Kurudisha Heshima, Mchague Sitta kuwa Waziri Mkuu

Kuna watu wanaogopwa na mafisadi, na wanaweka shinikizo wasipate nafasi nyeti. lakini wanamuharibia raisi wetu.

Mfano:
1. Six
2. Pombe M
3. Mwakembe
4. Mwamri

Nafikiri hivi vyote ni vichwa vizuri na vina msimamo, at least 50% ya Sokoine. Lakini wanaogopwa hao!!!!

Katika wanaccm waliobaki, ni heri akamchukua Pombe Magufuri kama waziri mkuu, maana angalau ni mtendaji na si mtu wa kulialia kwa kulaumu ambayo yako chini ya uwezo wake; ukiwa na Rais wa maneno tu unahitaji waziri mkuu wa vitendo. Ni tofauti na sasa wote ni wa kulalamika tu!!
 
Mkuu PM.

Sheria inasema waziri mkuu lazima atokane na wabunge wa kuchaguliwa [wabunge wa majimbo] F Sumaye,Salim A Salim na C Msuya si wabunge Rais anaweza kuwateua kupitia zile nafasi zake kumi lakini sheria inamzuia kuwapatia wadhifa wa waziri mkuu.

Kuchagua waziri mkuu wa ku serve miaka miwili it's a waste of resources ....na kodi zetu kuendelea kuwalipia mafao...Kama hataki Pinda ..basi afanye recycling kwenye mawaziri wakuu waliopita..Kati ya Frederick sumaye,Salim Ahmed Salim ...,cleopa David msuya etc..Hawa at least wana nguvu ya kumalizia miaka miwili iliyobakia....mzee malecela naona umri na mwili vinachoka though bado Ana akili safi.....
 
Kama naye si mwizi inakuwaje wanae wote wasome Marekani na ana nyumba ndogo lukuki.
Aliiba sana alipokuwa waziri wa mawasiliano, enzi za Mwalimu alinunua nyumba pale Alykhan Upanga kwa ajili ya nyumba ndogo mama Masoud. Alipata wapi pesa hizo?

Hakuna aliyewahi kuwa waziri ni msafi nchi hii, tofauti ni ile ukubwa ama kiwango cha WIZI
 
Msikariri. hao wote mliowataja wanatakiwa wastaafu na wapishe. so many competent people wapo. waondoke, wapo toka enzi za Mwalim, hv mnafikiri sisi vijana tutaongoza lini?
 
Mimi naweza kuwa waziri mkuu mzuri sana. Sina makundi wa kujuana, ni bakora kwa kwenda mbele na kuwapeleka gerezani mawaziri na makatibu wakuu wezi na wazembe. Kama si mimi Mtikila anaweza kufaa pia kwenye nafasi hiyo.
 
Sitta hana uwezo, kashindwa na kimama kile bungeni ataweza uwaziri mkuu?
 
Kuchagua waziri mkuu wa ku serve miaka miwili it's a waste of resources ....na kodi zetu kuendelea kuwalipia mafao...Kama hataki Pinda ..basi afanye recycling kwenye mawaziri wakuu waliopita..Kati ya Frederick sumaye,Salim Ahmed Salim ...,cleopa David msuya etc..Hawa at least wana nguvu ya kumalizia miaka miwili iliyobakia....mzee malecela naona umri na mwili vinachoka though bado Ana akili safi.....

..Hao uliwataja sio Wabunge wa Kuchaguliwa kwa sasa, na ukumbuke kuwa hicho ndicho kigezo kikuu cha mtu kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu....

...By the way, ata Sitta pia ataendelea kupokea posho yetu maisha yake yote kama Spika Mstaafu, hivyo kwa kigezo cha kuepuka hiyo pension, ambao hawatatuongeza hiyo burden ni Lowassa na Sitta, na kwa kuwa Lowassa tayari alishapewa hiyo nafasi na kuchemka chini ya Rais huyuhuyu, then option pekee inabaki kuwa Sitta...
 
Kwa status ya ccm na bunge lake,Mie naona jk amteue Lusinde kuwa PM ili mambo yawe shwari sirikalini,maana ataendana na Makinda.
 
Kuchagua waziri mkuu wa ku serve miaka miwili it's a waste of resources ....na kodi zetu kuendelea kuwalipia mafao...Kama hataki Pinda ..basi afanye recycling kwenye mawaziri wakuu waliopita..Kati ya Frederick sumaye,Salim Ahmed Salim ...,cleopa David msuya etc..Hawa at least wana nguvu ya kumalizia miaka miwili iliyobakia....mzee malecela naona umri na mwili vinachoka though bado Ana akili safi.....
nathani hufahamu katiba mzee Waziri Mkuu lazma atokane na Wabunge na uliowataja hamna hata mmoja anayekidhi hicho kigezo maana si Wabunge tena...!
 
Tatizo ni Rais mwenyewe hata amchague nani hataisaidia nchi hii, kazi imemshinda ameamua liwalo na liwe. Bado tuna miaka mitatu ya mateso mengi nadhani kama jamaa ataendelea kuiongoza nchi hii mfumuko wa bei utakuwa 50% kwani alikuta ukiwa 7% amatufikisha 19% anachanja mbuga kuelekea mdororo mkuu wa uchumi kuwahi tokea TZ. Ajichunguze na atoke hapo kama kweli ana nia njema na nchi hii,
 
Hakika ili chama cha mapinduzi kilete mvuto kwa watu ni muhimu Mr Standard and speed au Sita akawa waziri mkuu.
Sifa kubwa aliyonayo ni kuwa anakubalika sana na wabunge hasa wa upinzani.
Spika atakuwa amepunguziwa sana mzigo wa maswali ambayo mara nyingi yanakosa majibu.
Serikali itakuwa imekubalika na bunge, upinzani, mahakama na wanainchi kwa ujumla.
Ila akiteuliwa asiingize ndoto za kuutaka uraisi mwaka 2015 kwani hii itamchafulia sana hasa kwa vyama vya upinzani na kwa wanainchi kwa ujumla. Achape kazi tu na asiongelee kuhusu raisi ajaye
 
Sita nae ni msaliti alikuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi akatusaliti kusaini hoja ya zito hana lolote huyo....
 
sioni kwanini pinda asiendelee kuwa waziri mkuu,sio fisadi na ni mchapa kazi.
tatizo ni hao mawaziri and i can see pinda through 2015 as PM unless otherwise amuombe mh rais asimteue tena kwenye wadhifa huo iwapo kweli atavunja baraza lote la mawaziri.
 
Kaka fikiri mara mbili Pinda ni bingwa wa kulalamika tu hana lolote huyo hujagundua tu? Mbona Magufuli huwa halalamiki kama anavyofanya PM? na ndiyo waziri tu wa ujenzi je, akiwa PM waziri gani ataleta madudu? yeye yuko tayari kujiuzulu ikiwa atatofautiana na Boss wake lakini siyo huyo mtalaam wa radi wako ambaye hivi karibuni tutamtunukia PhD kulalamika.
 
Back
Top Bottom