Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Mimi si mwanasiasa na kwa bahati mbaya sana nimejikuta nikiichukia siasa kutokana na ulaghai na majigambo ya baadhi ya wanasiasa wa Tanzania. Nikiwa mkazi wa jimbo la kawe nimefikia mahali nashawishika kusema kuwa mbunge wa sasa wa jimbo la kawe Rita Mlaki si kiongozi wa kutumikia wananchi hata kidogo. Mtu anaweza kusema nina chuki na huyu mama, HAPANA...Lakini huyu mama katika muda wote akiwa mbunge ameshindwa kutekeleza yale aliyoahidi kwenye kampeni zake 2005. Baadhi ya mambo hayo ni kuondoa kero ya upatikanaji wa maji katika maeneo kadhaa ya jimbo hilo kama vile Makongo Juu, barabara mbovu kutokea chuo cha ardhi kuelekea huko huko makongo juu,barabara mbovu kabisa na kero ya maji eneo la goba.
Tunashuhudia kero na tabu ya usafiri kutoka mwenge kufika huko makongo. Nauli za daladala zinaongezeka kadri muda unavyokwenda. Kuanzia asubuhi mpaka saa 12 jioni nauli Sh. 250, kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 2 usiku nauli Sh.300, kuanzia saa 2 na kuendelea nauli ni Sh. 500. Unaweza kuwalaumu wenye magari lakini wanachofanya ni sawa kwa upande fulani kwani kwa hali ya barabara katika eneo hilo mwisho wa siku ni kuharibu magari yao. Kwa hiyo kwa mtazamao wangu huyu mama hafai tena kupewa kura za ubunge. CCM kama watataka kuleta mambo ya kushinikiza kuweka wagombea wao kwa interest zao ni wazi watapata aibu.....Wanakawe tuache unafiki tuwe wakweli kwenye hili. Kukubali kununuliwa na kisha kupata usumbufu na kero kwa miaka mingine mitano haiwezekani....