Kura yangu haitaenda CCM kamwe.

Hebie

Hebie

JF-Expert Member
1,317
2,000
Ni miaka 7 sasa tangu nimiliki kadi ya CHADEMA iliyosainiwa na Kamanda Mbowe. muda wote huo nimekuwa kwenye misukosuko na familia kwa kuwa wao ni makada wa ccm.

Kuna kipindi niliwahi kuletewa kadi ya ccm yenye jina (jofrey) ili nipige kura ya maoni ndani ya chama nimchagua Nape ili aweze kugombea ubunge jimbo la Ubungo nikala pesa nikalala mbele.

Nimeona mengi na ahadi nyingi za ccm na cdm nimegundua ccm longolongo hakuna utekelezaji.

Mbunge wangu Mwakyusa Wilaya ya Rungwe mashariki [imegawanywa] umeme umeishia mjini Tukuyu kila chaguzi ni wimbo wake kuwa tutatumia ule wa STAMICO hadi leo giza. je niendelee kuamini huku bibi yangu anatumia kibatari na mafuta yanapanda bei kila leo?

Barabara ya Ikuti inayounganisa hadi wilaya ya Ireje tope tupu mvua ikinyesha kodi yangu inaenda wapi? mlikiri kuna magamba (wasaliti) ndani ya ccm wanakwamisha maendeleo kwa wizi, mbona hamuwatoi?

CDM wameonyesha wakipewa madaraka wataweza kwa kuwatoa wasaliti pasi na kujali umaarufu wao. kura yangu nitawapa walionyesha nia.
 

Forum statistics


Threads
1,424,934

Messages
35,076,363

Members
538,167
Top Bottom