Kurudi kwa JF: Je, nini hatma ya umaarufu wake?

Mbalamwezi

JF-Expert Member
Sep 30, 2007
800
171
Wana JF;

hapana shaka kuwa kurejea tena kwa JF kutawasisimua sana hata wale ambao hawakuwa wakifuatilia ukumbi huu wa majadiliano. Je, mnadhani baada ya zogo lile kupita, JF itapata umaarufu zaidi au kukamatwa kwa vijana wawili wale kutaipunguzia heshima mbele ya jamii?

Mimi nadhani kashkash zilizotokea zinaifanya JF kuzidi kung'ara. Nategemea maelfu ya wanachama wapya kujiunga na forum hii miezi ya hivi karibuni, na hii italeta wigo mpana zaidi wa sehemu ya mijadala kwa kutumia teknolojia ya kiasasa zaidi ya mawasiliano.
 
Mbalamwezi you are very right kwa kweli wametupatia umaarufu mimi nilikuwa siijui JF na sasa nimejiunga rasmi. Nina mengi ya kushare na waTanzania wenzangu wenye uchu wa kuona nchi yetu inakuwa ya neema. Tunakemea wote wanaojaribu kudidimiza jitihada za JF za kuwaelemisha na kuwapa mwanga wananchi kinachoendela kwenye nchi yao inayozidi kudidimia siku hadi siku. Mungu ibariki Tanzania.
 
karibu sana Mtande_Halisi, ukumbi ni wako utande na nyeti zenye halisia.
 
Mbalamwezi you are very right kwa kweli wametupatia umaarufu mimi nilikuwa siijui JF na sasa nimejiunga rasmi. Nina mengi ya kushare na waTanzania wenzangu wenye uchu wa kuona nchi yetu inakuwa ya neema. Tunakemea wote wanaojaribu kudidimiza jitihada za JF za kuwaelemisha na kuwapa mwanga wananchi kinachoendela kwenye nchi yao inayozidi kudidimia siku hadi siku. Mungu ibariki Tanzania.

Karibu Mtade_Halisi,
Waambie na wengine wajiunge, si dhambi kujiunga JF.
JF ni uhuru wa maoni tu!
Umaarufu wa JF utaongezeka sana, nahisi watawala wataamua na wao kujiunga JF ila waweze kutoa maoni yao pia.
 
jamani HODIIIIIIIIII,wenye nyumba hii ya JF naomba kuingia ndani.

binafsi yangu nilikuwa sijui lolote khusu JF lakini baada ya kusoma magazeti na kusikiliza habari nyumbani nimekuwa na hamu kubwa kujiunga.

naomba mnikaribishe wenye NYUMBA HII.
 
Nitumie nafasi hii kwa mara nyingine tena kuwapongeza wapiganaji wetu popote pale walipo.Kwa kweli tumeonesha moyo wauzalendo kwa juhudi na nimejifunza kwamba wapo watu kweli walikuwa tayari kupigania nchi na uhuru wao.Watu hawakusita kuwa-face polisi huku wakiongozwa na mkuu mwanakijiji,naamini wengine pia walifanya juhudi binafsi,wengine waliogopa na kujificha hasa niliposikika polisi wanafatilia.Lakini la msingi kufahamu hapa ni kwamba kama unaamini unachofanya ni halali huna haja ya kuwaogopa polisi,haki yako ipo pale hata kama itacheleweshwa.Vijana wana jf wenzetu mliyepata mkasa ule poleni sana,maisha ni mapambano,nadhani jf admin,hao jamaa wapewe tuzo maalumu,manaake ni zaidi ya senior expert members.Labda tuwaite senior jf heros,kwa kweli sioni.
Lakini pia hii si mara ya mwisho kwa mafisadi kujaribu kuzima mtandao huu,watajaribu tena na tena,la msingi ni kujiandaa wakati wote na mapambano,kuwa na back up kadhaa, na ikiwezekana data ziwe kwenye zaidi ya server moja,kwa ufupi wataalamu wa fani hii mnaijua sana sina haja ya kuwaeleza.Jukwaa ni jukwaa,sote tunafurahi sana,tulikuwa 4000 sasa tutafika 15,000 na ninachosisitiza watu tuje na hoja humu,sio uzushi hata kama habari ni za mtu binafsi maadamu zina hoja za kuweza kujustify majadiliano yetu hiyo ndiyo itakuwa sialaha yetu daima.
Hata hivyo,kama wanasheria walivyo, enyi wanachama wapya na wenzangu wa zamani naomba kuwaaseni kwamba ndani ya jf lazima "kukubali kutokubaliana" hiyo ndiyo dira ya majadiliano "we must agee to disagree where possible".Hapa tutaondoa jazba na mengineyo.
Hongera jambo forum kurudi hewani.Mungu ibariki jf,mungu ibariki our beloved land Tanzania.
 
