Kurugenzi ya Habari Ikulu, yatoa tahadhari kwa watu waliotumiwa Barua za kugushi Mhuri wa Ikulu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuwatahadharisha kuwa kuna watu wametumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuchapisha na kusambaza barua kwa Kampuni Binafsi na Wakurugenzi Watendaji wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya kile kinachodaiwa kuwa ni "Mkutano Mkuu wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 21/09/2016 hadi 23/09/2016"

Mnataarifiwa kuwa barua hizo zilizotiwa saini na muhuri wa kughushi na ambazo hata maelezo yake hayaeleweki vizuri hazijaandikwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kwa maana hiyo zimeandikwa na watu wenye nia mbaya na wanaolenga kujipatia fedha kwa utapeli.

Yeyote aliyepokea barua hizo azipuuze na achukue hatua mara moja kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola kwa kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu haijaandika barua hizo na haitambui Mkutano huo.

Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuueleza umma kuwa uendelee kupokea taarifa sahihi zinazotolewa kupitia vyombo vya habari na pale ambapo kuna mashaka juu ya taarifa zenye nembo ya Ikulu wasisite kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu zilizotajwa katika anuani ya mawasiliano hapo juu.

Tafadhari atakayepata ujumbe huu umtaarifu na mwenzake.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

17 Septemba, 2016
uploadfromtaptalk1474126712246.jpeg
 
Hahahaha hii nchi sometime unaweza kucheka mwenyewe ukifikria namna tunavyoendesha mambo yetu. TUNA SAFARI NDEFU SANA.. BABA MAGUFULI MAMBO MABAYA WATU WATASAKA HELA KWA NJIA NYINGI NAONA UHALIFU UKIANZA KUONGEZEKA SOON
 
Tusipoziba ufa tutajenga ukuta very soon, tujiulize maswali kulikoni hadi watu kufikia kuichezea madhabahu ya nchi "Ikulu ni mahali patakatifu" kuna mahali lazima pamedhoofu ila hatujapaona, inabidi mamlaka zote zishirikiane kuwabaini hao watu haraka sana na watiwe kizuizini
 
Hivi wameshindwa kubaini chanzo cha hizo barua? Dispatch books hazioneshi ni nani aloyezipeleka? Kama ni email au fax nini kazi ya TCRA? Mbona UKUTA walikuwa madhubuti?
TCRAwanakamata eti wanaomuambia mkuu ukweli. Mie siiti kutukana naita kusema ukweli unaouma.
 
Duh!Wabongo noma!

Mbona hii rahisi kui track mwanzo wake! Wale viongozi wa UVCCM Arusha waliokamatwa na vitambulisho vya TISS (ambacho ni kitengo chini ya ofisi ya Rais) ndio wa kuanza nao. Tahadhari zilianza kutolewa siku nyingi kuhusu vijana hao lakini kama kawaida yetu kwa vile ni wa ccm zikapuuzwa na pengine madhara yalishakuwa makubwa na hatujui ni kiasi gani.
Na sio ajabu huo mchezo hata hapo mtaa wa Lumumba wapo wanao ufanya maana wanajua mpaka ratiba za mwenyekiti wao, ccm na watu wake ni hatari!
 
Mbona hii rahisi kui track mwanzo wake! Wale viongozi wa UVCCM Arusha waliokamatwa na vitambulisho vya TISS (ambacho ni kitengo chini ya ofisi ya Rais) ndio wa kuanza nao. Tahadhari zilianza kutolewa siku nyingi kuhusu vijana hao lakini kama kawaida yetu kwa vile ni wa ccm zikapuuzwa na pengine madhara yalishakuwa makubwa na hatujui ni kiasi gani.
Na sio ajabu huo mchezo hata hapo mtaa wa Lumumba wapo wanao ufanya maana wanajua mpaka ratiba za mwenyekiti wao, ccm na watu wake ni hatari!
Ni kweli kabisa. Tena ni rahisi sana kuwadaka waliofanya hili jambo, labda kuwe na mizengwe ya kuwabaini wahusika. Wanaweza kuanzia na waliopewa hizo barua halafu waliopewa watawataja wamezipata wapi. Ni rahisi sana. Kama waliopewa hizo barua wanajulikana, kwa nini wasitaje walizipata kutoka kwa nani hizo barua?
 
TCRA tusaidieni kwa hili maana ni hatari sana, naamini inteligensia itafanya kazi yake na hatmae mhusika kufikishwa kwenye vyombo vya usalama.
 
Nakumbuka kuna kipindi wabunge walikuwa wanatumiana vimemo bungeni wakawa wanaghushi saini ya mh Pinda. Watz ni noma sana kwa haya mambo.
 
Kwenye taarifa ya Msigwa anataja "nembo ya ikulu",nimejaribu kuitafuta hiyo anayoiita nembo ya ikulu kwenye taarifa zake anazozitoa sijaiona,Ipo wapi hiyo inayoitwa " nembo ya ikulu",kwenye taarifa za msigwa?Au "nembo ya Taifa" ndiyo inaitwa nembo ya ikulu?
 
Hivi wameshindwa kubaini chanzo cha hizo barua? Dispatch books hazioneshi ni nani aloyezipeleka? Kama ni email au fax nini kazi ya TCRA? Mbona UKUTA walikuwa madhubuti?
Dispatch books za wapi sasa? Kurugenz ikulu au hao matapeli? Mtu anajijua tapeli atatumia dispatch book kweli?
 
Back
Top Bottom