Kura za Watanzania zama hii zazidi kutokuwa siri

edwardbm

JF-Expert Member
Nov 3, 2016
292
251
Tofauti na vipindi vya Uchaguzi wa vyama vingi nilio ushuhudia, 1995 Hadi 2015, Uchaguzi wa mwaka huu wananchi wengi zaidi wako radhi kusema hadharani ama kukuambia Kura yake atampa Nani.

Kwa Chaguzi zilizopita ilikua ni kwa wale wakereketwa wa vyama husika tu ndio walikua wakitoa misimamo yao wazi, juu ya Nani ambaye atampigia Kura.

Wananchi ambao hawakuwa wanachama wa chama chochote Cha Siasa ama sio wakereketwa hawakuwa na tabia ya kusema wazi Kura zao wangempa mgombea yupi.

Zama hii imekua tofauti sana.

Kwa uchunguzi wangu binafsi Raia mitaani Sasa hivi wanakuambia wazi wazi kwamba Kura zao watampigia mgombea, au wa CCM au wa CHADEMA. Hasa vyama hivi viwili. Raia Hawa ni wale ambao hawaonyeshi kuwa ni wakereketwa na sio wanachama wa vyama vyovyote vya Siasa.

Awali kwa Chaguzi zilizopita ukimuuliza mtu aidha atakujibu, sijui bado, ama wengine watakuambia ni siri yangu. Ila kwa Uchaguzi huu mapema yote hii"bado zaidi ya mwezi kufikia siku ya kupiga Kura" tayari wengi wameshafanya maamuzi ya wampigie Kura Nani hasa kwa ngazi ya Urais.

Wapo ambao nimewauliza wakasema "CCM Magu mitano mingine."Na wapo ambao wasema wazi "CHADEMA Lisu, Ni yeye. ."

Kinachonifurahisha zaidi ni Pande zote mbili wanakujibu kwa Kujiamini na kujivunia machaguo yao.

Je, ni Raia tumekua na mwamko wa Siasa. Ama ni Uchaguzi huu tu.?

Au Ni Raia tumekua wawazi zaidi na wakweli na nafsi zetu.?

Au Ni Ushabiki umekomaa, au Ni Maisha yamebadilika.?

Isije ikiwa Ni mtazamo wangu tu. Na hamna kilicho badilika.

Tanzania ni Yetu sote, watanzania.

Ebm.
 
Tofauti na vipindi vya Uchaguzi wa vyama vingi nilio ushuhudia, 1995 Hadi 2015, Uchaguzi wa mwaka huu wananchi wengi zaidi wako radhi kusema hadharani ama kukuambia Kura yake atampa Nani...

Maamuzi ya kura apigiwe nani si Siri tena. Tunasubiri kura ziibiwe timbwili liwake moto. Wengine wawe wakimbizi, wengine waburuzwe The Hague (ICC) na wengine tukutane barazani kwa Mungu. NEC/ZEC fanyeni uhuni wa kijecha safari hii mshuhudie haya.
 
Kama walivyoburuzwa MIGA

Viva Magu
Maamuzi ya kura apigiwe nani si Siri tena. Tunasubiri kura ziibiwe timbwili liwake moto. Wengine wawe wakimbizi, wengine waburuzwe The Hague (ICC) na wengine tukutane barazani kwa Mungu. NEC/ZEC fanyeni uhuni wa kijecha safari hii mshuhudie haya.
 
Back
Top Bottom