Kurudisha mabinti waliopata mimba shuleni ni kunyoosha mikono juu na kulikabidhi taifa letu kwa wakoloni mambo leo kwa ajili ya mkopo wa bil 600

Acheni watoto nafasi wasome...mngejua mtoto wa kike anavopata shida ktk elimu mngewaacha tu!kwa walosoma Day scholars watanielewea nimesoma DSM firm Primary mpk High school...Changamoto ni kubwa enzi zetu kulikua hakuna bodaboda wala bajaj,madaldala haya madereva na kondakta ilikua inahitajika muongozo wa Mungu tu tusijihusishe kwenye mapenzi,bado wahuni wa mitaani plus wanafunzi wenza wa kiume..

Kuna wanafunzo wanatiwa mimba na wazazi wao (baba zao kabisaa wa kuwazaa),kaka zao,babu zao n.k Km mlezi au mzazi ambae jamii imemuamini anamtia mimba anaemlea unategemea kizazi cha aina gani au kosa La huyu binti ni lipi?
Serikali haijakurupuka juu ya hili namuunga mkono Maza 100% kuna mengi mitaani,mashuleni na katk mazingira mengine mabinti wanakutana nayo hvyo kwa mtoto aliyepata mimba kwa bajati mbaya akizaa na kurudo shule atasoma..ila kama alikua mcharuko hatarudi shule tena ataishia tu kuhangaika baasi..na sio wote watarudi shule.Hakua kazi ngumu kama kulea!
 
Kuna binti jirani yetu,alikuwa na ki boyfriend chake enzi hizo mi wakusoma, ikawa tukikutana ananisimulia jinsi alivyokuwa anasikia raha yule boy akimkumbatia,akimbusu, akimpiga matouch

Sasa na mimi nikawa natamani, lakini kila nikitongozwa nakumbuka kuna mimba,na shule yetu ukipata mimba unafukuzwa kwa fedheha hapo hapo genye zote zinakata

Shule niliyosoma tulikuwa tunapimwa mimba kila baada ya miezi 3,ilitusaidia kwa kiasi kikubwa kujilinda na ngono zembe!!!
Mtazamo wako kwenye hili ni upi?.je warudi au wasirudi?.
 
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua kisha akirudi shule akawa anasoma na mabinti ambao hawajawahi kubikiriwa, hatakuwa na ushawishi mbovu kwao ili waonje utamu wa ngono? Tumejustify mapenzi kabla ya kumaliza shule

Fikiria kijana mvuta bangi ambae alikosa malezi na akaacha shule alafu ukrudisha asome kisa tu unalazisha amalize shule. Hii sio justification kuwa kuvuta bangi na utoro sio kosa?

Mkopo wa bil 600 umetufanya tujikabidhi kwa wakoloni mambo leo. Hivi kwa rasilimali tulizonazo ndio tumelainika kwa wakoloni namna hii?
Rasilimali hazisaidii kwa sababu za ufisadi, tamaa, wizi, upumbavu, ujinga, akili finyu. Miaka 60 ya uhuru nchi hii ingekuwa mbali sana. Ingekuwa inajiendesha kiuchumi lakini tumeshindwa. Kwa hiyo tumebakia kukopa na kukubali masharti ya wakopeshaji.
 
Ulivyompuuzi unadhania maendeleo ni kuruhusu watoto wasio na maadili kurudu shule.
Maadili gani wewe?.Unajua watoto wakike wanakutana na changamoto kiasi gani kwenye maisha yao.Inaonekana huna hoja ya maana ila kwavile Jpm alikua tofauti na hili swala ndo nawewe unajitutumua hapa.Eti maadili,maadili kwenye mimba tu,kwenye ufisadi na mambo mengine ya ovyo yanayofanywa na viongozi uyaoni.
 
Ngoja saizi tuanze kuvipa mimba...alafu tunamalizana kifamilia
Hapana ndugu tudeal na wakubwa wenzetu(wake zetu). Hawa watoto ni wa kuwahurumia tu. Akili zao zipo juu juu wanahitaji kuongozwa katika njia njema ya kuwavusha maishani. Nipo nawafundisha kwenye kijiwe changu huku nawaona jinsi wanavyohitaji watu wema kwa ajili ya kuwajengea msingi bora wa maisha yao. Binafsi nimeapa kuwa na mchango chanya maishani mwao.
 
Wewe ni bonge LA Poyoyo, hufikirii kuhusu watoto wanaobakwa na hawaezi kusema, vishawishi wanavyokumbana navyo, umaskini uliokithirii na mengine. Wewe unaongea ujinga hapa, mpuuzi

Hiyo hoja yako inazua swali: kwa nini wanapata mimba? Iwapo sababu ndio hizo, tutegemee shule kujaa watoto-wazazi kwa kuwa zaidi ya 70% ya WaTz bado ni maskini. Uthibitisho ni pale Serikali ilipoondoa ada, wakaandikishwa watoto wengi.
 
Kaa kimya
Tajikistan ndani ya miaka 60 ya uhuru chini ya CCcM imeshindwa kuwa huru hadi mabeberu wameanza kuingilia tamaduni zetu.Kuna siku mabeberu watataka wamtie Rais kisa nchi ina Rais mwanamke.Nani wa kulaumiwa?

