Kura ya maoni zanzibar na muelekeo mpya wa kisiasa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kura ya maoni zanzibar na muelekeo mpya wa kisiasa tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fungu la kukosa, Aug 2, 2010.

 1. F

  Fungu la kukosa Member

  #1
  Aug 2, 2010
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote napenda kuzipongeza serikali zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais J.M.Kikwete na DR Karume kwa maamuuzi yao yaliyoshehena hekima na busara kwa kuwapa fursa wa Zanzibar kujiamualia wao wenyewe muundo wa serkar waitakayo katika siku zijazo baada ya uchaaguzi mkuu wa Marais na wabunge hapo mwezi wa kumi mwaka huu.
  Kwa maoni yangu binafisi kitendo hicho cha ashiria kukomaa kwa kiasi fulani kisiasa na kidemocrasia kwa vingozi wetu wa serkali-Bara na Visiwani. Hata hivyo maamuzi haya yamechelewa kufanyika kwa kiasi fulani. Viongozi waliotangulia walipaswa kufanya maamuzi kama hayo kabla ya wao kunga'tuka ili kutengeneza mising mizuri ya kidemokrasia kwa viongozi wajao baada yao. hata hivyo hapana budi kuwashukuru viongozi wetu kwa hatua hiyo waliofikia si haba, kwani maamuzi hayo yamefanyika katika kipindi haswa muafaka kwa Wazanzibar haswa ikitiliwa maanani karibu nusu ya Wazanzibari hawana imani tena na serkar ya CCC na badala yake wahitajia aina fulani ya mabadiliko ya kisiasa ndani ya nchi yao.Lakini kwa maoni yangu kuna jambo moja kubwa lililosahaulika katika kufikiwa kwa maamuzi hayo.
  (1) Kudhania kuwa haki ya kidemokrasia inahitajika zaidi visiwani tu na si Bara.
  Kwa mtazamo wangu wapinzani wa CCM si Maaduwi wa Tanzania bali ni wenyekuitakia kheri Tanzania na wananchi wake wote kwa ujumla. Hivyo kura hiyo ya maoni ilipaswa kufanyika na Tanzania Bara pia.
  (2) Serkali Mseto kwa Tanzania nzima na si kwa Zanzibar peke yake
  Swala la serkali ya mseto kwa Tanzania nzima ndiyo suluhisho muafaka la uwozo ulioshamili ndani ya serkali zote mbili na hususan ndani ya Bunge na Baraza la mapinduzi Zanzibar. Kumekuwepo na hali ya Mfumo Dume(Domination of opinion by the ruling party(CCM) MPs over the opposition) hata kama kinachoelezwa na wapinzania ni ukweli mtupu na wenye maslahi kwa wananchi;-Maspika wa Bunge la CCM na LILE LA Baraza la Mapinduzi LA zNZIBAR;-kwa makusudi wamekuwa wakizuwia hoja hizo kwa lengo la kuudhofisha upinzani na kuhalalisha ufisadi ndani ya nchi yetu. Kwahivyo, kwa kuwepo kwa serkali za mseto bara na Visiwani kutasaidia kuwepo kwa kile kiitwacho Balance of Power: Viongozi wa serkari toka upinzani watakuwa na fursa kubwa ya kukemea na hata kuzuwia uozo huo wa kisiasa. Kwa mfano ikiwa uozo utatokea kufanyika ndani ya wizara ya mambo ya ndani iliyo chini ya waziri toka CCM, Wabunge na Mawaziri wengine toka upinzin watakuwa na fursa ya kusema NO WAY FOR SUCH KIND OF STUPIDITIES TO OUR COUNTRY!!. Halikadhalika kwa mawaziri toka chama cha CCM watakuwa na fursa ya kufanya hivyo pinde mawazir wenzao toka kambi ya upinzani wataboronga.Sera ya CCM ya kulinda hata kama hapana ulazima wa kufanya hivyo sasa itakuwa imefikia kikoma chake.
  Kwa sasa hivi wananchi Bara na Visiwani shida yao kubwa ni maendeleo;- kwa maana ya kuwapatia huduma zote muhimu za kijamii kama vile ;- Afya, Elimu bora na si bora elimu, Usafiri wa kutegemeka(reliable transport), na si kuwa na mabehewa ya train na engines zi sizifanya kazi kikamilifu au sanamu za ndege zilizotelekezwa pale airports, Maji safi na salama, Mawasiliano, Ajira endelefu na si bora ajira. na kuimarika kwa sekta za kibiashara,kilimo, madini na nishati,viwanda na hata michezo.HAYA NDIYO HASWA MATAKWA YA WATANZANIA KWA WAKATI HUU WA KARNE YA 21 NA SI VINGINEVYO.
  Kwa hivyo,kwa muono wangu binafisi serkali za mseto Tanzania itakuwa ni hatua madhubuti ya kuelekea kwenye demokrasia ya kweli itakayojaribu kupunguza kwa kiasi fulani uozo wa siasa ndani ya Tanzania na kuwa chachu ya kuwaletea wananchi mahitajio hayo yaliyotajwa hapo juu.
   
 2. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu tatizo kwetu ni moja tu, upinzani bado uko week!!

  Laiti tungekuwa kama ZNZ, kwamba mshindi wa pili kwenye kiti cha uraisi asingalikuwa mbali na wa kwanza, hapo kweli. Ukiangalia matokeo ya 2005, utelewa hili. Ushindi wa Kikwete ulikuwa zaidi ya 80% anayemfuatia less that 50% (kama nakumbuka vizuri). Hii inawapa nguvu CCM kuunda serikali wao maana ushindi uko wazi tu.

  Natumaini OCT 2010 tutasikia tofauti maana mambo yamebadilika.
   
Loading...