Kurugenzi Serikali ya Mitaa (DLG) - TAMISEMI barua za uhamisho zimerundikana, ukiwafuata Mitumba wanachomoa yako kwa hongo ya laki 6

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
378
571
Utaratibu wa kutoa majina ya watumishi waliokidhi vigezo vya kuhama kwenye tovuti ya TAMISEMI kila mwezi wa Juni na Desemba umeshakufa. Kwa sasa barua zimerudikana pale idarani kurugenzi ya serikali za mitaa Mitumba.

Barua za watumishi waliokamilisha tàratibu za kuhama zote baada ya kupitishwa na ma-DED anakotaka kuhamia na anakotoka na baadae RAS wa mkoa anaotoka na kufikishwa wizarani pale zinapakiwa na haitashughulukiwa mpaka utakapoenda kuwaona.

Watumishi kadhaa waliofika pale kulalamika wapo ambao wamesubiria zaidi ya miaka 2. Mtumishi mmoja ambaye jina linahifadhiwa aliomba uhamisho kutoka Mtwara Mkindani na kufikishwa TAMISEMI mwaka jana alitakiwa kuona jina lake Desemba 2019 au Juni 2020, amedai wizara haijawahi kutoa majina tovutini hata moja katika kipindi hicho lakini tumekuwa tukishuhudia watumishi wakihama kimyakimya.

Mtumishi mwingine niliyekutana nae akitokea Singida licha kugoma kutaja Halmashauri anayotoka na anakotaka kuhamia amedai kuwa aliambiwa na mwenzake kuwa alihamia halmashauri yao baada ya kutoa rushwa ya laki 3, amefika akiwa na pesa hiyo baada ya kufanikiwa kumpata dalali hapo wizarani anadai atoe laki 6.

Inadaiwa afisa husika anachukua laki 3 na watumishi wote tunajua hivyo lakini kumpata muhusika mwenyewe ni shida mpaka upitie kwa madalali ambo huongeza cha juu. Mtumishi mwingine mfanyakazi katika idara nyungine pale wizarani alidai kuwa mambo ya hovyo yamejirudia kama enzi za Katibu Mkuu Sajini aliyewahi kutumbuliwa na Mhe. Rais.

Aliendelea kueleza enzi za Sajini kupata u-DED au ukuu was idara kwenye halmashauri ulilazimika kutoa rushwa ya milioni 5. Tunaomba mamlaka husika kuondoa kero hii. Kwani kila anayekubaliwa kuhama tena kwa kujihamisha ili mpaka kukubaliwa ulikotoka na unakohamia wamezingatia sababu za msingi watumishi hawa walizotoa.
 
Kwa sasa tupo kwenye uchaguzi
Hebu acheni kwanza dunia ipite (in member's voice)

Hapana , Tamisemi ipo chini ya Ofisi ya Rais na inaongozwa na Waziri makini na mchapa kazi Mr Jaffo lakini tatizo linalotajwa hapa sasa linaota magamba pamoja na kwamba wizara imejiwekea taratibu nzuri sana za kushughulikia maombi ya uhamisho, binafsi nina ndugu yangu yeye ameitwa Dodoma zaidi ya mara tatu eti barua zinapotea? kweli barua inapoteaje ndani ya ofisi ya serikali yenye watumishi walioenda shule?

Barua inapotea mara tatu kwa HR yule yule kama sio dalili za ku solicit rushwa ninini hiyo, mwaka wa tatu sasa unaishia yeye ni mwendo wa kupanda ma basi na pikipiki kwenda huko kwenye ofisi za Tamisemi nje ya mji sijui wanaita Itumba... , kijana huyo tayari alishatoa kitu kidogo nafikiri ni kwa middle man pale ofisini na sasa anasubiria aone kama atasaidiwa na kwa maelezo yake wakubwa hawana matatizo kabisa tatizo wamekabidhi madaraka makubwa kwa vijana ambao nao tamaa imewajaa maungoni mwao
 
Laki 6 watakuwa wamempata mhusika kabisa. Mimi jamaa yangu alitoa milioni moja kuhama , baaada ya barua yake kukaliwa kwa miaka 3. Umenikumbusha Comrade Jumanne Sajini wapi kijana yule kwa sasa?
 
Uwajibikaji sekta ya utumishi wa umma umeongezeka, siyo?

Jafo acha kukata mbuga za Uchaguzi angalia subordinates wako wanavyojitahidi kuharibu image ya Wizara yako na kama utapenda ushahidi ita wenye matatizo ya uhamisho waje kwako uone Dodoma itakavyojaza watu
 
Laki 6 watakuwa wamempata mhusika kabisa. Mimi jamaa yangu alitoa milioni moja kuhama , baaada ya barua yake kukaliwa kwa miaka 3. Umenikumbusha Comrade Jumanne Sajini wapi kijana yule kwa sasa?
Hili jamaa jumanne sajini kapita kura za maoni huko kwetu butiama shenzi kabisa
 
Hii wizara ipo chini ya rais, ina maana ofisi ya rais inachukua rushwa???? Yaani Dkt Magufuli anachukua rushwa??? Hao wafanyakazi wanaofanya hivyo hawajipendi. Lingine watanzania tuwe tuna ripoti matukio ya rushwa PCCB ili waweke mtego.
 
Hii wizara ipo chini ya rais, ina maana ofisi ya rais inachukua rushwa???? Yaani Dkt Magufuli anachukua rushwa??? Hao wafanyakazi wanaofanya hivyo hawajipendi. Lingine watanzania tuwe tuna ripoti matukio ya rushwa PCCB ili waweke mtego.


Kura za maoni ndani ya CCM zilijaa rushwa PCCB wapi wamekamata tukio na kulipe[eka Mhakamani? zamani wakati vitendea kazi vikiwa duni hili tatizo halikuwepo kabisa kwani ilikuwa ukiomba tu basi tangazo linalofuata utakuta jina limo lakini baada ya kufanya maboresho ya kuweka kumbukumbu kwenye database za wizara na kupunguza wafanyakazi hewa tatizo limejitokeza na rushwa juu hii yote nafikiri ni kati ya yale majanga yanayoitwa "Man made"
 
Jafo acha kukata mbuga za Uchaguzi angalia subordinates wako wanavyojitahidi kuharibu image ya Wizara yako na kama utapenda ushahidi ita wenye matatizo ya uhamisho waje kwako uone Dodoma itakavyojaza watu
Umempa wazo nzuri awaite wenye matatizo ya uhamisho wizarani kwake ofisi ya wazi kama alivyokuwa anafanya Makonda.
 
Umempa wazo nzuri awaite wenye matatizo ya uhamisho wizarani kwake ofisi ya wazi kama alivyokuwa anafanya Makonda.

Akiwaita wote wenye tatizo la uhamisho hapo Dodoma hapatatosha kwani neno "Njoo kesho au wiki ijayo" limekuwa ni sara ya bikra Maria kwa hao HR vijana wa Jaffo tena hawana hata aibu hawaulizi hata kuwa umetokea wapi lakini kikubwa nilichogundua tatizo kubwa pale hawana malengo ya kazi na hakuna mtu wa kufanya checks kuona kuwa kila mmoja kafanya kazi na kufikia target yake...Poor Supervision delivers poor service!
 
Nitapambana Na Rushwa Bila Kigugumizi Chochote Na Dawa Ya Jipu Ni Kulitumbua. Nimejipa Kazi Ya Mtumbua Jipu
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom