Kura yangu kwa atakayeshulikia kero ya "Fixed Charge" katika madai ya Tanesco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura yangu kwa atakayeshulikia kero ya "Fixed Charge" katika madai ya Tanesco

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ntemi Kazwile, Oct 5, 2010.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kero ya Fixed Charge kwenye ankara za Tanesco ni miongoni mwa kero nyingi ambazo zimekuwepo muda mrefu lakini hakuna hata kiongozi mmoja anayeelekea kuitatua.

  Ukitaka kuweka umeme kwenye jengo lako na ukawafuata Tanesco watakwambia ulipe gharama za kuweka huo umeme, ambazo ni pamoja na gharama za kufungua file, utanunua meter, na gharama nyinginezo; na wakati mwingine utalipia nguzo ambayo baada ya hapo inakuwa mali ya Tanesco. Hizi kabla hujaweka gharama za kuwapoza wahusika ili kusudi file lako lisipotee au kuwekwa kwenye foleni na mizimu ambayo inaweza kukuchukua hata miaka mitano kama hautawatoa wahusika.

  Cha kushangaza ukianza kutumia huo umeme wanacharge, pamoja na mambo mengine FIXED CHARGE, hii ni gharama ya kudumu na sijui ni kwa ajiri ya kugharimia kitu gani.

  Miujiza haishii hapo tu, lakini inaongezeka na kuwa mauza uza pale shirika hili linapolitiwa kuwa linaendeshwa kwa hasara!!!

  Sijasikia hata mgombea yeyeto wa ngazi ya urais au ubunge ambaye anataka kuishughulikia kero hii.

  Jana nilinunua umeme wa luku wa sh.30,000 na jumla ya kodi mbali mbali nilizolipa zilikuwa ni 10,150 hii ina maana kuwa ninachangia kodi za serikali kwa takribani asilimia 49% ya kila umeme ninaonunua . Hii ni kodi kubwa sana na ninastahili kupata huduma stahili siyo kukatiwa umeme bila taarifa, kupata umeme chini ya kiwango (low voltage), kuchelewa kurejeshewa umeme pindi linapotokea tatizo kwenye mfumo wa usambazaji au uzalishaji.

  Ninaomba kero hii ipatiwe majibu
   
 2. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Suluhisho lako ni Dr.Slaa jibu analo
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nami nakeleka na fixed charge isyo na maelezo. Nafikiri ni mchango kwa kampeni za majambazi wa CCM
   
 4. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100, michango sijui zinaitwa kodi au sielewi jina lake kuna EWURA, REA, TRA(VAT) n.k vyote vimo kwenye bill sielewi maana yake nini, Maana kodi ( VAT) ilivyopo hapo ndiyo inayokwenda serikalini kwa ajiri ya uendeshaji wa serikali yake pamoja na taasisi zake kama EWURA , REA n.k. Sasa iweje mwananchi, mlalahoi, masikini achajiwe mara mbilimbili????

  Kweli suluhisho ni Dr. Slaa na akiingia hii kero aishughulikie mara mmoja.
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na kila mwaka wizara ya nishati inapangiwa budget, sijui hii hela ni mishahara na marupurupu ya vikao??? Yaani CCM hakuna kipaumbele kabisa
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,604
  Trophy Points: 280
  Kodi zote ziondolewe kwenye umeme kama kweli tunataka sera ya umeme vijijini kuwa na tija na mafanikio. Hizi bei za umeme kamwe vijijini hawataweza kuzimudu kutokana na mapato yao hafifu.

  Sehemu kubwa ya kodi ya umeme wala haiendi kuimarisha miundo mbinu ya umeme ila inakuwa kichocheo cha ufisadi kama EPA, RADAR, na mwingineo.
   
Loading...