jamani HODIIIIIIIIII,wenye nyumba hii ya JF naomba kuingia ndani.

binafsi yangu nilikuwa sijui lolote khusu JF lakini baada ya kusoma magazeti na kusikiliza habari nyumbani nimekuwa na hamu kubwa kujiunga.

naomba mnikaribishe wenye NYUMBA HII.

karibbu karibu tena nyumba hii nymba kunga ina wengi na ina mengi tumo wahandisi waandishi wanasheriA walokole mujahidina waponzani na wanaopinzaniwa ila wagaidi sina uhakika nao kama wamo lkn nilisikia kuwa ukiitwa eti mtandao wa kigaidi.


hapa ni pahala petu pa kukata issssssue kubadlishana mawazo na kujiliwaza.

ukiwa umenuna ww njoo tu hapa namini utafurahi.

pia tuko mbele kulisaidia taifa letu kujua wabaya wa taifa letu.

nnategemea umoja wetu ndio unaoifanya jambo kuwa chombo imara.

kila ajae kwa shari
waijua yake siri
ivunje yake dhamiri
asiweze kusimama


kila ajae kwa heri
mzidishie sururi
atupe yalo mazuri
kuuendeleza ummma

tuwachape mafisadi
pamoja na makuwadi
zimalize zao kedi
tuwaache wakihema

jf moto mkali
unaangaza wa mbali
waunguza mafedhuli
wanaopenda naqama

mwisho hapa nnafika
jf burudika
hakuana litokufika
kwa damu tutakulinda
 
Jamani ninapata slam toka sehemu mbali mbali duniani za kuipongeza JF kwa kurudi na moja wapio ni sista Natasha fro Stockholm ambeye ni self confessed JF addict na anasema kuwa Mafisadi wakitoee

smq350.jpg
 
Jamani ninapata slam toka sehemu mbali mbali duniani za kuipongeza JF kwa kurudi na moja wapio ni sista Natasha fro Stockholm ambeye ni self confessed JF addict na anasema kuwa Mafisadi wakitoee

smq350.jpg

Mmmh shughuli......
 
Napwapongeza wote waliochangia kwa namna moja au nyingine kuirudisha JF hewani

Umekuwa muda wa majonzi na kusubiri kwa wengi wetu kutokana na kutokupatikana kwa JF

Lakini sasa mambo ni mbele kwa mbele na kwa kweli mi naona kwa tukio hili, JF imekuwa juu zaidi na itakuwa imeongezeka umaarufu

Kazi iendelee
 
Wana JF;

hapana shaka kuwa kurejea tena kwa JF kutawasisimua sana hata wale ambao hawakuwa wakifuatilia ukumbi huu wa majadiliano. Je, mnadhani baada ya zogo lile kupita, JF itapata umaarufu zaidi au kukamatwa kwa vijana wawili wale kutaipunguzia heshima mbele ya jamii?

Mimi nadhani kashkash zilizotokea zinaifanya JF kuzidi kung'ara. Nategemea maelfu ya wanachama wapya kujiunga na forum hii miezi ya hivi karibuni, na hii italeta wigo mpana zaidi wa sehemu ya mijadala kwa kutumia teknolojia ya kiasasa zaidi ya mawasiliano.

Ukweli ni kwamba mimi naamini JF ilikuwa maarufu kabla ya hii kasheshe iliyoibuliwa na polisi. Kupata wanachama wapya kati ya 80 mpaka 100 kwa wiki si kitu kidogo, hata CCM haipati hata robo ya wanachama wanaojiunga JF kwa wiki. Na JF itaendelea kupata umaarufu mkubwa kwa sababu tunayojadili hapa yanawagusa Watanzania walio wengi kwa namna moja au nyingine.

