Kurudi tena shambani mwaka 2012 katika kilimo cha mahindi

Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,375
3,654
Helo JF katika sekta ya kilimo mwaka huu wakulima wengi hawakupata mazao jambo ambalo linawakatisha tamaa wengi wao.n Nililima ekari tano mwaka huu na matarajio yangu katika kila ekari itoe angalau gunia 20x5=gunia 100 na kila gunia ningeuza kwa bei iliyokuwepo sokoni kwa wakati huo!

Lakini nikashangaa naambulia gunia 3, Je Na wenzangu ambao ni wakulima ekari moja hutoa gunia ngapi? Naombeni mnijuze labda kuna sehemu nilikosea katika kilimo hiki cha mahindi! Na nifanyeje ili nipate mazao mengi?

Ngoja malila aje kwa ushauri.

Haya Husninyo,
Mwaka huu ulikuwa balaa sio mchezo,hata Elnino nadhani yamemkuta makubwa kuliko yako. Kwa wastani ukilima vizuri na mbegu nzuri ktk altitude sahihi, basi eka moja hutoa si chini ya gunia 20/30 hivi. Tatizo kubwa la wakulima wengi ni kulima kwa historia ya eneo husika la miaka hiyo ya nyuma bila kuangalia mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa. Kwa mfano Ismani Iringa,zamani bila mbolea unavuna kama huna akili nzuri,baadae ikaja matumizi ya mbolea, ghafla mvua zimekata milele, na sasa kuna njaa huko ya kufa mtu.

Huko huko Iringa, wilaya ya Kilolo, kijiji cha Mawambala, kuna Wazungu wamelima mahindi hadi wanashindwa kuvuna,hivi tunavyo jadiliana hapa,wao wanalalamikia manpower kuwa ni haba. Kule mvua za Mungu zinanyesha hadi basi. Acha Mby/Rukwa/Songea.

Ninachotaka kusema, kilimo cha kutegemea mvua kwa baadhi ya maeneo hakifai. Kuna maeneo ya Mfindi,ambayo mvua inanyesha sana na yana rutuba ya asili,no mbolea, lakini serikali imewapa wazungu wanapanda miti ya mbao/boriti ambako akina sie tulipaswa tulime kwa gharama nafuu.

Jibu swali hili, je shamba lako ni jipya au used? mbegu uliyotumia ni compartible na location yako? Je ulifuata msimu halisi?

Malila ushauri uliompa mkuu hapo umetusaidia wengi,naomba unisaidie na mimi kuhusu kilimo cha maharage on average hecta moja inaweza zalisha kiasi gani kama taratibu zote zikifuatwa mimi nataka kulima mwaka huu kwenye mkoa mmojawapo huku nyanda za juu kusini.

Nakuunganisha na mtalaamu wangu wa pale Uyole kwa simu,ili akupe uwezo wa kila mbegu ya maharage kwa eka moja, mbegu iko wapi na kwa hali ya hewa ipi nk nk. Piga 0765504765

Asante sana mkuu.

Haya Husninyo,

Mwaka huu ulikuwa balaa sio mchezo,hata Elnino nadhani yamemkuta makubwa kuliko yako. Kwa wastani ukilima vizuri na mbegu nzuri ktk altitude sahihi, basi eka moja hutoa si chini ya gunia 20/30 hivi. Tatizo kubwa la wakulima wengi ni kulima kwa historia ya eneo husika la miaka hiyo ya nyuma bila kuangalia mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa. Kwa mfano Ismani Iringa,zamani bila mbolea unavuna kama huna akili nzuri,baadae ikaja matumizi ya mbolea, ghafla mvua zimekata milele, na sasa kuna njaa huko ya kufa mtu.

Huko huko Iringa, wilaya ya Kilolo, kijiji cha Mawambala, kuna Wazungu wamelima mahindi hadi wanashindwa kuvuna,hivi tunavyo jadiliana hapa,wao wanalalamikia manpower kuwa ni haba. Kule mvua za Mungu zinanyesha hadi basi. Acha Mby/Rukwa/Songea.

Ninachotaka kusema, kilimo cha kutegemea mvua kwa baadhi ya maeneo hakifai. Kuna maeneo ya Mfindi,ambayo mvua inanyesha sana na yana rutuba ya asili,no mbolea, lakini serikali imewapa wazungu wanapanda miti ya mbao/boriti ambako akina sie tulipaswa tulime kwa gharama nafuu.

Jibu swali hili, je shamba lako ni jipya au used? mbegu uliyotumia ni compartible na location yako? Je ulifuata msimu halisi?

ubarikiwe sana.

Haya Husninyo,
Mwaka huu ulikuwa balaa sio mchezo,hata Elnino nadhani yamemkuta makubwa kuliko yako. Kwa wastani ukilima vizuri na mbegu nzuri ktk altitude sahihi, basi eka moja hutoa si chini ya gunia 20/30 hivi. Tatizo kubwa la wakulima wengi ni kulima kwa historia ya eneo husika la miaka hiyo ya nyuma bila kuangalia mabadiliko ya tabia nchi kwa sasa. Kwa mfano Ismani Iringa,zamani bila mbolea unavuna kama huna akili nzuri,baadae ikaja matumizi ya mbolea, ghafla mvua zimekata milele, na sasa kuna njaa huko ya kufa mtu.

