Uchaguzi 2020 Kura zipigwe kwa kwa kutumia simu/kompyuta, uchaguzi 2020

ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,317
1,229
Tumaini langu mko sawa !!

Ni wiki mbili sasa au pengine na zaidi , tumekuwa tuna kuna vichwa kuwaza ni kwa jinsi gani serikali itaweza kutatua tatizo hilo la watu kutofika katika vituo vya kupigia kura

Nawaza TU kwa sauti kwamba katika dunia hii tuliyopo ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa teknolojia almost katika kila kitu

Imekuwaje Imeshindikana kutengenezwa mfumo maalumu ambao utaratibiwa vilivyo ,ambao kimsingi utawezesha mtu mwenye vifaa Kama simu au kompyuta kupiga kura sehemu yoyote alipo
Ikizingatiwa kuwa kwa sasa watanzania wanao miliki smartphone wameongezeka Sana kiidadi

NIELEWEKE ;Sisemi kuwa huu mfumo uliopo tuuache Hapana ,kwa sababu najua IPO idadi kubwa pia ya watanzania waishio vijijini ambapo mfumo huo Wa kupiga kura kwa kutumia smartphone au computer ukawa mgumu kwao

Mifumo yote iwepo kwamba anaye weza kwenda kupanga foleni basi afanye hivyo
Na kwa yule ambaye anatingwa na harakati zingine basi apige akiwa popote pale

NI MAWAZO TU NA NIPO TAYARI KUSAHIHISHWA NA KUELEKEZWA karibuni !!!
 
si unaona watu wa masaki it wa bao la mkono walivyotaka kuleta tabu na watu wa it waliochukuliwa na marope kutoka mlimani city tallying center ni muhimu japo watu wanaweza kuzihack
 
si unaona watu wa masaki it wa bao la mkono walivyotaka kuleta tabu na watu wa it waliochukuliwa na marope kutoka mlimani city tallying center ni muhimu japo watu wanaweza kuzihack
yes kweli lakini, hata zisipo kuwa hacked bado watu wana chakachua kote shida IPO
Nililenga katika namna ya kurahisisha zoezi
 
wazo lako ni zuri kwa kuwa kimekenga kuondoa msongamano na muda kupotea. lakini jiulize maswali yafuatayo:

1. Kuna ambao wamefariki au wameugua kichaa baada ya kujiandikisha kupiga kura, je mfumo huo utatambuaje watu hao?

2. Je, uhakika wa kura zinazopigwa kujumishwa katika mfumo Wa jumla utahakikishwa vipi?

3. Je , mfumo huo utazuiaje watu kupigiana kura? Je ,hautavunja katiba kwa baadhi ya wagombea kufanya kampeni siku ya kupiga kura?
 
uwekwe mfumo siyo kupiga kwa namna ya mitandao ya simu Bali internet Kama TUZO za MUZIKI vile
Kwa akili hizi za kiafrika kabisa?? Mtu anaingia kwenye chumba cha kupigia kura, anabeba box lenye kura, anaondoka nalo, anaenda huko nyuma anafanya anavyotaka na kisha kurirudisha tena!! Na bado zoezi linaendelea, na anaonekana wazi na vyombo vya ulinzi na usalama, sembuse huko mtandaoni?!!!! You are joking!!!!
 
Kwa akili hizi za kiafrika kabisa?? Mtu anaingia kwenye chumba cha kupigia kura, anabeba box lenye kura, anaondoka nalo, anaenda huko nyuma anafanya anavyotaka na kisha kurirudisha tena!! Na bado zoezi linaendelea, na anaonekana wazi na vyombo vya ulinzi na usalama, sembuse huko mtandaoni?!!!! You are joking!!!!
mbona unazo documents zako umehifadhi mtandaoni na ni very potential
NA wewe unatania siyo?
 
KARLO MWILAPWA,

MAJIBU

1. Kama kweli mtu kaugua kichaa basi ni dhahiri hatokuwa na uwezo Wa kutumia devices Kati ya hizo, kwa hapo itakuwa ni sàwa na mtu ambaye amejiandikisha lakini hajapiga kura ,the thing which is normal

2. Kuhusu mjumuhisho Wa kura haiwezi kuwa tatizo ka ma kuna dhamila ya kweli ni suala la collect data correctly

3. Nadhani suala la kupigiana kura ni jambo Dogo ukiwa Kama kitawekwa kipengele cha kutumia finger prints Kama tulivyo jisainisha katika ule mfumo Wa BVR
 
Inawezekana hata kwa vitochi,muhimu elimu na maboresho sheria uchaguzi kumiliki line ya simu iwe kigezo,NIDA id
 
Ccm bado tu watatafuta namna waibe, hata kama ingekuwa mtihani wa watoto wa chekechea kwa vyama, bado wataiba tu. These people are sworn kleptomaniac.
 
Back
Top Bottom