Kuhusu matusi, sijui kuwaita 'mafisadi' wahusika waliosaini mikataba feki ya madini na wao kuwa shareholders wa Barrick wakati Tanzania haikuambua kitu, ni matusi. Sijui kama kuwaita mafisadi waliohusika na wizi mkubwa BoT wa bilioni 500 wakati mahospitali yetu yakiwa hayana madawa, shule zetu hazina madawati na walimu, usafiri wetu ni wa kubabaisha, Watanzania walio wengi hawana kazi, ni tusi.

Matusi wengi tunayajua na kusema kweli mimi sijawahi kusoma tusi alilotukanwa kiongozi yeyote yule. Kumwita mwizi, jambazi, fisadi kwa jina ambalo anastahili kuitwa kwa yale anayoyafanya au aliyoyafanya kwangu mimi si matusi hata kidogo.

Tusubiri moderators watakuja na sheria gani mpya katika uchangiaji katika ukumbi huu. I hope hawatapunguza uhuru wa wanachama katika kuchangia bila kuogopa kusema ukweli wa mambo kama vile fisadi kumwita fisadi. Maana kama uhuru wa kuchangia katika ukumbi huu utapunguzwa kwa namna moja au nyingine basi umaarufu wake unaweza kupungua.

Matusi ya nguoni siku zote tusiyakubali. Wale ambao wanadhani kuna haja ya kuingia msituni na kuanza kuuana nao wasipewe nafasi kabisa katika ukumbi huu, lakini uhuru wa kuandika mengine naomba usipunguzwe hata kidogo.
 
Natumai JF itazidi kupasua anga na nawakaribisha wale wote ambao wamejoin recently.
To me naona ni haki ya kila mtanzania kupata the right information at the right time ili aweze jua nini kinachoendelea ndani na nje ya Taifa la Tanzania.
Mungu ibariki JF,idumu milele
 
JF idumu milele yote amina.

pasipo shaka umaarufu wa JF utaongezeka saaaana, kwani sasa watu wengi hata wale ambao walikuwa hawaijui forum hii wameanza kufuatilia kwa karibu sana.

Ni vizuri serikali ikafahamu kuwa watu wakikosa sehemu ya kusemea yale wanayoamini kuwa ni muhimu kwa basi watatafuta njia mbadala. Na kwa hili JF inakidhi haja.

Ndiyo maana hata wakati wa kamati teule ya Bunge ya Mwakyembe tumeelezwa kuwa watu wengi waliogopa kusema ukweli mbele ya kamati. Hata baadhi ya watu wanaandika articles nyingi magazetini lakini wahariri wengi hufungwa na interest za wamiliki kwa hiyo hata huko articles nyingi haziwezi kutoka, ukiachia magazeti machache ambao walishaamua kuwa na lolote liwalo lakini kuandika wanaendelea. Kumbuka hata majina ya mafisadi yaliyotajwa na dk Slaa pale Mwembe Yanga magazeti mengi haya kuandika ila sehemu mbili tu watu waliweza kupata yale majina, nazo ni hapa JF na gazetu ndogo lakini lenye mdomo mpana...I mean Mwanahalisi.

Tuendelee mbele daima na JF idumu milele.

Nsololi
 
Mkuu Brazameni,

samahani, lakini hiyo picha inaharibu sana mpangilio wa fikra zangu...kila ninapotaka kujadili jambo hapa...
 
Hodi jamani wakuu

Da! Nilikuwa siijui JF, Nimegundua ni Mtandao Makini na
nimeamua kujiunga na Wapiganaji wote
 
karibbu karibu tena nyumba hii nymba kunga ina wengi na ina mengi tumo wahandisi waandishi wanasheriA walokole mujahidina waponzani na wanaopinzaniwa ila wagaidi sina uhakika nao kama wamo lkn nilisikia kuwa ukiitwa eti mtandao wa kigaidi..............

..Bila kuwasahau wasanii, Wakulima, madaktari na machinga...

tuendelee kukata issue
 
Back
Top Bottom