Kurejeshwa kwenye Cabinet kwa mawaziri Simbachawene na Mwigulu - tatizo ni bulb au holder?

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
12,386
2,000
Kama tunavyokumbuka, wakati mawaziri hawa wakiondolewa walikuwa branded kama "wazembe" na walikuwa almost criminalized na mamlaka ya uteuzi.

Mamlaka ya uteuzi imefanya u-turn na kuwarejesha kwenye cabinet with pomp.

Maswali ni mengi kwa kweli. Sina uhakika kama majibu yapo ya kutosha.

Jee, walipoondolewa walikuwa wametolewa kama mbuzi wa kafara tu kuficha udhaifu wa watu wengine kwa wakati ule au tuhuma zile zilikuwa ni za kweli? Kama tuhuma zilikuwa ni za kweli, inakuwaje wamerejeshwa kwenye baraza kabla ya tuhuma dhidi yao hazijawa cleared? Soma Rais Magufuli aeleza sababu 13 za kumfukuza kazi Mwigulu Nchemba - JamiiForums

Sasa wananchi tujue kipi kuhusu kiini cha tatizo....ni mamlaka ya uteuzi au wateuliwa wenyewe?

Jee, tatizo ni bulb au holder kama huyu mdau wa Twitter alivyouliza?
 

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
8,096
2,000
Duh kwa mwigulu kachemka. Labda kwa vile alimtetea ile juzi kwa kujificha chato kipindi hiki cha corona
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,342
2,000
Magufuli alitaja sababu 13 za kumng'oa Mwigulu ( uzi upo jf ) lakini leo kabwia matapishi yake !
Yaani ukitaka kujua namna Jiwe "anavyochemka" katika teuzi zake ni huu wa Mwigulu!
Duh kwa mwigulu kachemka. Labda kwa vile alimtetea ile juzi kwa kujificha chato kipindi hiki cha corona
Hakuna kiongozi ambaye ni kigeugeu, ambaye Taifa hili limepata kuwa naye kama Jiwe!

Hivi Mkuu wa nchi unawezaaje kutokea mbele ya hadhara na kuanza kumponda mteule wako kwa kashfa chungu mzima, kama alivyofanya kwa Mwigulu??

Haijapita hata miaka 2 unamrejesha yule yule uliyemuona takataka hapo siku za nyuma!

Huo ni ushahidi tosha kabisa kuwa kumbe kashfa zote ulizotoa wakati ule ilikuwa majungu!

Hivi kweli hakuna wananchi wengine ambao wako competent kushika nyazifa hizo??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom