Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,302
- 24,142
Mcheza kwao hutuzwa.Katika hali ya kushtua na inayopiga butwaa ni kubwagwa kwa Mwakyembe kura za maoni.
Mawaziri wa kiume woote kasoro yeye tu wamepita kwenye kura za maoni.
Manaibu waziri pia woote, yaani wote hata wale waliotoka upinzani wamepita.
Cha kwanza nakosa imani na kura za maoni majimbo yaliyokuwa na mawaziri, nanusa harufu fulani ya mkono wa mtu katika kura za maoni majimbo ya mawaziri na manaibu waziri.
Pili, nashindwa kuwa na jibu inakuaje Mwakyembe peke yake waziri katika mawaziri wote wa kiume yeye pekee tu apoteze kura za maoni?
Waziri asiyeahidi neema kwa wapiga kura wake ana faida gani?
Tumeona Dr Harrison Mwakyembe , akijisifu sana na degree zake nne na udaktari wa falsafa ambao haujawasaidia sana wapiga kura wake.
Sana sana anawadharau wapigakura wake darasa la saba,masikini, ambao ni wengi jimboni kwake.
Huyo hafai, hafai hafai.