Yaliyotokea Uganda tayari ni red light kwetu ila maCCcM bado yanang'ang'ania kuongoza nchi ambayo imeshawashinda.
cxJ.jpg
 
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua kisha akirudi shule akawa anasoma na mabinti ambao hawajawahi kubikiriwa, hatakuwa na ushawishi mbovu kwao ili waonje utamu wa ngono? Tumejustify mapenzi kabla ya kumaliza shule

Fikiria kijana mvuta bangi ambae alikosa malezi na akaacha shule alafu ukrudisha asome kisa tu unalazisha amalize shule. Hii sio justification kuwa kuvuta bangi na utoro sio kosa?

Mkopo wa bil 600 umetufanya tujikabidhi kwa wakoloni mambo leo. Hivi kwa rasilimali tulizonazo ndio tumelainika kwa wakoloni namna hii?
Serikal iombe msaada wa vidonge vya kuzuzia mimba
 
Kwan wakirudi shule ww itakuathiri vp ktk uchumi wako au maisha yako kwa ujumla acha madogo wasome tuwe na kizazi kilicho elimika
 
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua kisha akirudi shule akawa anasoma na mabinti ambao hawajawahi kubikiriwa, hatakuwa na ushawishi mbovu kwao ili waonje utamu wa ngono? Tumejustify mapenzi kabla ya kumaliza shule

Fikiria kijana mvuta bangi ambae alikosa malezi na akaacha shule alafu ukrudisha asome kisa tu unalazisha amalize shule. Hii sio justification kuwa kuvuta bangi na utoro sio kosa?

Mkopo wa bil 600 umetufanya tujikabidhi kwa wakoloni mambo leo. Hivi kwa rasilimali tulizonazo ndio tumelainika kwa wakoloni namna hii?
Wewe usijali mikono yako kunja tuu na uvimbe kabisa ila sisi tunajali hatima ya Watoto wetu ,sio watoto wa mabeberu..

Pili mtoto wako akipata ujauzito kwenye Umri mdogo onyesha ushujaa kwa kumpiga marufuku shule hapo ndio utakuwa umemkomoa vizuri beberu.
 
Ujuzi gani wa veta usiohitaji mfumo rasmi?Wanaofeli tu wenyewe kuingia veta bado wanakutana na vigezo chungu nzima sembuse hili la wajawazito.
Wajawazito wapewe upendeleo kwenye hilo!!
Kuliko kuwarudisha darasani wakachangamane na wenzao ni sawa na kubariki ngono mashuleni!!!

Tumepitia huko tunaelewa,wakati mwingine tulijizuia kufanya sio kwa sababu ya kupewa elimu rika hapana tuliogopa mimba kuliko Ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa!

Je tunaporuhusu mimba mashuleni huoni kama unakuwa umeruhusu ngono?

Hawa wanaharakati badala ya kutafuta njia za kuzuia mimba mashuleni wao wanakimbilia kubariki na kuona ni jambo la kawaida,kesho wataanza kupiga kelele kuhusu baba wa mtoto asifungwe ili mtoto asikose malezi ya baba na mama
 
Fikiria jamii ambayo ni halali kuoa binti mwenye miaka 13 lakini inashangaa wa miaka 14 kupata mimba.

Fikiria jamii ambayo inaamini mimba zote ni kutokana na uhuni wa mabinti zao.

Fikiria jamii ambayo inaamini kuwa mimba inaambukizwa.

Fikiria jamii ambayo haitaki kuwapa watoto wake elimu ya miili ( ambayo mabibi na mababu zao walikuwa wakiitoa) halafu wanashangaa wanapopata mimba.

Fikiria jamii yenye tatizo kubwa la mimba za utotoni ( sio wanafunzi peke yao) lakini haitaki kuwapa contraceptives.
Fikiria jamii inayoamini watoto wote wanaofukuzwa shuleni ni wavuta bangi na wanastahili kufukuzwa.

Fikiria jamii inayoona heri kukosa mkopo utaowasaidia kujenga shule kwa ajili ya watoto kuliko binti aliyepata uja uzito kuendelea na masomo.

Baada ya panya hivyo jiulize tena kwa nini nchi hiyo bado ina umasikini wa kutupwa miaka 60 baada ya kupata uhuru kutoka kwa mabeberu.

Amandla...
Shida "alternatives' ,wale wanaosoma shule za serikali wengi ni watoto wa sisi walala hoi,ni wepesi kuiga kujaribu ya kusikia,rahisi kushawishika kwa vizawadi,nakumbuka enzi hizo zangu nikiwa la pili nilianza kusikia nakutaka kujaribu shida ikawa hakuna aliyekuwa haswa namna ya kuula mhogo ,na enzi hizo ilikuwa kosa kubwa kumtamkia neno jinsi tofauti ungeuwawa,na ndiyo maana tulimaliza la Saba bila msichina yoyote kupata mimba,hebu fkiria Leo hii ni vijana wangapi wa kiume wanalawitiana.Je tungewajua mapema wenye tabia hiyo tukawaondoa mapema tungeepusha wangapi na kuharibikiwa huko,sasa nashauri serikali ijenge shule za boording za mzingi na sekondari Moja Moja Kila wilaya/halmashauri ambako itakujwa inawasomeshea wanafunzi walipata mimba kujifungua,itakujwa ni rahisi kuweka wodi ya kuwatunza hao watoto wakati mama zao wako darasani,ni rahisi .mama zao kuwanyonyesha kwa wakati,ni rahisi wao kwa wao kubadilishana mawazo ya kikubwa,na rahisi kupewa nasaa za kujiepusha na ngono za utotoni.TUKUmbuke wenye fedha wanasoma sent Fulani na english medium fulani.hadi huruma
 
Back
Top Bottom