Kurasa darasa TBC1: Magazeti na majarida katika historia ya Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,900
30,235
KURASA DARASA TBC1: UCHAMBUZI WA MAGAZETI, MAJARIDA KATIKA HISTORIA YA TANGANYIKA

Leo nilikuwa na matembezi ndani ya mitaa na vichochoro vya Maktaba nikimzungusha Mtangazaji wa kipindi cha ''Kurasa Darasa,'' Bi. Maureen Minanago.

Bi. Maureen alitaka kujua sababu za mimi kuhifadhi baadhi ya magazeti na majarida ambayo yeye aliyaona katika Maktaba yangu.

Nilimfahamisha kuwa mara nyingi nimekuwa nikihifadhi magazeti na majarida ambayo mimi mwenyewe kama mwandishi ndani yake kuna makala zangu nilizoandika.

Hii mosi.

Pili nimehifadhi majarida na magazeti yenye habari ambazo mimi nimeona zina umuhimu mfano wa Newsweek lililokuwa na makala ya kumbukumbu ya Auschwitz Kituo Kikuu Cha mateso na mauaji ya Wayahudi Vita Vya Pili Vya Dunia.

Nikamueleza kuwa kuna majarida ambayo wahariri wake tulikuwa tukifahamiana na ikatokea kuwa walipendezwa na makala zangu na wakawa wanachapa kila makala ninayowapelekea.

Nikamweleza mfano wa jarida la New African ambalo nikifahamiana na mmoja wa wahariri wake wakuu, Anver Versi na kwa bahati New African walikuwa wakipenda sana kuchapa makala kuhusu Julius Nyerere na siasa za Tanzania.

Katika kundi hili linaingia jarida la Africa Events ambalo lilijielekeza sana katika kuandika makala kuhusu Tanzania na hasa Zanzibar.

Nilimuonyesha jarida la Change ambalo Mhariri Mkuu alikuwa Juma Mwapachu na msaidizi wake Abdul Mtemvu.

Jarida hili lilikuwa la nyumbani likichapwa Dar es Salaam na wahariri wazalendo.

Nikagusia pia gazeti la Drum lililokuwa linachapwa Kenya mmiliki wake Jim Bailey raia wa Afrika ya Kusini na tukifahamiana.

Jim Bailey alijitahidi sana na kwa ujanja mkubwa kueleza mengi kuhusu Afrika ya Kusini katika kipindi kile cha ubaguzi.

Nilipata fursa pia ya kumuonyesha Bi. Maureen Scrap Book yangu ya mwaka wa 1988 ambayo ndani yake nilikuwa nimehifadhi mambo mengi kutoka magazeti yaliyokuwa yakichapwa nchini.

Ni tegemeo langu kuwa kipindi kitakaporushwa watazamaji weni wa kipindi hiki wataona magazeti mengi ya zamani ambayo mengi yao hayachapwi tena.

Screenshot_20220311-225654_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom