Kurudisha kodi ya kichwa nyakati hizi za ulimwengu ulioendelea ni aibu kubwa. Mwigulu Nchemba kuwa na aibu. Mbona kuna vyanzo mbadala vingi

VYANZO MBADALA SIYO UFUMBUZI, BALI KILA MTANZANIA MWENYE SHUGHULI YA KIUCHUMI ALIPE KODI YA MAPATO KILA MWEZI

Wigo mdogo wa eneo la kukusanya kodi mtihani mkubwa kwa TRA na pia mzigo mkubwa kwa walipa kodi wachache kutwishwa jukumu la kulipia kodi Tanzania

Habari ya ziada:

13 January 2023
UMOJA WA ULAYA UMESHAURI WAWEKEZAJI NA SEKTA BINAFSI KUWA NA USHIRIKIANO WA WAZI NA TRA

Balozi Manfredo Fanti amezungumza hayo akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya mkutano mfupi na wahariri pamoja na wadau wa habari nchini.



Source : MLIMANI TV UDSM
 
02 February 2023
Ukumbi wa JNICC
Dar es Salaam, Tanzania

MAJADILIANO KATI YA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI, HOJA NZITO ZAFIKISHWA



Washiriki wasema Fedha zimo humuhumu ndani nchini hakuna haja ya kutegemea vyanzo vichache vya ndani au kukopa toka vyanzo vya nje ya nchi anasisitiza sheikh Mohamed Issa.

Edward Issa Maduhu mtafiti wa misitu, mchoma mkaa mkubwa ambaye ni Muuza mkaa nje ya nchi kimataifa aiomba serikali kuwezesha mazingira rafiki ili nao waweze kuchangia mapato na kodi kwani kontena zake zimekwama bandarini kwa vile mchakato wa kibali siyo endelevu. Muuza mkaa huyu ana tenda ya tani 100,800 hivyo ni mtihani mkubwa kutokana na changamoto ya sekta ya mazao ya misitu kutokuwa na sera endelevu isiyo badilika basilica ktk kipindi kifupi.

Riziki Ganga aangazia bandari ya Dar es Salaam kuendekeza kodi ya makadirio badala ya kodi elekezi ambayo ni endelevu kwa sababu wafanyabiashara watakuwa na uhakika ni kodi kiasi gani watatakuwa kukilipa kwa uhakika na kuondoa mianya ya ukadiriaji kila mzigo unapoingia. Bw. Riziki anasema hii itasaidia bandari ya Dar es Salaam kuwa eneo la kukimbilia wafanyabiashara wa kutoka nchi zote jirani na pia Kariakoo ya Dar es Salaam kuwa kitovu cha biashara ukanda wote huu wa Afrika Mashariki na ya Kati .

Nayo BRELA BRELA | Mwanzo waongelea kuhusu kusajiliwa kwa kampuni ...
 
Back
Top Bottom