Kurudisha mabinti waliopata mimba shuleni ni kunyoosha mikono juu na kulikabidhi taifa letu kwa wakoloni mambo leo kwa ajili ya mkopo wa bil 600

Bora kujikabidhi kwa mabeberu kuliko kwa wachina, beberu hata uzidiwe vipi na deni lake akamati mali na aachi kukukopesha. Mchina atakamata Bandari, airport, ziwa victoria, mlima kilimanjaro.

Beberu anahofu ya Mungu Mchina amjui Mungu pesa mbele utu nyuma.
Aaaah hapo shida co wachina shida n viongoz wasio n maarifa imagine umeruhus kitu Kam hiko kitokee lkn pia imagine n kwa kias gan tunaenda kulipeleka taifa pabaya maan hapo mwanzo Sheria ilikua n ngum n mimb walikua wanapat bila hofu yeyote je walivokua huru itakuwaj??
 
Mkuu hayo maadili mbali na kufundishwa nyumbani watoto waliendelea kufundishwa swala zima la maadili shuleni, sasa kama kufanya mapenzi hadi kupata ujauzito imekuwa ruksa kwa watoto wa shule ni jambo gani unatarajia hata kama umewapa malezi hao watoto huko nyumbani, au labda utawafungulia shule yao wenyewe.
nani amekwambia kwa kuwarudisha shule waliozaa ni kutoa rukhsa kufanya mapenzi? Kama ni hivyo basi wenye vvu wasipewe ARV maana kwa kufanya hivyo ni kuwaambia waendelee kufanya uzinzi....think!!

Na wanafunzi wenzao wa kiume wanaowatia mimba mbona hamuwafuatilii?
 
Aaaah hapo shida co wachina shida n viongoz wasio n maarifa imagine umeruhus kitu Kam hiko kitokee lkn pia imagine n kwa kias gan tunaenda kulipeleka taifa pabaya maan hapo mwanzo Sheria ilikua n ngum n mimb walikua wanapat bila hofu yeyote je walivokua huru itakuwaj??
Hakuna binti mwenye kutamani kuharibu maisha yake kwa kugawa hovyo bali zipo sababu nje ya hilo.So tusiwanyime haki zao.Hata mbali na sheria still waliomimbwa wazazi waelewa waliwarudisha shule na wakafanya vizuri tu.
 
Duuh,
Nilikuwa naunga mkono kufungwa jela mwanamume aliyempa Mimba mwanafunzi hata kwa miaka mingi Sana!

Ila ulichoandika hapa UMENIAMINISHA kuwa kuzaa mtoto haipaswi kuwa kosa la jinai!

Yaani mtoto amezaliwa, anaenda msikitini au kanisani kumshukuru MUNGU kwa uhai aliopewa, halafu anaambiwa baba yake amefungwa kwa kosa la kumzaa yeye!

Baba aliyempa mwanafunzi Mimba apewe jukumu la kusimamia huduma ya elimu ya msichana aliyempa Mimba pindi akirejea shuleni, na asipoweza afungwe kwa kosa Hilo, na sio la kusababisha ujauzito
True,
 
Fikiria jamii ambayo ni halali kuoa binti mwenye miaka 13 lakini inashangaa wa miaka 14 kupata mimba.

Fikiria jamii ambayo inaamini mimba zote ni kutokana na uhuni wa mabinti zao.

Fikiria jamii ambayo inaamini kuwa mimba inaambukizwa.

Fikiria jamii ambayo haitaki kuwapa watoto wake elimu ya miili ( ambayo mabibi na mababu zao walikuwa wakiitoa) halafu wanashangaa wanapopata mimba.

Fikiria jamii yenye tatizo kubwa la mimba za utotoni ( sio kwa wanafunzi peke yao) lakini haitaki kuwapa contraceptives.
Fikiria jamii inayoamini watoto wote wanaofukuzwa shule ni wavuta bangi na wanastahili kufukuzwa.

Fikiria jamii inayoona heri kukosa mkopo utaowasaidia kujenga shule kwa ajili ya watoto kuliko kuruhusu binti aliyepata uja uzito kuendelea na masomo.

Baada ya kufikiria hivyo jiulize tena kwa nini nchi hiyo bado ina umasikini wa kutupwa miaka 60 baada ya kupata uhuru kutoka kwa mabeberu.

Amandla...
Hatari sn
 
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua kisha akirudi shule akawa anasoma na mabinti ambao hawajawahi kubikiriwa, hatakuwa na ushawishi mbovu kwao ili waonje utamu wa ngono? Tumejustify mapenzi kabla ya kumaliza shule

Fikiria kijana mvuta bangi ambae alikosa malezi na akaacha shule alafu ukamrudisha asome kisa tu unalazisha amalize shule. Hii sio justification kuwa kuvuta bangi na utoro sio kosa?

Mkopo wa bil 600 umetufanya tujikabidhi kwa wakoloni mambo leo. Hivi kwa rasilimali tulizonazo ndio tumelainika kwa wakoloni namna hii?
Punguza kasiriko mzee 😂😂!! Ile awamu ndo ishatoweka mazima 🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom