Kura Zakutwa karibu na msituni kata ya Njoro wilayani Moshi

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,904
4,050
Njoro wameokota kura 448 ltkt mfuko wa rambo, za CCM, wameokota katika pori huko Njoro.

000000000000000000000000kura.png

Wakazi wa kata ya njoro katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wameokota kura zipatazo 448 ,zikiwa kwenye mfuko uliyotupwa kandokando ya msitu wa asili wa njoro uliyopo katika kata ya hiyo ,baada ya kupata taarifa kutoka kwa mtua ambaye hakuweza kufahamika mara moja.

Akizungumza katika eneo la tukio ,katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Moshi mjini Loti Olenesele amesema baada ya kupata tarifa walifika katika eneo hilo ,na kuzikuta kura hizo ambazo ni miongoni mwa kura zilizopigwa October 25 mwaka huu katika nafasi ya ubunge na urais kupitia CCM ,na kwamba zilikuwa na mhuri halali wa tume ya uchaguzi.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro Aggy Mariale amesema awali kulikuwa na malalalamiko ya kupotea kwa masanduku mawili ya kura na kwamba baadhi ya mawakala halishatoa malaamiko kuhusu hujuma zilizo kuwa zikifanyika kwenye uchaguzi wa octoer 25 mwaka huu lakini hawakuweza kusikilizwa .

Chanzo: Channel ten
 
Walishindwa kuziingiza kituo cha kupigia kura wampelekee Lubuva azijumlishe kwenye zile milioni 8
 
Njoro wameokota kura 448 ltkt mfuko wa rambo, za ccm, wameokota ktk pori huko Njoro,

source CH 10

tume itende haki. Uchaguzi wa ubunge Moshi ulikuwa na mizengwe mingi hivyo ni vema ukarudiwa. Yaani chadema mwaka huu wametumia kila aina ya ujambazi wa kura!
 
tume itende haki. Uchaguzi wa ubunge Moshi ulikuwa na mizengwe mingi hivyo ni vema ukarudiwa. Yaani chadema mwaka huu wametumia kila aina ya ujambazi wa kura!
Mkuu umeamanisha CHADEMA au CCM….Vingine njoo huku urekebishe
 
Na zipeleke kwa Lubuva akazijumlishe mana hizi sio za kwanza kukamatwa na hajawahi kutoa tamko lolote zaidi ya kuendelea kujumlisha kura zake
 
Lubuva akaziongeze na hizo zifikie 100% kabisa, haka kazee nakachukia sana.
 
Kwanini ziwe za CCM tu, inamaana watu wote kwenye box hizo waliipigia CCM tu? Hizi ni kura za wizi CCM walishindwa kuzitakatisha.
 
Mimi naamini ipo siku MUNGU atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. MUNGU huwa hadhiakiwi, apandacho mtu ndico atakachovuna, kama sio hapa duniani basi ni jehanamu ya moto baada ya kufa.
 
Mtakuja kuokota hadi kinyesi kilichoandikwa Ccm,,alimradi tuonekane wabaya si ndio,,,mmejiprintia kura ili mpate ushahidi wa kupeleka Icj
 
Wameibaaaaa hadi karatasi za kura zimezagaa mitaani za Kura za CCM, na zimepigwa...!!!

Aiseee...!!😨😨
 
Mimi naamini ipo siku MUNGU atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. MUNGU huwa hadhiakiwi, apandacho mtu ndico atakachovuna, kama sio hapa duniani basi ni jehanamu ya moto baada ya kufa.
Hili ndilo unalikumbuka leo? Tena kwenye siasa? Fisadi angeshinda ungelikumbuka? Wewe hapo una madhambi mangapi? Unafikiri Mungu Akiamua kukushughulikia hapo utapona? Acha unafiki wewe. Wasiliana na Mshenga atakufafanulia vizuri jinsi Mungu wetu mwenye upendo na rehema tele anavyofanya kazi.
 
tume itende haki. Uchaguzi wa ubunge Moshi ulikuwa na mizengwe mingi hivyo ni vema ukarudiwa. Yaani chadema mwaka huu wametumia kila aina ya ujambazi wa kura!

Maajabu haya, yaani kura zimeokotwa zimepigwa tick ya CCM halafu majambazi ya kura hizo wawe Chadema?
 
tume itende haki. Uchaguzi wa ubunge Moshi ulikuwa na mizengwe mingi hivyo ni vema ukarudiwa. Yaani chadema mwaka huu wametumia kila aina ya ujambazi wa kura!
Umeambiwa hizo kura ni za CCM..hujui kusoma? Mwambieni Lubuva afute uchaguzi kama Jecha alivyofanya Zanzibar. Tume si ya kwenu?
 
Maajabu haya, yaani kura zimeokotwa zimepigwa tick ya CCM halafu majambazi ya kura hizo wawe Chadema?
Labda hatujamwelewa. Yawezekana majambazi ya CHADEMA yaliiba kura za CCM wakaenda kuzitupa huko porini. Kwa maana hiyo CCM wakashindwa kuzifikisha vituoni, jambo lililowanyima ushindi. Wao wanaona kuingiza kura kwa hila ilikuwa haki yao.

Yaani kama nasoma kile kisa cha Mfalme Juha
 
Mimi naamini ipo siku MUNGU atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. MUNGU huwa hadhiakiwi, apandacho mtu ndico atakachovuna, kama sio hapa duniani basi ni jehanamu ya moto baada ya kufa.

Malipo ni hapahapa duniani,si umaona Zanzibar hiyo inaondoka. Hiyo iyakuwa pigo takatifu kwa ccm.
 
Back
Top Bottom