Kura ya Mungu ipo kwa Lissu 2020: Mwaka 2015 Ilikuwa kwa Magufuli; wapi alikosea Magufuli? jionee

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,882
MUNGU AMEMPA KURA LISU, JE WEWE UTAMPA NANI?

Na, Robert Heriel

Hata Mungu hufanya uchaguzi, Hata Mungu hupiga kura. Sio mwanadamu peke yake apigaye kura, hata Mungu Muumba wa Mbingu na ardhi hupiga kura.

Katika Historia ya Biblia wapo watu kadhaa waliopigiwa kura na Mungu miongoni mwao ni hawa hapa;

1. Daudi mwana wa Yese
2. Yakobo mwana wa Isaka
3. Yusuph mwana wa Yakobo ndiye Israel
4. Suleiman mwana wa Daudi
5. Yesu mwana wa Maria
6. Yeremia Mwana wa Hilikia
7. Muhamad mwana wa Abdullah
8. Musa kutoka Kabila la Lawi Miongoni mwa wateule wengine.

Wapigiwa kura karibu wote au tuseme zaidi ya 99% ya waliochaguliwa na Mungu walikuwa na sifa zifuatazo;

1. Hawakutoka katika familia kubwa zenye utajiri. Karibu wote wametokea familia masikini au za kawaida
2. Wote walikuwa na ujasiri unaofanana wa kutetea haki
3. Karibia wote walikimbia uhamishoni
4. Karibia wote walinusurika kuuawa, na wapo waliouawa kabisa. Waliozeeka walikuwa wachache pia
5. Wote walipata kura chache kutoka kwa wanadamu wenzao, walikataliwa, ila walipata kura ya Mungu.
6. Karibu wote waligombana na serikali zilizokuwa madarakani kwa wakati wao. Na sifa zingine.

Mfalme Daudi hakupigiwa kura na wanadamu, au ndugu zake. Kisa kinaanzia pale Nabii Samweli anatumwa akampake mafuta Mfalme mpya wakati tayari yupo Mfalme Sauli anatawala. Nabii Samweli anamuwekea ubishi Mungu kwa kuogopa kuuawa na Mfalme Sauli mara atakaposikia kuwa yeye kaenda kumpaka mafuta mfalme mwingine. Hapa tunaweza kusema Nabii Samweli anaogopa kupindua serikali ya kifalme ya Sauli(Hata sasa ni kosa la jina kupindua serikali "UHAINI" na hukumu yake ni kifo) Basi tunaweza kusema Nabii Samweli alikuwa anahaki ya kukataa wito wa Mungu wa kwenda kumpaka mafuta Mfalme mpya Mfalme Sauli yungali hai.

Mungu anamshawishi Nabii Samweli kwa kumwambia kuwa Roho yake imehama kutoka kwa Mfalme Sauli kutokana na Maovu ayafanyayo. Basi Nabii Samweli akakubali wito wa Mungu wa kufanya kosa la Uhaini(kupindua serikali ya Sauli) huku akijua madhara yanayoweza kumpata.

Nabii Samweli anateremkia Bethlehemu huko aishipo Mzee Yese, ndiye huyo Baba wa watoto wakiume Nane Daudi akiwa mmoja wapo kama mtoto wa mwisho. Samweli alipoona watoto wakubwa wa Yese akiwepo ELIABU na ABINADABU moyo wake ukawachagua hao, hata Yese mwenyewe ambaye ni Baba alijua kuwa watoto wake wakubwa ndio watapata hiyo Bahati ya kupakwa mafuta ili baadaye mfalme atoke kutoka kwao. Lakini Kura ya Mungu haikuwa juu yao. Mungu akasema; Yeye aangalii sura au urefu wa mwili bali anaangalia Moyo.

Basi Daudi akaenda kuitwa kwani hakuwepo bali alikuwa akichunga mifugo huko porini. Alipofika tuu, Mungu akamuambia Nabii Samweli, mpake huyo Mafuta. Huyo ndiye atakuwa Mfalme.

Kumbuka, hata Mfalme Sauli alipakwa mafuta na alichaguliwa na Mungu lakini baadaye alikuja kuzingua, na ndio maana Kura ya Mungu ikahama kutoka kwake kwenda kwa Daudi.

Daudi anakuja kwenye utawala baada ya kumuua Goliath au Jaluti, kisha anakoswa koswa kuuawa na Mfalme Sauli, lakini Bado Mungu anakuwa juu yake.

Kisa cha Daudi ni moja ya visa vinavyoweza kumpa mtu maarifa na uzoefu wa mambo ya kisiasa na kiutawala.

Katika kisa hiko tunaona kuwa, Kura ya Mungu ilikuwa kwa Daudi na ndio maana Mfalme Sauli alishindwa, ingawaje naye alipewa kura zamani ndio maana akawa Mfalme.

Kisa cha Pili ni Kisa cha Suleiman mwana wa Daudi ambaye tumeona kwa ufupi kisa chake.

Baada ya Mfalme Daudi kuzeeka, kifo ndio ilikuwa jawabu. Kikawaida mtoto wa kwanza ndiye hurithi ufalme kwa Desturi ya kizamani mtoto wa kwanza ndiye alikuwa anarithi kiti cha Ufalme, Mtoto wa kwanza wa Daudi aliitwa Amnoni mama yake aliitwa Ahinoamu; Huyu aliuawa na Absalomu ambaye ni mtoto wa tatu wa Daudi kwa kosa la kumbaka Tamari(Dada yake Absalomu), Mtoto wa Pili aliitwa KILEABU, mama yake aliitwa Abigaeli, huyu naye alikufa. Mtoto wa tatu alikuwa ni Absalomu kwa mama aitwaye Maaka, huyu naye alikufa alipokuwa akipigana na Daudi Babaye ili ampoke ufalme.

Mtoto aliyefuatia ambaye mpaka Mfalme Daudi anazeeka na ndiye angepaswa achukue ufalme aliitwa Adoniya mama yake aliitwa Hagithi. Huyu kabla Mfalme Daudi hajafa ndiye alipaswa arithi kiti cha Ufalme kwa taratibu za kizamani. Na ndio maana Adoniya alipoona haoni dalili ya kupewa ufalme akaanza harakati za kuchukua ufalme.

Lakini Mungu alikuwa hajamchagua Adoniya Bali kura yake ilikuwa juu ya Suleiman ambaye Mama yake aliitwa Bathsheba, Solomoni au suleiman ni jina lililotungwa na Daudi, lakini Mungu alimpa jina liitwalo YEDIDIA yaani "Kwa ajili ya Mungu" kwa kinywa na Nabii Nathani.

Suleiman akatawazwa kuwa Mfalme kwa sababu alipewa kura na Mungu.

Tuishia hapo kwenye hiyo mifano miwili.

Kutawala kwa Mhe. Magufuli ndani ya nchi yetu, nako siwezi kuwa mnafiki kuwa mwaka 2015 kura ya Mungu ilikuwa kwa Mhe. Magufuli. Hata ukiangalia mazingira ya utokeaji wa Magufuli akiwa na visiki vya mpingo viwili ambavyo ni Mzee Edward Lowasa na Mzee Bernard Membe. Kwa hali ya kawaida hakuna aliyekuwa anamfikiria Magufuli atatawala nchi hii. Lakini Kura ya Mungu ilikuwa juu yake mwaka 2015. Magufuli hakuwa chochote mbele ya watu waliodhaniwa kuutwaa urais. Lakini Magufuli alikuwa chochote mbele za Mungu.

Lakini mwaka 2020. Mambo yamebadilika, Magufuli ameshindwa kulinda Kura ya Mungu juu yake kwa kushindwa kutetea baadhi ya haki za kuishi kwa Watanzania. Kitendo cha uwepo wa Mauaji na utekaji uliofanyika miaka hii mitano na hakuna hatua zilizochukuliwa zimeondoa kura ya Mungu kwa Magufuli. Kitendo cha Magufuli kushindwa kusimamia uhuru kwa vyama vyote kimeondoa kura ya Mungu juu yake.

Magufuli angekuwa Rais Bora kama mambo hayo mawili yangefanyika kwa usahihi. Na kura ya Mungu ingekuwa juu yake. Wala asingetumia nguvu nyingi kuomba kura awamu hii.

Na hata Huyu Lisu asingekuwa chochote kwenye uchaguzi huu. Lakini Kura ya Mungu imehama kwa Lisu na ndio maana utamuona Lisu hana nguvu yoyote yeye kama yeye lakini anapaka nguvu kwa kadiri Muda unavyoenda.

Naamini, Maandiko yangu mengi yanasomwa na watu wengi, yanasomwa na viongozi wengi,

Yeyote apataye Nafasi ya Urais, iwe Tundu Lisu, iwe Mhe. John Pombe Magufuli Lindeni kura ya Mungu kwa kujali na kutetea yafuatayo;

1. Haki za watu, ikiwepo haki ya kuishi.
Haiwezekani mtu afe au apotee kama mnyama alafu serikali ikae kimya. Hakuna Mungu atakayefurahia utawala wa namna hiyo.

2. Kutetea nchi na wananchi
Tunataka Rais atakayetetea wananchi na nchi. Kila mwananchi ni muhimu kwa taifa hili. Hakuna aliyezaidi ya mwingine. Rais lazima ahamasishe umoja na heshima kwa kila mtu. Rais atakayetetea maslahi ya wananchi na rasilimali zake.

3. Atakayetambua Uongozi ni dhamana, asitumie kama nyenzo ya kuumiza wengine.
Tunataka Rais ambaye hatajifanya mungu mtu. Tunataka Rais ambaye atakubali kupongezwa na kukosolewa. Rais wa hivi lazima atakuwa mnyenyekevu

4. Mwenye hukumu zenye haki(asiwe Double Standard)
Tunataka Rais ambaye hatakuwa na mawe mawili ya kupimia. Huyo hatatenda haki, asihukumu kwa kubagua watu, au asitoe maendeleo kwa makundi ya watu bali apende nchi na wananchi wake wote. Iwe ni CCM au CHADEMA, iwe ni Mhaya au Mkaguru, iwe ni Mkristo au Muislamu. Wote wahukumiwe kwa haki pasi na hila

5. Atakayeleta maendeleo
Maendeleo yasiwe chanzo cha kuharibu haki na utu wa watu. Na ndio maana nimeiweka hii kama sababu ya tano na sio ya kwanza. Mwanadamu baada ya uhai kitu cha pili ni uhuru, uhuru huletwa na haki, haki huleta amani, amani ndio huzaa maendeleo.
Tunataka Rais atakayeweza kutuletea maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiutamaduni na kifikra.

Mpaka sasa, Kura ya Mungu ipo na Tundu Lisu, hata kama wananchi hawatampa kura Lisu za kutosha kumfanya Tundu Lisu awe Rais, basi hii itamfanya MAGUFULI kama anahekima kujifunza mambo mengi ambayo naamini yatambadilisha kwa sehemu Kubwa.

Magufuli endapo utashika nafasi ya pili, jitahidi utumie nafasi hiyo kama njia ya kujisafisha mbele za Mungu, muombe Mungu msamaha kwa kushindwa mambo niliyoyataja hapo juu. Naamini unaelewa ninachokisema; usijejifanya kiburi kwa maana unafahamu fika umri ulionao kwa sasa ni mkubwa, ni umri wa kufanya matengenezo, umri wa kutubu. Umri wa kumaliza na Mungu.

Lakini ukijifanya jeuri ukatenda kwa kiburi basi fanya zaidi na zaidi kwa kadiri ya jeuri yako itakavyo kutuma. Lakini ukae ukijua hauna muda tena, nawe sasa ni mtu mzima.

Nawe Lisu, kama utapata kibali cha kuongoza nchi hii, Usije kutenda kwa hila, wala usijelipa kisasi, kwa maana kisasi hufanywa na waovu, bali muachie Mungu ndiye ajuaye.

Magufuli usijekuwa kama Mfalme Sauli alipokataa kuachia Ufalme kwa Daudi, akasahau hata yeye aliwekwa na Mungu na sasa huyo huyo aliyemweka ndiye anataka kumuengua. Kama utashindwa kihalali, muachie Lisu atawale. Nawe utakuwa kama Musa alivyolilia kufika Kanani lakini Mungu akakataa, akamuachia Joshua.

Lissu anaweza kuwa Joshua wa Magufuli. Lissu anaweza kuwa Daudi, na Magufuli akawa kama Sauli.

Nawe Lisu kama utapata nafasi ya kutawala uwe kama Mfalme Daudi, ambaye baada ya kuchukua Ufalme hakutaka kumlipa kisasi Mfalme Sauli aliyetaka kumuua.

Jamani andiko hili limekuwa refu sana, hata hivyo nimelifupisha mno, kwani yapo mengi niliyotaka kuyasema.

Kwa habari ya kura yangu, nitampa Tundu Lisu, lakini hata kama akishindwa sitamchukia Magufuli, nitamsapoti kwa yaliyo mema na nitampinga kwa mabaya. Hata Lisu naye kama atapata utawala nitamuunga kwa mema lakini kwa mabaya sitomnyamazia asilani.

Itoshe kusema; Tupendane, kwa maana wote wapendanao ni watoto wa Mungu.

Ulikuwa nami:

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Huyu Mungu mnaemzungumzia sijui ni Mungu yupi maana naona ccm inamzidi maarifa huyo Mungu kwenye kila uchaguzi,ngoja uchaguzi uishe sijui huyo Mungu nae atalalamika kuibiwa kura yake ama sijui vp?
 
Kwa Tanzania bara nina uhakika Upinzani haujawahi kushinda kwa nafasi ya Urais.

Labda wizi huko kwenye nafasi ya ubunge. Vyama vya upinzania kushinda nafasi ya Urais itakuwa muujiza.

Hata Huyu Lisu kama atashinda, nitaona ni maajabu ya dunia kama alivyopona hizo risasi
 
Kosa lingine kubwa la Magufuri ni kuruhusu yeye kuabudiwa kutukuzwa ; ,kupewa sifa,kuimbiwa hadi kuitwa Yesu.

Nkwame Nkuruma nae aliruhusu Raia wa Ghana wautafute kwanza ufalme wa Ghana na haki yake ndipo watakapoongezewa baada ya kutafuta ufalme wa Mungu.

Magufuli nae ametaka yeye asikosolewe kama Mungu, asishauriwe, Asisemwe kwa mabaya nk.

Magufuli amejipa sifa za Mungu.
Akajiahau kwamba yeye ni Mwanadamu hadi bingu imemkataa
 
Kwa hili bandiko lako unastahili kuitwa Taikoni

Umesema sawasawa na ukweli mtupu
 
Nimependa sana jinsi ulivyochambua masomo haya ya kibiblia hakika uko vyema sana.

Kwa nyongeza tu Magufuli amekuwa kama Mfalme Sedekia alionywa sana na Nabii Yeremia juu ya kufungamana na makahaba( manabii wa baal) laakini hakusikia. Hata Yeremia anamwabia mzee kuwa makini saana Mungu kanituma nikwambie ujirekebishe mienendo yako haiko swa? Sedekia alidharua mpama siku anatobolewa macho na wanaye kuchinjwa mbele yake.
 
Leo umemgeuka ndugu yako. Anga limemkataa amepoteza kibali toka kwa Mungu amepimwa hatoshi.
Amepewa kondoo awalishe anawapoteza amemkosea hata Mungu
 
Lisu Hana mabango Hadi chooni Wala matangazo lkn kila mahali watu wanamfuata. Lisu ndie mtetezi halisi Tena kwa vitendo na sio majukwaani wa wanyonge. Alijitolea bure kuwatetea bure watz 250 wamiliki wa maeneo ambayo Mkapa alitaka kuwapora kibabe wakaidi waliobambikwa kesi wafungwe maisha lkn aliwatoa bure jela. Tangu akiwa shuleni amepinga Sana watu kuonewa, amewatetea watz wengi waliozulumiwa haki zao na Utawala huu dhalimu bila hata sent na akawashindia.
Sifa za raisi Bora Ni lzm atokane na fani ya sheria, diplomasia, uchumi au biashara hizi fani zinahitaji reasoning tofauti na fani ya sayansi inahitaji claiming capacity. So Lisu Ni mtu sahihi Ni mtanzania mwenzetu halisi pa Sina shaka ya uraia wake hawezi umiza watu.
 
