Kurugenzi ya Habari Ikulu ifafanueni vizuri 'Vyeti Feki' nao 'Kulipwa' kwani huku Mitaani Mbwembwe na Hofu zimetawala

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,585
2,000
Kwako Ndugu na Kamarada ( Comrade ) Gerson Msigwa ( Msemaji wa Rais Ikulu ) ambaye najua pia kuwa huwa unanisoma mno GENTAMYCINE hapa JamiiForums ( tena 24/7 ) hebu ama hapo ulipo nae sasa umuulize Mama au lifafanuliwe vyema nawe kwani ninayoanza kuyaona kwa 'Wahanga' nalo huku Mitaani ni makubwa.

Kuna Dada ( aliyekuwa Mwalimu katika Shule moja maarufu sana Wilaya ya Kinondoni ) ambaye ni 'Mhanga' wa kukutwa na 'Vyeti Feki' tokea asikie Taarifa hi 'Tata' sasa anazunguka Mitaani hasa kwa wale Watu waliomcheka Yeye Kukosa Ajira hiyo akiwa ameshika Chupa ya K-Vant na 'anawakoga' kwa Kuwaambia kuwa 'Watamkoma' akilipwa ( akizikamata ) Pesa zake ambazo Mwenyewe 'anatamba' kuwa atalipwa kati ya Tsh 45 Milioni hadi Tsh 55 Milioni.

Tafadhali lifafanuliwe haraka lijulikane.
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
42,938
2,000
Vyeti feki hawatalipwa
Nimesikia hotuba vizuri sana
Kasema waliopunguzwa hasa darasa la saba ndo watalipwa ...
Na kasisitiza sheria izingatiwe..
Sasa vyeti feki ni forgery. .watalipwa Kwa sheria ipi?
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,585
2,000
Vyeti feki hawatalipwa
Nimesikia hotuba vizuri sana
Kasema waliopunguzwa hasa darasa la saba ndo watalipwa ...
Na kasisitiza sheria izingatiwe..
Sasa vyeti feki ni forgery. .watalipwa Kwa sheria ipi?
Asante kwa huu 'Ufafanuzi' wako 'Jadidi' kabisa Mkuu. Huwa nakuamini na Kukubali pia hapa JF.

Hivyo ngoja basi nitoke nje mara moja nimwambie huyu Dada aliye na 'Matumaini' ya Kulipwa kuwa 'Msoto' unaendelea na tena nitamtisha kuwa Wote waliokutenda na 'Vyeti Feki' wanasakwa na Jamhuri ili Washtakiwe.

Nadhani hata hii Pombe yake iliyompanda 'Kichwani' itamtoka ghafla.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
9,465
2,000
Mama jana kasema tusiwe watumwa wa sheria maana sheria zipo kwa ajili yetu wanadamu.

Namuomba mama Samia kwa huruma yake na utu wake, awalipe chochote kitu watu wa vyeti feki maana ni kweli walihudumu na jasho lao lipo ktk kazi waliyofanya.

Sisi wenyewe tusio na vyeti feki hatujakamilika, hata wanasiasa nao hawajakamilika maana wao kufanya udanganyifu katika masuala ya kura ni jambo la kawaida
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
17,163
2,000
Vyeti feki hawatalipwa
Nimesikia hotuba vizuri sana
Kasema waliopunguzwa hasa darasa la saba ndo watalipwa ...
Na kasisitiza sheria izingatiwe..
Sasa vyeti feki ni forgery. .watalipwa Kwa sheria ipi?
Kwanza masuala ya vyeti feki ulikuwa ni uonevu na ukatili kupindukia.

Ukiona unataka kufanya jambo halafu litabagua watu tayari jambo lenyewe linapoteza uhalali.

Vyeti feki ni kosa, lakini kwanini uhukumu watu wengine halafu uache JESHINI, POLISI na Wanasisasa. Kwamba sheria zina macho ???

Mimi nina watu watatu wa karibu ni wanajeshi na wana vyeti feki ila wako kazini, na wengine mpska mission za nje wanaenda.

Above all, pesa za PSSSF siyo za serikali, ni makato ya watu waliokuwa wanaweka wakati wa utumishi wao, kuzikatalia ni DHULMA, ulishawafukuza kazi basi hiyo adhabu inatosha. Wapewe pesa zao.

Mimi ninavyojua darasa la 7 wengine waliokuwa wamefutwa walirudishwa kazini.

Na hata hawa vyeti feki ni darasa la 7 vile vile unless wakifeki mpaka vyeti vya darasa la 7. Sisemi na wao warudishwe kazini, ninachosema wapewe pension zao ni haki yao.

Kwenye pension hakuna pesa ya serikali wala mlipa kodi hata 100 kwanini serikali iwadhulumu au kuwakatalia???
 

Jon Stephano

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
5,786
2,000
Yaani 'Tapeli' ambaye hata Kisheria ni 'Mhalifu' alipwe? Samahani Mkuu waya zako za Kuratibu Mfumo wako mzima wa Akili na Ubongo una uhakika zimekaa sawa?
Tapeli mkuu jizi la rambirambi na matrilion na kodi za watanzania lililodhani litaishi milele liko underground sasa hivi linaliwa na funza.

Mungu fundi na halirudi tena na life tena huko lilipo.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,585
2,000
Mama jana kasema tusiwe watumwa sheria maana sheria zipo kwa ajili yetu wanadamu...
Kuna Watu nilikuwa nikiwaheshimu sana hapa JamiiForums hasa kwa Michango yenu ila taratibu sasa kwa kuja na Hoja zenu zenye Huruma za Kinafiki kwa 'Wahalifu' niseme tu kuwa nitaanza Kuwadharau na kuwaona ni 'Hopeless' wakubwa tu.
 

jkipaji

JF-Expert Member
Sep 22, 2019
1,658
2,000
Asante kwa huu 'Ufafanuzi' wako 'Jadidi' kabisa Mkuu. Huwa nakuamini na Kukubali pia hapa JF...
Si umwache ajifariji aongeze siku za kuishi kuliko kumkatisha tamaa? Ya Mungu Mengi huwezi jua alilompangia Mjaa wake!!
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
41,585
2,000
Kwanza masuala ya vyeti feki ulikuwa ni uonevu na ukatili kupindukia.

Ukiona unataka kufanya jambo halafu litabagua watu tayari jambo lenyewe linapoteza uhalali...
Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akilipitisha hili na kuruhusu Walipwe ndiyo utakuwa mwanzo wangu wa Kumdharau.

Yaani Crooks walipwe? Are we Serious?
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,716
2,000
Waliotumia vyeti vyeki kusomea fani flaniflani, wakafaulu, wakaajiriwa na kulitumikia Taifa kwa miaka mingi kwa ustadi mkubwa wanapaswa kulipwa at least michango yao iliyokatwa kupelekwa kwenye mifuko.

Serikali inaweza kuamua kubaki na % iliyochangia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom