 2005. Acha abebe mzigo wake mwenyewe...
 
Lugha ya taifa ni kiswahili, ni vema taarifa za ikulu zikaandikwa kwa kiswahili muda wote. Tusikiabudu kiingereza sio lugha yetu.

Kipengele chako cha pili kirekebishe kisomeke vema kinajichanganya.
 
Tangu mwanzo tulipoona anahangaika kuingia Ikulu kwa kupitia dirishani, wenye akili tukajua hakuna la maana huko mbele ya safari!
 
sasa hamsemi tena ni Chadema..eh.Sasa mnarudi nyumbani pa problems.Nyumbani pa problems zinazowatafuta watanzania.
 
Back
Top Bottom