Kurejea kwa 'Bongo Muvi' kupitia tamthilia, waandaaji wamejifunza au watarudi kule kule?

Nimewahi kuwataja kina Ray, JB n.k kama Watuhumiwa namba moja ya walioiua Bongo muvi.

Hawa na Wenzao walishika Tasnia wakishirikiana na Wasambazaji walikuwa wametanguliza pesa mbele.

Ipo haja Kampuni kama Azam na wengine kujifunza vizuri ujinga uliofanywa na kina Ray na steps wao wakauwa tasnia ili wasije wakarudia makosa.

Hawa Wasanii kuwapa full control ni hatari maana wao kipaumbele ni pesa na umaarufu, kama alivyokuwa steps alishika mpini...kwa sasa nao kina Azam, dstv na wengine wasiruhusu ule ujinga ujirudie.
Ray hajui kuigiza na sijawahi muelewa yeye anapayuka tu.
 
Dstv wamewapa promo kwa kuwatengea channel yao.

Na mimi si mpenzi wa hizo Bongo movie ila nilipomuona Joti nikaanza kuwa muangaliaji wa tamthilia ya Mwantumu.

Ila Wazambia ndio wanakimbiza na tamthilia yao ya MPALI iliyoingizwa sauti za kiswahili.
Yaaa,mpali noma!
Hata jua Kali,duh kwa bongo imetisha!
Huba ya kawaida
 
Bongo movie wanachemka kwenye waigizaji wao.Wanaangalia watu wanao trend social networks, akina dada wenye mishape na wenye sura nzuri, waigizaji wa kiume wana angalia ushombeshombe/hb ,kwao upande wa casting uzuri 90% talent 10%,vingine utajulia mbelembele matokeo yake story nzuri waigizaji wabovu.

Sasa husiombee ukutane na story mbovu waigizaji wabovu, utatamani uwaambie wenye ving'amuzi wakurudishie hela yako.

Wee Pierre Likuid na Nicolejoyberry nk nao waigizaji siku hizi, wadangaji wa mjini wote wamekimbilia bongo movie.
Na rommy ndugu yake dai,eti nae anaigiza!!!?
 
Yaaa,mpali noma!
Hata jua Kali,duh kwa bongo imetisha!
Huba ya kawaida
Kama kina Azam watashika hatamu vizuri huenda tukaendelea kuona mazuri zaidi na hata kufikia kazi nzuri kama zinazofanyika huko nje.

Ila kama nao watataka kuwaachia Waigizaji full control yatajirudia yale yale.

Kina Ray au JB sio watu wakuzingatia sana weledi kama utawaacha huru wafanye watakavyo, wao siku zote watakimbilia wanachokifikia kwa urahisi ili yao yaende....hatimaye tutarudi kule kule na Mashabiki kuipa tena tasnia kisogo.

Huo mfano wa mdau hapo juu kwamba nusu saa nzima Mtu anageuza Gari ndio yale yale yaliyokuwa yanafanyika Bongo muvi za steps..sasa Steps yeye hakujali ila sasa kina Azam, dstv n.k.wasikubali tena.
 
Mwanzo walibugi kumpa one step entertainment hakimiliki ya kazi zao.
Hili kosa lilipelekea kufa kwa bongo movie mapema sana.

Now kosa hili lisijirudie tena.

Pia wakati huu filamu zetu zinapaswa kutumia waigizaji wasomi kutoka katika vyuo vyetu.
Hiki ndo kimeibeba HOLLYWOOD. WAIGIZAJI WENGI NI WASOMI WANA ELIMU YA WANACHOKIIGIZA.

Sababu ya kujihusisha na siasa pia iliua bongo movie.

Hili niliweke wazi kabisa Watanzania tulimkosea Mungu ili kutuadhibu akatuletea hili dubwana la kuitwa CCM. huwezi lishabikia ukawa na akili au ukafanikiwa unakuwa mtu wa hovyohovyo tu.
Angalia wanachofanya waigizaji wetu kipindi cha kampeni upuuzi upuuzi mtupu..na kinachopelekea hivyo ni njaa.

Now wasijichanganye tena uigizaji ni sanaa inayoimulika serikali kwa undani sana. Thats why HOLLYWOOD kuna movie zinazohusu CIA,FBI, white house.

Kwetu hapa watu wasiojulikana ilipaswa iandaliwe filamu, Sabaya the criminal, Makonda misifa. Haya matukio yalihitaji filamu.

Jeshi letu pia lilipaswa kutuonesha walichoko nacho kupitia movie na sio kubeba magogo sikukuu za uhuru.

Police waruhusu matumizi ya nguo na vituo vyao katika filamu kuweka uhalisia.
Sio kila movie "mimi ni afisa wa police kutoka kituo cha kati"🤣

Jambo la mwisho ni rushwa ya ngono.
Waigizaji wengi kipindi kile walipata nafasi kwa sababu walikuwa wanapigwa mbupu na ma producers.

HAwakuangalia ubora wao na vipawa.
3DAB1797-29B7-4A54-AE8B-B21AD2B7F3DB.jpeg
 
Dstv wamewapa promo kwa kuwatengea channel yao.

Na mimi si mpenzi wa hizo Bongo movie ila nilipomuona Joti nikaanza kuwa muangaliaji wa tamthilia ya Mwantumu.

Ila Wazambia ndio wanakimbiza na tamthilia yao ya MPALI iliyoingizwa sauti za kiswahili.
Ila Nguzu ni mnyama aisee...
 
Za Azam bado kidogo. Filamu au Tamthilia za Bongo Movie zipo viwango zipo Dstv.
Hiyo ni kwa sababu dstv wanaweka vigezo.

Nimetoa mfano hapo juu namna ambavyo Holywood tangu 1920's walikuja na sheria zao kuhakikisha kazi hazifanywi kiholela ili kulinda hadhi na soko.

Azam wawe makini na wafuatilie maoni ya Watazamaji wao kwa ukaribu ili baadae wasije kukosa Watazamaji wa hizo tamthiliya kwa kuponzwa na Wasanii...twajua wao wana content nyingi za kuonesha hata bila Tamthiliya lakini chonde chonde wasiachie njiani nia yao nzuri ya kufufua Bongo muvi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom