Kurasa 30 za ripoti ya Majangili Tanzania - wapo Mapolisi, Wanasiasa, Wafanyibiashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kurasa 30 za ripoti ya Majangili Tanzania - wapo Mapolisi, Wanasiasa, Wafanyibiashara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Aug 24, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Idara ya Ulinzi, Kitengo cha Intelejensia cha Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), imetoa ripoti ya ujangili iliyo na majina ya wahusika wakuu na namna wanavyolindwa na vyombo vya dola nchini.

  Habari hiyo iliyochapishwa kwenye gazeti la JAMHURI inasema kuwa, gazeti hilo (JAMHURI) litachapisha katika matoleo yake yajayo, ripoti iliyoipata yenye kurasa 30 iliyosainiwa na Mhifadhi wa Intelejensia, Renatus Kusamba.

  Gazeti hilo linaendelea kuandika,


  Kubwa zaidi kwenye ripoti hiyo ni kwamba hali ya ujangili katika hifadhi zote nchini inatisha, usalama wa wanyamapori uko shakani, idadi ya wanyamapori inaelekea kupungua, na juhudi za lazima zinatakiwa kuchukuliwa na jamii nzima katika kukabiliana na hali hiyo.

  Chanzo cha kuwapo uchunguzi huo ni mauaji ya faru jike na mtoto wake katika Hifadhi ya Taifa Serengeti, Mei mwaka huu. Ingawa dhima ya kitengo hicho cha intelejensia ilikuwa kufuatilia mauaji ya faru hao, mambo mengi yameibuliwa kwenye uchunguzi huo.

  Imebainishwa kuwa mtandao wa ujangili nchini unahusisha wafanyabiashara, watumishi wa idara za Serikali (Polisi, na Idara ya Wanyamapori - watumishi wa halmashauri) na baadhi ya raia wa kigeni.

  "Kundi hili ndilo linalofanya mipango ya kutafuta na kuleta silaha (bunduki hasa za kivita) na risasi na kuwapatia baadhi ya majangili/majambazi hao. Wafanyabiashara hao hukusanya meno (ya tembo na faru) na kuyasafirisha kutoka wilaya zinazozunguka Hifadhi ya Serengeti. Wafanyabiashara wakubwa wanawafadhili wafanyabiashara wadogo wa meno ya tembo. Wafanyabiashara wako katika wilaya za Bariadi, Kasulu, Kibondo na Lunzewe wilayani Kahama," inasema sehemu ya taarifa hiyo.

  Pamoja na makundi hayo, taarifa ya Tanapa imebaini kuwa waganga wa kienyeji wanatumika mno kwenye ujangili. Wanatumiwa kuwazindika majangili na majambazi kwa imani kwamba hawataweza kukamatwa wakati wa kuendesha vitendo hivyo.

  Kwa upande mwingine, baadhi ya viongozi wa Polisi wanatuhumiwa kuwamo kwenye mtandao wa kuwalinda majangili. Hayo yanathibitishwa na ripoti hiyo katika ukurasa wa 20 kwa mfano mmoja wa matukio hayo.

  "Asubuhi ya Juni 12, 2012 alikamatwa mtuhumiwa mwenye umri wa miaka 43 (jina tunalihifadhi kwa sasa) na bastola yenye risasi 10. Ni mkazi wa Magu. Katika mahojiano alionyesha kibali cha umiliki (photocopy) ambacho kinatia shaka na alidai bastola hiyo aliletewa na polisi aitwaye Mbogo aliyeko Mwanza na kwamba yeye hajui kuitumia. Aliachwa Kituo cha Polisi Mugumu Wilaya ya Serengeti ili mpango wa kufuatilia uhalali wa umiliki wake ukifanyika, lakini OCD wa Mugumu alimwachia muda mfupi baada ya askari wa Tanapa kumkabidhi kituoni hapo," imesema ripoti.

  Katika tukio jingine, ripoti inasema Julai 12 mwaka huu, taarifa za kiintelejensia zilionyesha kuwa mtuhumiwa mkuu wa ufadhili wa ujangili (jina tunalihifadhi kwa sasa), mkazi wa Kijiji cha Busunzu, Kibondo mkoani Kigoma, alionekana katika Kijiji cha Kifula wilayani Kibondo.

  Mtuhumiwa alikuwa akisakwa kwa muda mrefu kutokana na kutajwa na watuhumiwa wengine waliokamatwa Mei 11 mwaka huu, wilayani Serengeti wakiwa na risasi 430 na kufunguliwa kesi namba MUG/IR/1330/2012.

  Watuhumiwa hao walimtaja kiongozi wao (mkazi wa Busunzu) wanayesema huingiza silaha za kivita na risasi kutoka Burundi. Silaha hizo ndizo zinazotumika kufanyia ujangili katika Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire, Ziwa Manyara, Katavi, mapori ya akiba ya Moyowosi, Maswa, Rukwa/Rukwati na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

  "Mfadhili/jangili huyu ana uwezo mkubwa wa kifedha na ana mtandao mkubwa ulioenea karibu nchi nzima palipo na maliasili," imesema ripoti.

  Ripoti inasema kwamba afisa wa intelejensia alitumwa Juni 12 mwaka huu kumfuatilia. Alionekana katika Kituo cha Polisi Kifula akifungua kesi ya kuibiwa vitu katika baa yake.

  "Mtuhumiwa akiwa kituoni hapo, Kitengo cha Intelejensia kilichokuwa Serengeti kilimuagiza afisa wake aliyekuwa akimfuatilia amkamate mara moja kwa kuomba msaada wa polisi kituoni hapo. Hata hivyo, afisa huyo hakupata ushirikiano ikamlazimu kutumia mbinu za kisasa kufukuzana naye na kisha kufanikiwa kumkamata na kumrudisha kituoni. Wakati huo Kikosi cha Tanapa (Serengeti) kwa kushirikiana na askari polisi kutoka Kituo cha Mugumu, walikuwa wako njiani kumfuata mtuhumiwa huyo na walipofika walimkuta ameshakamatwa. Mtuhumiwa alipelekwa katika Kituo cha Kibondo ili kusubiri askari kutoka Serengeti wamchukue. Mara baada ya askari wetu kufika kituoni hapo walikataliwa kumchukua kwa amri ya RPC Kigoma, RCO Kigoma, OCD Kibondo na OCD-CID Kibondo. Kutokana na hali hiyo RPC na RCO Kigoma walituma kikosi maalumu cha kumfuata na kumpeleka Kituo cha Polisi Kigoma mjini. Hali hiyo ililazimu kuomba msaada kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania ili awasiliane na ngazi za juu kuangalia uwezekano wa kumchukua mtuhumiwa huyo na kumfikisha Kituo cha Polisi Wilaya ya Serengeti (Mugumu) aweze kujibu mashitaka. Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa alituma Kamanda mstaafu Venance Tossi kwenda Kigoma kwa ndege ya shirika kumchukua mtuhumiwa huyo na kumleta Serengeti-Seronera na kumkabidhi mtuhumiwa huyo kwa Mkuu wa Hifadhi na kupelekwa Kituo cha Polisi Mugumu," imesema ripoti.

  Watuhumiwa wengine wa ujangili wanaotajwa ni Bwana Nyama Wilaya ya Karatu aliyetajwa kwa jina moja la Simon. Anamiliki rifle aina ya 404, Mzee Lazaro anayetajwa kwamba ni Mwenyekiti wa CCM Kitongoji cha Karatu, na watumiwa wengine ambao ni watu maarufu.


  Source: Kurasa 30 za ripoti ya Majangili Tanzania - wapo Mapolisi, Wanasiasa, Wafanyibiashara - wavuti
   
 2. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Namhurumia Mwema na vikaragosi vyake. Hawatakaa wafaidi matunda ya kazi zao baada ya kustaafu.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nasubiri MAJINa kwenye toleo LIJALO,ENDAPO LITABANDIKWA HAPA,,,,SITALINUNUA
   
 4. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Halafu Ezekiel Maige anakuja kudai AMEFADHAISHWA SANA, AMEDHALILISHWA SANA, AMEONEWA SANA kutolewa Uwaziri wa Maliasili. Hii Nchi nani kairoga!!!???.
   
 5. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni Mchungaji Msigwa aliliambia Bunge kuhusu huyu Mzee Lazaro kuwa ni anahusika wa ujangili wa wanyama pori.
   
 6. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kila kukicha tunapata taarifa za ufisadi mkubwa kuliko ule tuliokuwa tunajua. Hii nchi ingekuwa tajiri kuliko Luxemburg
   
 7. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  rage nae ndani
   
 8. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hili JAMHURI hili.....linajifanya kumrithi MwanaHalisi!
   
 9. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii nchi imeoza kila mahali. Ukiitisha uchunguzi wa kina kila sekta kila idara, you will be shocked. Report ya CAG ni just a tip of an iceberg.
   
 10. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,382
  Likes Received: 319
  Trophy Points: 180
  Msigwa Haya madudu yote aliyasema ila kwa vile tunaongozwa na wala rushwa,
  huu ni upepo tu.....
   
 11. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Huu ni upepo tuu na another silly episode nayo itapita tuu
  maana hakuna mwenye ujasiri wa kumvika paka kengele kwenda kumkamata panya
  panya wamekuwa na nguvu na umoja wa hali ya juu hawawaogopi paka maana panya wanaongia mkapa chumbani kwa mwenye nyumba na kutafuna mpaka suti zake na kula chakula cha paka ila paka hawana tena hata ubavu wa kuwakamata panya
  Na panya wana pesa na nguvu za ziada kiasi kwamba hata paka hawaoni wakati wanakula rasilimali zake
   
 12. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,640
  Likes Received: 2,002
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa magamba, Spika, Nape,& et al walikataa katakata na kusema eti taarifa hiyo ni Uzushi mtupu!
   
 13. mito

  mito JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,653
  Likes Received: 2,039
  Trophy Points: 280
  Tumpe muda Kaghasheki aunde upya safu ya uongozi pale maliasili, haya madudu yatapungua sana kama siyo kuisha akiweka watu makini
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Polisi wanawafahamu majangili sema ndio wapo nao karibu sasa.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kitendo cha report kuwekwa hadharani ni sehemu ya soln,Kagasheki sasa pa kuanzia unapo and I know you can
  wakikuletea blah blah jiuzuru tuu maana deep inside your heart una uzalendo
  watz tuko nyuma yako na tunakutegemea ktk ilo
  all the best
   
 16. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Endapo watastaafu
   
 17. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwa hali ya mambo kama haya kila kukicha jk na serikali yako utathubutu kusema ni safi na sikivu?
   
 18. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  nilikuwa najiandaa kupost hapo bold, sijaona cha maana kwenye hii habari kwasababu waliotajwa ni wawindaji wa vijijini "Wafanyabiashara wako katika wilaya za Bariadi, Kasulu, Kibondo na Lunzewe wilayani Kahama" na si yale majangiri tunayoyataka yanayomiliki meli iliyokamatwa na tani za pembe za ndovu huko Hong kong

  vigogo wenyewe wa polisi wanaotajwa humu ni "askari polisi kutoka Kituo cha Mugumu"! tunahitaji kufahamu nyara zinatoka vipi nje ya mipaka ya nchi either kwa kutumia ndege, bandari au border na si habari za wanunuzi waliotajwa hapo ambao ni waganga wa kienyeji
   
 19. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii habari inaudhi, inakasirisha na kusikitisha. CCM na serikali yake wametuangusha wananchi katika kila hali. Madudu kama haya na mengine mengi serikali ilibidi iwe imejiuzulu zamani lakini mfumo ni tatizo. Watanzania tutalalamika mpaka lini? Tuvumilie tu japo kwa utendaji huu 2015 ni mbali sana sijui nchi itakuwa na hali gani wakati huo. Sanduku la kura ndiyo dawa ya kuondokana na huu utawala dhalimu
   
 20. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ccm wakiendelea kuingoza hii nchi kama miaka kumi tena tutabaki majivu ahadi walizooa 50 yrs ni tofauti kubwa kwahio wafanya kazi wengi asilimia kubwa ni wizi kwenda mbele hata ukiwasikiliza mfano juzi mkuu wa takukuru chn 10 eti anasema sheria ni mbaya hazimpi uwezo wa kufanya kazi inamaana yeye pale anafanya nini .
  plce ,mahakama ,hospital ardhi hata siku hizi mabenk nayo yamesha ambukizwa unaweza kaa benk masaa 4 mara mtandao mbovu mara teller kaenda chooni basi tu
   
Loading...