Kura ya maoni ya katiba mpya huenda isifanyike!

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,796
12,239
Kuna vuguvugu kubwa la kisiasa linaloendelea nchini ambalo lengo lake ni kuhakikisha kuwa bunge la katiba halipitishi rasimu ya katiba! Ili rasimu ya katiba ipitishwe kunahitajika theluthi mbili za wajumbe kutoka kila upande wa muungano kuikubali na kuipigia kura ya ndiyo pamoja na marekebisho yake!

Baada ya CCM kushindwa kushawishi kuendelea na serikali mbili katika rasimu ya katiba, baadhi ya makada wake wa Tanganyika na Zanzibar wameanzisha harakati za chini kwa chini ili baadhi ya wajumbe wake watakaokuwa katika bunge la katiba waikatae rasimu hiyo na hivyo kusababisha idadi ya theluthi mbili isifikiwe ama kwa wajumbe wa Tanganyika au wa Zanzibar! Baadhi ya makada wanaoendesha harakati hizo ni mawaziri wa serikali zote mbili, wenyeviti wa CCM wa mikoa na wilaya, wabunge na wajumbe wa baraza la wawakilishi na wajumbe wa NEC!

Endapo harakati hizi zitafaulu na rasimu kushindwa kupitishwa basi kura ya maoni haitafanyika na tutaendelea na katiba iliyopo kama Rais JK alivyosema wakati akipokea rasimu ya pili ya katiba!
 
Wazanzibari wanahitaji kupumua Hilo haliwezekani.theruthi itapatikana wala usihofu,Ccm tayari wamepigwa bao.chezea Cdm na mikakati
 
Wazanzibari wanahitaji kupumua Hilo haliwezekani.theruthi itapatikana wala usihofu,Ccm tayari wamepigwa bao.chezea Cdm na mikakati


Hapo kwenye red ufafanuzi tafadhali! CDM ilikuwa na ushawishi wote katika kupatikana kwa rasimu iliyopatikana? Kama ndivyo, ni ushawishi upi?
 
Back
Top Bottom