Huko huko Iringa, wilaya ya Kilolo, kijiji cha Mawambala, kuna Wazungu wamelima mahindi hadi wanashindwa kuvuna,hivi tunavyo jadiliana hapa,wao wanalalamikia manpower kuwa ni haba. Kule mvua za Mungu zinanyesha hadi basi. Acha Mby/Rukwa/Songea.

Ninachotaka kusema, kilimo cha kutegemea mvua kwa baadhi ya maeneo hakifai. Kuna maeneo ya Mfindi,ambayo mvua inanyesha sana na yana rutuba ya asili,no mbolea, lakini serikali imewapa wazungu wansd

Nakuunganisha na mtalaamu wangu wa pale Uyole kwa simu,ili akupe uwezo wa kila mbegu ya maharage kwa eka moja, mbegu iko wapi na kwa hali ya hewa ipi nk nk. Piga 0765504765

Big respect kwako mkuu malila kwa msaada unaotupatia na ushauri,weka na namba yako basi kama inawezekana

Mimi nililima hekari 100 dodoma nikaambulia gunia 150 tu ila atleast nimegundua baadhi ya makosa yangu,nilitaka kulima kwa remote control Palizi haikuwa nzuri

Mkuu hapo kwenye red umeniacha hoi kabisa, nilijaribu kufanya huo mchezo kilichonikuta najua mwenyewe....

Yaani hapo kwenye red nipakubadhiti maana mi nilishawahi kugawana mavuno sawa na msimamidhi wangu.Safari rekebisha palizi na usimamizi mzur utaona matokeo

Mkuu we acha tu ilikuwa mara yangu ya kwanza kulima nimegain bonge la experience asikudanganye mtu ukitaka kulima kwa mafanikia lazima usonge front mwenyewe hata kama huwezi kuhamia shamba walau kila hatua iwe kulima,kupalilia au kuvuna lazima uifuatilie kwa ukaribu shambani sio kukaa ofisini tu kwenye kiyoyozi unapiga simu itakula kwako tu,huu ni ushauri kwa staters wenzangu wote

Yaani hapo kwenye red nipakubadhiti maana mi nilishawahi kugawana mavuno sawa na msimamidhi wangu.Safari rekebisha palizi na usimamizi mzur utaona matokeo

Mkuu ntarekebisha hayo mambo msimu ujao,mbona ukigawana nao usawa ushukuru mungu la sivyo watakuachia mazao ya ushahidi tu kuwa na wewe uliwahi kulima.
Mkuu hiyo user name yako nimeikubali sana naota sana kumiliki hiyo kitu,ni ya ukweli kishenzi Ferguson hatii mguu hapo labda FIAT

Jamani wana ukumbi, ninawashukuru sana kwa mawazo yenu wote, shida yangu kubwa ningependa kujui EKA moja ya maharage ya kisasa ambayo yapo "Compatible" na sehemu ninayotaka kulima, k.m. Nyanda za kasikazin Kilimanjaro, Arusha, Morogoro Tanga, na Dodoma; na uangalizi ukiwa wa karibu "Nikiwa front" mwenyewe hasa wakati wa kulima, kupalilia na kuvuna, naweza pata gunia kiasi gani kwa EKA?

Pia ninapenda kulima vintunguu sehemu za IRINGA, na ninategemea kuwa front pia, garama za uandaaji nimezipata lakini sijui kama nitunza vizuri, nitegemee kiasi gani kwa EKA? NB: Katika kilimo chote hiki nitategemea kumwagilia "Irigation" na siyo mvu ya mwenyezi mungu, kwa manano mengine nitkuwa naweza kupanga na kuyamiliki maji.

Tatu, naombeni mawazo ya kujenga "Bwawa" ili niweze kuvuna maji ya mvu na kuweza kuyatumia baadaye wakati mvua zimeadimika, naombeni ushauri wenu wana-forum wenye mawazo katika nyanya hizi.

Wana-forum, nimefanikiwa kununua trector MF 565, ipo kwenye hali nzuri, ningependa niwekeze kwenye mashamba ya kukodi, na kwa vile ninazo accessories za kutosha kwa kuanzia kama, Boom Sprayer, Planter, Disc Harrow, Sub soiler, weed Cultivator na Water Pumps za nguvu, ningependa niwekeze kwenye kilimo cha mahindi, maharage, vitunguu, Karanga na ufuta. Shida kubwa niliyo nayo ni jinsi ya kupata mashamba ya kukodisha of course used, sio ya kuvunja, japo hata kama nikipata ya kuvunja kwa garama nafuu kwenye Potential areas zenye mvua za kutosha na mito ya kutosha kama vle Morogro ili niweze kuvuna maji ningefurahi sana, tatizo kubwa sijui wapi nitapata haya mashamba hata kam nikuanzia eka (70m) au Hecta (100m), 20 - 500 ekas / hectas, nitajitahidi niweze kutumia vifaa vya kilimo nilivyo navyo, na kama mnavyoona ninajitahidi sana kuondokana na kutegemea human lobour kwani kwa maisha ya leo Human labour imekuwa ya ghali sana. Jamani naombeni mawazo yenu. Natanguliza shukrani zangu za awali.

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom