Kura yako ilihesabiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura yako ilihesabiwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jobo, May 22, 2011.

 1. J

  Jobo JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Leo nimekaa nikiwaza nchi yangu inapoenda, nikaamua kujiuliza kama kweli tuna viongozi wenye nia ya kutuongoza na kutufikisha katika neema ya angalau milo mitatu kwa siku! Nimeshindwa kuelewa ni kwa sababu zipi kila siku inabidi mtu uondoke nyumbani saa kumi alfajiri ili kuwahi kazini na ukifika huko kazi zenyewe hazileti tija bali ni kukaa, kusoma magazeti ya udaku na kujaribu kuganga njaa kwa kutafuta semina na mikutano ili angalau uambulie posho itakayopelekea familia yako ipate mlo kwani mshahara hautoshi hata kidogo. Ni nchi ambayo hata zinaponyesha mvua umeme ni wa mgao na bei ya mafuta na gesi haishikiki! Nikajiuliza kama kweli Watanzania ambao kila siku ndugu zao wanauwawa na askari polisi, majambazi na ajali za barabarani bila kujali mabomu ya kijeshi wanaweza kuwapatia kura viongozi ambao aghalabu hawajali hali zao bali matumbo yao na ya vimada wao! Ndiyo maana nakuuliza, hivi kweli kura yako ilihesabika Desemba mwaka jana? Nipeni jibu labda akili yangu itatulia kidogo!
   
 2. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  KURA zilichakachuliwa NYINGI sana ikiwemo KURA YANGU
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Hata mtu ungeruhusiwa kupiga mara3 kwa mtu1 bado NEC isingeruhusu kura zako kubadilisha matokeo,kimsingi kura zetu hazikuhesabiwa,kura ziliwekwa kando wakatoa walichokikusudia wao na ndo maana mpaka leo NEC imeshindwa kutoa jumla ya matokeo ya kura zetu...it was like voting for leisure,the cursed nec!
   
 4. J

  Jobo JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sad isnt it? Na watanzania wamekaa kimya kama vile kilichotangazwa ni halali! Siku zote huwa najiuliza, hivi mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi hana kikomo? Kuna jamaa aliniambia kuwa wakati wa uchaguzi Katibu na Mwenyekiti wa Tume walikuwa wamemaliza muda wao! Hivyo uwepo wao ulikuwa batili na yamkini walibakizwa kwa shughuli ya kuchakachua
   
 5. J

  Jobo JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hata yangu ilichakachuliwa! tufanyeje ili kura ya kila mtanzania ihesabiwe?
   
Loading...