Kurudisha Kadi - Kwa nini "hurudishwa" kwa chama chengine? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kurudisha Kadi - Kwa nini "hurudishwa" kwa chama chengine?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMMAMIA, Jun 10, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kwa maana rahisi ya neno kurudisha, ni kuwa unarejesha kule ulikochukua; lakini kwa "siasa za Tanzania", mwanachama anapohama chama kimoja tunasema anarudisha kadi kwa chama anachohamia. Mantiki iko wapi?

  Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote na wala sijui "Yaliyomo" ndani ya kadi hizo, lakini kwa uelewa wangu ni kuwa kwenye kitambulisho chochote rasmi (kadi hii in this case). huwa na kipengele kinachosema "Kadio hii ni mali ya chama". Pengine kunaweza kuwa na maneno ya ziada "Ikipotea auukiiokota peleka ripoti au irejeshe kunakohusika".

  Nahisi ingekuwa busara kadi hizo kurejeshwa kwa vyama husika, pamoja na mambo mengine hii itazuwia ule mpango unaodhaniwa wa cham fulani kuchapisha kadi feki au hata kununua kadi za chama chengine ili kujidai tu kuwa wanachama elfu tano wamerudisha kadi. Au angalau kungekuwa na sheria/kanuni inayovitaka vyama vilivyopokea kadi hizo kuzirejesha kwa chama husika ili viweze kuhakiki wanachama wake.
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  you are very right ... you have apoint ..... "chama chengine" - sound like you are from Nachingwea
   
 3. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,064
  Trophy Points: 280
  Point hiyo kaka ila kwa upande wa jicho la pili inaweza kuwa ni sehemu ya kudhibiti wanachama ndumilakuwili yaani kama ulitamka wewe ni chama flani basi wape kadi yako wakupe yao.
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Jana kadi za magwanda ya khaki zilipokusanywa zilitaka kuchomwa moto Kinana wa CCM akawaambia "msizichome" tunataka tuwarudishie hukohuko kwao.
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Umenigundua, kiumbe nilitakiwa kuandika "kingine" badala ya "chengine". Nina matatizo na ngeli za KI-VI linapokuja suala la maneno ya Ch.
   
 6. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hata wewe point yako ni nzuri, lakini angalia maneno ya zomba hapo chini:

  Nionavyo, huu ndio utaratibu ambao ungepaswa kutumika ili kuzuwia "majigambo" na kwa chama kilichokimbiwa kujua kama kweli kadi zilizorudishwa ni zao kweli na pia kufanya uhakiki wa wa wanacham wao.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unaonesha hukuhudhuria wa kutazama kwenye runinga "live" mambo ya jana. Usihjali unaweza ku "google".

  Hayo ndio yaliojiri, wala usiwe na hofu, utatuzoea kwani huu ulikuwa mwanzo, tunapita Kiondoni, Temeke halafu tunashuka Kusini. Nikupe siri?

  Kutakuwa kuna timu tatu "moja kusini, moja kaskazini, moja mikoa ya kati". Kaa chonjo. Mmetuudhi sana kwa uongo wenu, si bora mngekuwa mnasema kweli tu, kuwa jamani, CCM wanajenga kilomita 11,000 za barabara za lami , sisi tutajenga 24,000. Tungewaelewa lakini kwenda kuzuwa kwa wananchi hatuwakubalii na hatuwawachii mpaka mjuwe kusema ukweli.
   
 8. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu naomba tenda ya kubeba watu kupeleka kwenye mikutano yenu. Nina Coaster zangu 3 na moja nyingine ya mshikaji naisimamia na pia kama mtataka Hino ipo ya abiria 65 na ina coridor kubwa pia wengine wanaweza kusimama, 10% ipo. Tuanze na mikutano ya hapa DAR halafu hiyo ya kusini tutaongea
   
 9. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,637
  Likes Received: 2,064
  Trophy Points: 280
  Hata mie nimeukubari utaratibu huu kwani utawezesha vyama ku-update taarifa za wanachama wao ikiwemo na idadi japo CCM na serikali yake wanaamini ubora wa kitu wowote unatoka na takwimu kubwa ya kitu flani na hata wakihama kuwafuta kwenye data base yao inakuwa kazi kweli
   
 10. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Asante sana Mkuu kwa taarifa na ninakupongezeni, lakini mimi ninaingiaje humo kwenye shutuma unazoshusha? Ukiangalia upya kwenye post yangu, kuna maneno haya:
  .
  Kwa siasa za TZ mimi ni mtazamaji tu, angalau mpaka sasa, ili nibaki na uhuru wangu wa kutoa mawazo bila ya ushabiki. Nilichotaka kusema ni kuwa TZ tunaendesha mambo kwa jazba na mazowea. Sina hakika lakini nina wasiwasi kuwa hata huko kwa msajili wa vyama, hakuna orodha ya wanachama wa kila chama, na kama ipo sijui kama wanapelekewa "updates" za wanachama wapya kila baada ya muda.

  My take: Kitengo cha msajili wa vyama vya siasa angekuwa na tovuti ambayo orodha ya majina ya wanachama wa vyama vyote na kuwa "updated" kila baada ya muda. Wanakula jasho letu hawa, sio wasubiri uchaguzi mpaka uchaguzi tu kupokea kesi za pingamizi.
   
 11. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hizo kadi tulizotengeneza huku kariakoo. Lowassa lazima awalize na hivyo visiasa venu uchwara kama alivyosema yule mwamba wa Igunga Rostam Azizi
   
 12. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pepo mchafu hutolewa kanisani na sio kwa mganga ulikompatia.

  Mnaogopa kwa kuwa mnaona aibu jinsi watu wanavyomiminika CDM. Nyie ndio mlianza, sasa inakula kwenu
   
 13. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  ccm ilizaliwa mwaka 1977


  zika rasmi potea 2015
   
 14. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  All said na umeeleweka na tupo wengi tusiotaka utumwa wa vyama......kuna walakini na mfumo huu wa kurejesha na kugawa kadi kama njugu...huyo muhusika aweke database na kila zikirudishwa zipelekwe kwa chama husika na kuwasilishwa kwa msajili na hawa "political prostitutes" wadhibitiwe sio kila mkutano mtu awe na uhru wa kuhama......hata choo siku hizi unalipia bana sembuse kuhangaisha politicla equilibrium????
   
 15. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  I should have said it better. Jana nilikutana na data zinazoshitusha - CDM 26,000 wamerejesha kadi - . This is FOUR MUCH, too much ni kidogo.
   
 16. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kurudishwa kwa chama husika ni wazo zuri kwani itakuwa kazi pia kufoji kadi hizo, sema tu kwa siasa za bongo hiyo ishu ni ngumu sana
   
 17. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  Imagine 26 thou......na hao wenye wanachama wao pia wawe na database ili vikirudishwa hivyo vipande wakae na kucheck validity and viability maana hawa wanasiasa tukiwachekea tu baaas itakuwa hadithi ya mto kutiririsha maji.

  M happy kujua kuna watu wengi bado hawana "political myopic syndrome", let us hold on ili kuwe na watu wa kuandika historia sahihi if need be
   
 18. B

  Bob G JF Bronze Member

  #18
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  CCM hawawezi kuzirejesha zile kadi kwa CDM na CUF coz zile walizitengeneza ccm wenyewe kufurahisha baraza
   
 19. u

  umsolopagaz Member

  #19
  Jun 10, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ......salute mkuu! yours is de sword on dem throat!
   
Loading...