Hizo mkuu ni stress tu,huyo Mungu hajaanza leo kuhusishwa na wagombea urais wa upinzani.

Mara ngapi Mungu anahusishwa na Magufuli?

Nakubali kabisa Magufuli 2015 alipita kimungu mungu, na ndio maana nikasema Kura ya Mungu ilikuwa juu yake.

Sipo hapa kumtetea yeyote, sina maslahi na yeyote, iwe huyo Lisu au Magufuli.
 
Lisu Hana mabango Hadi chooni Wala matangazo lkn kila mahali watu wanamfuata. Lisu ndie mtetezi halisi Tena kwa vitendo na sio majukwaani wa wanyonge. Alijitolea bure kuwatetea bure watz 250 wamiliki wa maeneo ambayo Mkapa alitaka kuwapora kibabe wakaidi waliobambikwa kesi wafungwe maisha lkn aliwatoa bure jela. Tangu akiwa shuleni amepinga Sana watu kuonewa, amewatetea watz wengi waliozulumiwa haki zao na Utawala huu dhalimu bila hata sent na akawashindia.
Sifa za raisi Bora Ni lzm atokane na fani ya sheria, diplomasia, uchumi au biashara hizi fani zinahitaji reasoning tofauti na fani ya sayansi inahitaji claiming capacity. So Lisu Ni mtu sahihi Ni mtanzania mwenzetu halisi pa Sina shaka ya uraia wake hawezi umiza watu.
Hawa watu wangekuwa wanamfuata Lissu tu na kujazana huko hapo ndio tungewaelewa ila ajabu watu hao hao ndio wanaenda pia kujazana kwenye mikutano ya ccm na kuburudika muziki,hawa watu bado hawajielewi na hivyo wingi wao hauna maana yeyote maana ni kama watu washamba tu waliyokosa kazi wakati huo na ndio wanaenda kujazana kwenye mikutano ya kampeni.

Wakitoka hapo kwenye kampeni wahoji kama wameelewa hizo sera zilizozungumzwa ndio utajua hakuna kitu kabisa hakuna wanachoelewa.
 
Tatizo la magufuli ni kiburi, dharau na ujuwaji mwingi.me nilimshangaa alipoanza kusimama makanisani na kuanza kuhubiri nikajuwa kuna anguko kubwa.
 
Hawa watu wangekuwa wanamfuata Lissu tu na kujazana huko hapo ndio tungewaelewa ila ajabu watu hao hao ndio wanaenda pia kujazana kwenye mikutano ya ccm na kuburudika muziki,hawa watu bado hawajielewi na hivyo wingi wao hauna maana yeyote maana ni kama watu washamba tu waliyokosa kazi wakati huo na ndio wanaenda kujazana kwenye mikutano ya kampeni.

Wakitoka hapo kwenye kampeni wahoji kama wameelewa hizo sera zilizozungumzwa ndio utajua hakuna kitu kabisa hakuna wanachoelewa.
Ipo tofauti kwa ccm wamepooza Ni Kama wamelazimishwa kuwepo pale baada ya fiesta walikuwa wakiondoka awangojei kusikia sera za mgombea wa ccm thus siku hizi wanawekewa uzio ili wasitoroke baada ya kuangalia wasanii,pia wanaoshangilia au kuinua mikono huwa ni wachache,. Kwa upande wa Lisu huwa amshaamsha furaha, hamasa kuinua mikono akisema wangapi mtanichagua karibu wote wanajaa bila fiesta Sasa hapa ujapata tu jibu. Mbona kwa lipumba, mbatia awajai vile. Ukishindwa kusoma hata picha zinajisoma. Watu wanataka mabadiliko.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom