Mimi ni mtoto wa Polisi na wazazi wangu wote walikuwa kwenye jeshi hili kwa miaka mingi sana. Kwa ufupi wazazi wangu hawajawahi kufanya kazi nyingine.
Ukweli kumekuwa na malalamiko mengi sana ya unyanyasaji wa Polisi wa hali ya juu. Hii sio kwa wanasiasa pekee tumesikia haya malalamiko kutoka kwa raia wa kawaida . Zamani tulikuwa hatusikii haya malalamiko ya unyanyasaji.
Hivyo kurudisha heshima ya jeshi hili la raia inabidi iundwe tume ili wale walionyanyaswa waweze kusema na kutoa machungu yao na kuondoa chuki kwa jeshi nzima. Hii itasaidia vitu viwili (1) kuhakikisha Polisi wenyewe wanafuata utaratibu na sheria (2) Itawafanya raia wajue kwamba serikali inajali haki za binadamu. Inashangaza sana wakati hayati Magufuli alivyokuwa anasema wananchi wasionewe ndiyo wakati huohuo Polisi wametesa watu kuliko wakati mwingine wowote.
Vilevile hakuna sababu ya Polisi kutumia machine gun kulinda hata kwenye traffic wakati mwingine wakati siku hizi kuna bastola ambazo sio mzigo na zinaweza kuchukuwa risasi za kutoka na bei sio ya juu sana. Polisi wa raia wanatakiwa kuheshimiwa na sio kuogopwa na wananchi wasio na haki.
Serikali ifikirie kuunda tume ya watu kusema machungu yao hasa wale walio teshwa bila sababu