Kurenew leseni ya udereva, TRA kutukata miaka ambayo leseni ilikua imeisha muda wake pasipokuwa na uhakika kama imetumika nchini au la!!

Mr Miller

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
11,445
25,727
Habari wanaJamii.

Kuna hili swala la TRA kuhesabu(kukata) na miaka ambayo leseni ilikua imeisha muda wake pindi unapoenda kuRenew.

Mfano; leseni yangu imeisha muda wake mwaka 2016, nikaja kuRenew mwaka 2019, unashangaa unaambiwa muda wake umeisha tayari inabidi ulipie tena upate miaka 3 mingine..(hiki ni kipindi kile cha miaka 3 ya leseni kuwa legal) kwahiyo kama ningelipia mwaka ule ule 2016 ingedumu hadi 2019.

Nashindwa kuelewa kwanini inakua hivi maana kuna wengine wanaweza kusafiri nje ya nchi kikazi au kimasomo kwa miaka kadhaa, wakirudi inawabidi walipie miaka yote hata kama hawakuitumia!!!

Sijajua ni sheria au ni utaratibu tu uliwekwa....nimekua najiuliza sana hili swala, kama kuna mwenye uelewa zaidi naomba anisaidie kunielewesha hili swala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda gani unatakiwa ku renew baada ya kuisha?
Kuanzia miezi 6 kabla haijaisha unaruhusiwa ku renewal sema tu mifumo yetu wanaoiendesha hawako makini, haiwezekani leseni iishe hafu ikae miaka 3 ndo mtu anaenda kutaka kuhuisha bila sababu za msingi napo anakubaliwa, maana anaweza kuwa ameshasahau hata kuendesha na alama za barabarani kazisahau alitakiwa akajaribiwe kwanza
 
Ni muda gani unaruhusiwa kukaa bila ku renew na usijaribiwe tena?
 
Ulitakiwa uambiwe omba upya, miaka 3 leseni imeisha muda wake maana yake hata muda wa kuhuisha ulikuwa umeshapita. Kijana acha kulalamika ungeshukuru kuwa hawajaitoa kwenye database yao
kuomba upya ni pamoja na kuanza tena mafunzo ya udereva sio!?
nimeona hicho kipengele kwenye tovuti yao...inamaana kila muda wake unapoisha natakiwa kuanza upya application za leseni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuanzia miezi 6 kabla haijaisha unaruhusiwa ku renewal sema tu mifumo yetu wanaoiendesha hawako makini, haiwezekani leseni iishe hafu ikae miaka 3 ndo mtu anaenda kutaka kuhuisha bila sababu za msingi napo anakubaliwa, maana anaweza kuwa ameshasahau hata kuendesha na alama za barabarani kazisahau alitakiwa akajaribiwe kwanza
okay, kwahiyo miezi 6 kabla tunatakiwa kuanza mchakato wa kulipia ili kuRenew, kisheria pia imekaaje baada ya hiyo miezi 6....tunaruhusiwa kuja kulipia?

lkn kama itafungwa, miaka 3 baadae nikaja kulipia kwa kuanza mchakato wa mwanzo sawa, as long as sitakatwa hiyo miaka 3 niliyokaa bila kutumia leseni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ulipaswa kulipa faini
Vitu vingine ni kujiongeza tu tuache kulalama na vitu visivo vya msingi
Ulichukua linsence 2015 ukaenda nje ya nchi umeludi 2019 maana yake mda waleseni yako ulishaisha na ukaongeza na mwaka mmoja tena
Hilo nikosa kisheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Too illogical & unreasonable. Kwanini haukuandika na kuwasilisha barua katika mamlaka husika ukielezea kuwa leseni yako kuanzia muda fulani isingetumika kwa sababu unaenda masomoni nje ya nchi?
sio wote tunauelewa huo kuhusu kutoa taarifa kama leseni yangu haitatumika kwa muda fulani,
na sikumbuki kama kuna kipengele kinachoeleza kufanya hivyo wakati wa mchakato wa kutengeneza leseni ya udereva kwa mara ya kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
leseni inapo expire,hata ukae miaka 10 bila ku-renew bado siku utakayo kwenda ku-renew utapewa nyingine hayo mengine sasa yatakayojitokeza ni kutegemeana na utakayemkuta siku hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
yes utapata nyingine, lkn watakata miaka 10 yote hata kama haukutumia leseni yako...

unavyosema inategemeana na mtu utakayemkuta siku hiyo unamaanisha ni wafanyakazi tu ndio wanaopanga kukata hiyo miaka na sio system yenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
leseni inapo expire,hata ukae miaka 10 bila ku-renew bado siku utakayo kwenda ku-renew utapewa nyingine hayo mengine sasa yatakayojitokeza ni kutegemeana na utakayemkuta siku hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kupotosha watu kwa leseni ya udereva, toka imalize muda wake(miaka) 3,unatakiwa ku i renew si zaidi ya miaka 2,zaidi ya hapo inafutwa, na utatakiwa kurudu chuoni ukasome tena. Ndio utaratibu uliopo
 
Back
Top Bottom