Kurudishiwa pesa iliyokatwa baada ya card kumezwa ATM NMB

Cincinnati

Member
Jul 23, 2019
24
8
Wakuu, habari. Wiki iliyopita nilienda ATM kutoa pesa shs laki 3. Baada ya kuingiza kadi na kucommand itoe pesa, ghafla ATM card yangu ilimezwa na ATM ikazima na kuwaka tena ndani ya sekunde kadhaa bila kutoa pesa yoyote wala risiti. Ila kwenye simu yangu ikaingia message kuwa nimeitoa ile pesa na salio limepungua.

Sikupoteza muda nikaenda branch wakasema pesa itarudi ndani ya masaa 24. Nimekaa leo ni siku ya 5 kila nikiangalia salio hamna kitu. Msaada kwa anaejua haya mambo, ni steps gani napaswa kufata nirudishiwe pesa yangu maana nina wasiwasi na majibu ya wafanyakazi wa pale sio mazuri
 
Kuwa mpole tu itarudi. Iliwahi kunitokea halafu atm ya benki tofauti na yangu. Waliniambia ni kweli tumeona hela hsijatoka ila itachukua wiki mbili au tatu. Ilikuwa hela ya mwisho kwenye akaunti iniwezeshe kusavaivu two weeks! Ile hela ilirudi baada ya mwezi nafikiri!
 
Mkuu hujui kudai hela?Unatukana,unadai kumuona boss, unapiga simu makao makuu,unatishia kufunga akaunti. Unadai namba ya mkurugenzi mkuu mpaka wanakupa nhela yako fasta
 
Mkuu hujui kudai hela?Unatukana,unadai kumuona boss,unapiga simu makao makuu,unatishia kufunga akaunti.Unadai namba ya mkurugenzi mkuu mpaka wanakupa nhela yako fasta
Hahaa. Mkuu hvyo mm siwezi. But ninavyofatilia hiyo hela ni kama naomba mkopo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom